VITUKO VYA Juma Pondamali

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,706
155,284
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikisikia visa na vituko mbalimbali vya golikipa maarufu wa yanga na taifa stars Juma Pondamali.

Nasikia amewahi kuudaka mpira na kuuficha watu wakabaki wanashindwa kuelewa ni goli limeingia au la...

Pia nimeshawahi kusikia amewahi kuudaka mpira kisha akamrushia kwa makusudi adui, adui alipopiga akadaka kisha akamrushia tena...

Je hivi visa ni vya kweli, au ndio yalikuwa magirini ya kitoto?

Kama ni kweli naomba nijulishwe pia nipewe habari zake zaidi kwani amekuwa ni kivutio kikubwa sana kwani alikuwa na kipaji cha hali ya juu sana.
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikisikia visa na vituko mbalimbali vya golikipa maarufu wa yanga na taifa stars Juma Pondamali.

Nasikia amewahi kuudaka mpira na kuuficha watu wakabaki wanashindwa kuelewa ni goli limeingia au la...

Pia nimeshawahi kusikia amewahi kuudaka mpira kisha akamrushia kwa makusudi adui, adui alipopiga akadaka kisha akamrushia tena...

Je hivi visa ni vya kweli, au ndio yalikuwa magirini ya kitoto?

Kama ni kweli naomba nijulishwe pia nipewe habari zake zaidi kwani amekuwa ni kivutio kikubwa sana kwani alikuwa na kipaji cha hali ya juu sana.
Kama unaweza kupata gazeti la tarehe 9/11/09 la mwananchi kuna makala yake amehojiwa na mwaandishi ameelezea vituko vyake vyote! hivyo hapo ulivyosema ni kweli na sio stori....hiyo ishu ya kudaka mpira na kuuficha ilisababisha akapwewa kadi ya njano kwani refa alijua ni goli!!
 
nasikia kuna wakati alirudisha mpira baada ya kuudaka na jamaa kafunga goli.watu walitaka kumshushia kipondo lkn kwa vile Juma Pondamali alikuwa baunsa kawakomalia na wakafyata mikia.........
 
Pondambali hakuwa baunsa bali alikuwa gangwe.

Lugha tu ndugu,mi nimekulia s'wanga watu hawa tuliwaita baunsa wakati wetu....nawe wamwita gangwe....
sie wakati ule magangwe tiliwaita watu ambao leo hii unaweza kuwaita wasela....
 
Ninawasiwasi wewe unaweza kuwa babu,maana hili neno la gangwe walitumia babu zetu!!
mchajikobe kwa ku assume wewe!

Kwakuwa amesema neno la zamani wa assume kuwa huyo ni Babu. Nawe ukiulizwa Vita vya majimaji vilipiganwa lini, ukijibu tukuite Kikongwe eti?
 
Pondamali.jpg


alikuwa mbabe huyu
 
Katika miaka yake ya mwisho katika soka, alipenda sana ugomvi...! Nakumbuka mechi moja kati ya Pan na Majimaji, iliyofanyika katika uwanja wa Majimaji Songea. Alianza kwa kupiga push up mbele ya mkuu wa mkoa wa wakati huo.. na vituko vingine kadhaa

Pan walipojikuta wakifungwa goli la tatu, Peter Tino na Juma Pondamali walimvaa refa na kumpiga kisawasawa kiasi cha FFU kuingilia kati. Hata hivyo Pondamali aliweza kuwatoka FFU hao na kuendeleza kipondo kwa refa huyo.

Vurugu hiyo ilisita baada ya FFU wengine zaidi kuingia uwanjani huku wakipiga mabomu ya machozi...
 
Huyu jamaa bangi ilikuwa imekaa sawa hata sasa kwani kuna kipindi alikuwa anahudhi sana nakumbuka mechi moja uwanja wa taifa (uhuru sasa) kati ya yanga na Pamba huyu bwana alifungwa goli la kizembe ila alikuja juu na kumkaba koo beki wake Fred Minziro pale alipolalamikia uzembe huo. Sio mtu wa kuigwa.
 
Huyu mthenge watu sijui walikuwa wanamwogopea nini? Ana bahati nilikuwa dogo enzi zake
 
..kwa kweli Pondamali alikuwa burudani ya aina ya pekee.

..mashabiki wa mpira wa Nigeria wanaamini kwamba Pondamali ni kati ya magolikipa wenye ndumba kali waliopata kutokea Africa.

..Pondamali alikwenda Nigeria na Taifa Stars, halafu baadaye alirudi tena na Pan African walipocheza na Ibadan Shooting Stars.

..Wazambia nao bado wanamkumbuka Pondamali maana yeye ndiye alikuwa kikwazo kikuu cha Wazambia kutokwenda Nigeria kwenye kombe la Afrika.

..kwa kweli huyu hakuwa mcheza mpira tu, bali ni INTERTAINER. ulikuwa unaweza kwenda kwenye mechi, ukapoteza muda kuangalia vituko alivyokuwa akifanya Pondamali, badala ya mechi inayochezwa.
 
jamaa alikuwa 'gangwe' haswa..
niliwahi msikia dhahiri akimfokea golikipa wa timu moja ya mchangani aliyokuwa akijitolea kuifundisha(miaka kadhaa baada ya yeye kuacha kucheza),'we golikipa gani sijawahi sikia hata siku moja umempiga foward ngumi ya shingo wakati wa kuokoa kona,gangamaa'...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom