Vitisho vya serikali ya awamu ya nne kwa watu wake

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,270
533
Maandamano yanapingwa kwa nguvu zote na kujaribu kuaminisha watu kuwa yataleta vurugu na uvunjifu wa amani.
Wanafunzi vyuo vikuu wasiulize swali lolote hasa kuhusu mambo yasiyoenda vizuri "Wewe si umekuja kusoma? Umekuja kufanya siasa hapa? Mnatumiwa tu na wapinzani" Ndiyo hoja ambazo hutolewa ili kumnyamazisha mnyonge asiseme lililo moyoni mwake. Kama jina lako limeandikwa kwa penseli (si mwenzetu au mtoto wa mwenzetu) basi huna haki ya kuzungumza lolote mahali popote. Wanafunzi wakitaka waitishe maandamano ya kuusifu utawala uwe wa chuo au wa serikali, basi vibali vitatolewa hapohapo.

Hizi ni dalili za serikali fisadi, uongozi fisadi nk. Katika wote waliofukuzwa hakuna hata mmoja aliyemtoto wa kigogo (yaani mtoto wa mtu mwenye jina). Wale watoto wa vigogo wao hupewa mikopo bila ya maswali...watoto wa mlala hoi mpaka aipate!!!!

Kuna tatizo hapa ndugu zangu ambalo ni lazima tulione kwa haraka. Mbona ni rahisi kupambana na wanaodai haki lakini si rahisi kupambana na mafisadi? Ningelifurahia kusikia wale wanaokula rushwa wanafukuzwa mara moja kama wale walioandamana kudai haki ya kutoa ujinga. Kinyume chake, virungu kwanza, vitisho, kufukuzwa, ili na wengine wasije wakadai tukaonekana hatuwapi haki zao...Huu nao ni ufisadi.
Nawasilisha.
 
Hiii post yako kila nikiisoma natamani hata kulia. Hebu usiweke tena post kama hii naweza kumuiga yule kijana wa Kitunisia
 
Cha kufanya mnakijua! wabongo woga mtaacha lini? Born free but living in bondage....break the shackles!
 
Back
Top Bottom