Vitu nisivyovipenda nikiwa naendesha.

Sipendi wakati naendesha mbele yangu kuwe na roli la taka,then while mm nakereka na harufu wale vijana wako pale juu taratiiiiiiibu wanakula bila shida!poor them,naona huruma sana
sipendi mwendesha pikipiki awe mbele yangu.
Sipendi tabia ya taxi kuchomekea bila sababu ya msingi,
sipende bajaj zinavyoendeshwa.
Sipendi guta wanavyong'ang'ania kutumia barabara kubwa wakati service roads zipo.
 
yani utatamani kulia guta wanakaa katikati ya barabara na usijeukakosea likakugonga linaumiza gari kweli

imaging guta katikati, pembeni baiskeli or pikipiki mbele daladala limechomeka khaa


Jamani acheni ubishololo badala ya kumhurumia uliyemgonga unahurumia kimtumba chako kipi bora mwendesha guta au hako ka kobe kako hata gharama yake inakaribia kulingana na ya guta acheni hizo huo ni ulimbukeni.
 
Sipendi wakati naendesha mbele yangu kuwe na roli la taka,then while mm nakereka na harufu wale vijana wako pale juu taratiiiiiiibu wanakula bila shida!poor them,naona huruma sana

Hupendi roli la taka wakati huenda hizo taka zinatoka nyumbani kwenu wakiacha kuzoa si mtavunda kwenu.
 
-Sipendi mtu kuchomekea mbele yangu
-Sipendi lori au yale mabasi ya mikoani kuwa nyuma ya gari yangu.
 
mimi sipendi kupigiwa 'horn' au usiku kumulikwa na flashi lights!
 
Mie sipendi watu wanaoendesha taratibu below speed limit na wakati mwingine dreva huwa anaongea na wasafiri wake humo kwenye gari, na aliyenifundisha gari aliniambia kwamba horn haikuwekwa ndani ya gari kama pambo ama kuwasalimia washikaji, bali ni kuwaonya madreva ambao kwa namna moja au nyingine wanafanya mambo ambayo hawastaili kuyafanya barabarani ambayo yanaweza kabisa kusababisha ajali. Siwapendi kabisa waendesha pikipiki na Baskeli wanaotaka kujitandaza barabara yote kama vile wamekodisha barabara hiyo. Siwapendi wale wanaotaka kufanya mashindano barabarani kuonyesha gari yao ina speed kubwa kuliko yangu, siku nikiamka vibaya huwaonyesha kwamba wasipende kushindana nami, najua haya ni makosa, lakini hey I am human and therefore I am not perfect. Sipendi watu wanaondesha huku wanakula, wanapaka wanja au lipstick, wanaongea kwenye simu au wanatuma text messages. Nikiwagundua huwa nawakimbia haraka sana maana hawa mara nyingi husababisha ajali barabarani. Ni dreva mzuri sana sijagonga hata panya buku barabarani :)...LOL!
 
Kwa mtako wako ni kuwa hutaki wawepo watumiaji wengine wa barabara ambao kimsingi ni wadau halali wa barabara.we ni mwoga na udereva wako unatia shaka.ushauri wa bure rudisha leseni then ajiri dereva akakongoroe kimkoko chako sikt mbili mbali au nione nikujuvye mbinu na medani za barabarani vingine utakuwa m2 wa lawama kila cku:cool:
 
waendesha baiskeli....jamaa wanakera sana wale, ustaarabu zero barabarani
 
Sipendi mwendesha pikipiki awe mbele yangu.
Sipendi tabia ya taxi kuchomekea bila sababu ya msingi,
Sipende Bajaj zinavyoendeshwa.
Sipendi guta wanavyong'ang'ania kutumia barabara kubwa wakati service roads zipo.

Vipi mdada akinengua kiuno barabarani wakati umemruhusu avuke barabara badala ya angalau kuchechemea kuonyesha shukrani? Au akisimama barabarani kusubiri daladala huku anajua kabisa ni hatari, ukimwonya asogee nje atagongwa anakubetulia mdomo kukudharau na kukuambia "unajifanya wewe kidume? Kwani huna macho mshamba wewe?"

Jamani, utadhani alitamani asiuone mwaka mpya na sasa analazimisha asiumege hata nusu mwaka!!

Leka
 
Mfamaji, kama wewe hujawakodolea macho yako umejuaje wao wamekukodoale?????!!!!! uliwakodolea na wao wakakukodelea eboooooooo
 
Back
Top Bottom