Vituko vya Bongo: January Makamba Apata "verified Twitter accounts" kabla ya CCM, Ikulu na JK

Game Theory I

Member
Nov 28, 2011
32
8
Success.png

Nimeibamba hii kwenye account ya Makamba Fesibuku. Imekaaje wadau? Hizi badge huwa wanapewa viongozi na taasisi kubwa katika mtandao wa Twitter. Naona jamaa kapata kabla hata ya CCM (ambao wako Twitter). A man popular and important than the party? Kama kuna wasomi CCM hebu nifafanulieni hili.

Heshima mbele

GT I
 
Sioni tatizo hapo, give the guy credits he deserve for being ahead of the party.

Kama chama hakijiongezi haimaanishi watu wengine msubiri hadi chama au ikulu ianze. Website ya Ikulu yenyewe ku update ni mgogoro. Big up JM
 
[h=2]January Makamba si wa kwanza kupata "verified Twitter accounts" kabla ya taasisi fanya utafiti mdogo wala haitakushangaza. Taasisi ndio zilizowajenga watu hivyo hivyo January amepata verify kwa kuitumikia taasisi lakini kama angekuwa nje ya taasisi ni jambo tofauti. Mimi napata shida ninapoona mtu anapata verify nje ya taasisi akiwa peke yake na nampongeza. Nani angemjua Jk bila CCM kumjenga?[/h]
 
Nani angemjua January Makamba bila Ikulu na Bunge?

Ukipata uprofesa ni dhihaka kusema kwa nini mwalimu wako bado ni mwalimu wa shule ya msingi bila kukiri kwamba yeye ndiye kakufikisha juu.

Mwalimu wa shule ya msingi anakufundisha na hatimaye unaweza kuwa profesa baadaye wakati yeye bado ni mwalimu wa shule ya msingi.

Jambo kubwa hapa ni kwamba mwalimu huyo ndiye kakupa msingi wa kufika uprofesa.
 
1st you have to be a public figure. 2nd There has to be a fear of impersonation na conditions nyingine.
 
Umeona swali nimeulizaje? Kwa nini hizo taasisi kubwa zilizomjenga ulizozitaja hazijafikia hatua hiyo aliyofikia yeye?
 
Na ufanye utafiti ziko accounts ngapi verified katika Afrika kwenye Twitter halafu uongee tena.
 
View attachment 49866

Nimeibamba hii kwenye account ya Makamba Fesibuku. Imekaaje wadau? Hizi badge huwa wanapewa viongozi na taasisi kubwa katika mtandao wa Twitter. Naona jamaa kapata kabla hata ya CCM (ambao wako Twitter). A man popular and important than the party? Kama kuna wasomi CCM hebu nifafanulieni hili.

Heshima mbele

GT I

Slaa, Mbowe na CHADEMA wameshapata?
 
Wagosi wa BUMBULI UKIWAAMBIA "twitter" wanadhani unawatukana, wao wanataka maji, elimu bora, maisha nafuu, barabara na usalama wao na mali zao..hizi nyingine ni mbwembwe tu!
 
Tunaongelea nje ya jimbo lake pekee? Kwa hujui jamaa ana SMS program kati yake na WanaBumbuli? Aki= integrate anaweza kuweka mchezo mzima katika platform moja. Amka mbimbio. Swali langu ni je, walio juu yake au hata vyombo vya habari kama IPP mbona wasitume hayo maombi na wakafanyiwa hivyo?! Miafrika!
 
Back
Top Bottom