Vitisho vya Mwigulu vyamng'oa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya

CHADEMA wana kazi kubwa huku Iramba Magharibi. Miezi miwili iliyopita Mwenyekiti wa Wilaya wa CHADEMA alibambikiziwa uchawi nyumbani kwake huko Kijijini Kisana. Wanakijiji wakakusanyika na kutaka kumpiga akakimbia. Tangu kipindi hicho amekuwa akijificha. Watu walidai kipindi hicho kwamba mpango ulisukwa na Mwigulu ili kumchafua na kuharibu taswira ya CHADEMA kwa kuonyesha kwamba viongozi wa CHADEMA ni wachawi! Watu hawakuamini sana.....

Chadema can fix that by electing a real an m4c guy na inakuwa jibu kamili am sure wako wengi wanajuana so go Iramba go
 
CHADEMA wana kazi kubwa huku Iramba Magharibi. Miezi miwili iliyopita Mwenyekiti wa Wilaya wa CHADEMA alibambikiziwa uchawi nyumbani kwake huko Kijijini Kisana. Wanakijiji wakakusanyika na kutaka kumpiga akakimbia. Tangu kipindi hicho amekuwa akijificha. Watu walidai kipindi hicho kwamba mpango ulisukwa na Mwigulu ili kumchafua na kuharibu taswira ya CHADEMA kwa kuonyesha kwamba viongozi wa CHADEMA ni wachawi! Watu hawakuamini sana......
Mkuu Mwigulu kazi yake ni kusafisha wachawi?
 
duh...si utani ..mwigulu kweli ni mwigulu
Mkuu, haya tuliyategemea. kilichopo ni kwamba, tutakula nao sahani moja mpaka kieleweke. huu upuuzi wa mwigulu wala hata usikubabaishe, tunamlia timing, muda ukifika huyu jamaa ni mwepesi mno. acha abwate na hizo pesa zake za kifisadi, atawahonga mpaka lini??? halafu ajue huwezi kununua roho ya mtu, hao wanazitumbua tu, ila nyoyoni mwao wapo na CDM.
 
Mwana gwanda wa kweli hanunuliwi na pesa za ufisadi. Bora alivyojionyesha mapema kama yeye ni gamnba. Watu kama hao hawatakiw I cdm.cdm sio ya maslai binafsi ni ya nguvu ya umma. Mwambieni aendeeee hatuhitaji watu kama hao.
 
huyu Chemba ni mpuuzi saaana! Ngoja niku PM namba za viongozi
Mkuu tatizo sio CHEMBA,tatizo ni wana ilamba bado wanaitaji kuelimishwa waichukie RUSHWA waipende TANGANYIKA yao.Huu ni UDHAIFU mkubwa kwa wana ilamba kuendelea kurubuniwa na hii ni ishara kwamba mapambano yakulikomboa taifa letu kutoka mikononi mwa WAKORONI weusi nikubwa.Mungu ibariki TANGANYIKA.
 
Du hii mbinu kali ngoja Josephine aje atajua km IMEBIDI ni Mwigulu mwenyewe,
Pili nachosema huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote iko siku watakudanganya na hutaamini kuwa wameku-kula KISOGO
 
Huyu mwingilu anatakiwa azibitiwe na watu wasio ogopa vitisho vya aina yoyo kama marehem Chacha Wangwe(R.I.P)
 
Achana nae huyo Katibu,,kama c nafsi inayomtuma kuwa CDM bali mambo ya pesa hawafai CDM na wapenda mabadiliko wote!
 
Hapo ndio mjifunze kuwa watanzania ni walewale na usitegemee kuna chama cha siasa kitakachokomboa maisha yako. Kazi ya chama cha siasa ni kujenga mazingira ili wewe uchakarike na utoke. Kama huoni mazingira ya kutoka wakati wenzako wanayaona basi ujue mwenye tatizo ni wewe sio chama cha siasa.
 
Huyo mwenyekiti na katibu wake bora wakaondoka kuna team mpya iliyokaa sawa from ARUSHA inakuja kukaba hapo Mwigulu kaa tayari kama unaweza kweli coz umewezeshwa tu wewe
 
Watu wa aina hiyo wako wengi na ndio sababu mojawapo ya Chadema kuja na utaratibu mpya wa kusimamia na kuendesha zoezi la uchaguzi waq viongozi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya misingi. Sitarajii kuona hawa waganga njaa wakiendelea kupata nafasi za uongozi.
 
Watu wa aina hiyo wako wengi na ndio sababu mojawapo ya Chadema kuja na utaratibu mpya wa kusimamia na kuendesha zoezi la uchaguzi waq viongozi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya misingi. Sitarajii kuona hawa waganga njaa wakiendelea kupata nafasi za uongozi.

Hata mimi naamini hivyo. Lakini bado najiuliza Nchemba amerithi wapi uwezo wa kumsafisha mtu mwenye tuhuma za uchawi!?
 
Tusimlaumu mwigulu ambaye kazi yake ni siasa,tumlaumu mwenyekiti alieamua kwa akili yake mwenyewe kurudi kundini.

Mkuu, mimi niko tofauti kidogo na wewe. Nadhani si vema kumlaumu huyu mwenyekiti na huyo mwingine anayesemekana anataka kurejea CCM.
Ni swala la kushukuru kwamba wamejipambanua wenyewe mapema kabla hawajaleta madhara makubwa kwa CDM katika kipindi nyeti kama za uchaguzi mkuu wa 2015.

Wapenda CDM halisi ni wale ambao badala ya kupokea pesa kutoka CDM wao huchangia japo Tsh. 350/= kwenye M4C, au wale ambao japo hawana kitu cha kuchangia lakini wanayaona machungu ya umaskini wao ambao wanajua chanzo chake ni nini.
 
Askari na usalama wa Taifa wanashindwa kuunganisha dots kwamba mwigulu ni mtu wa namna gani? Kama wameweza kutumia video clip iliyotundikwa you-tube wanashindwa kutumia social media kama Facebook, JF, you-tube, twiter na TV kujua mwigulu ni mtu wa namna gani!
CHADEMA wana kazi kubwa huku Iramba Magharibi. Miezi miwili iliyopita Mwenyekiti wa Wilaya wa CHADEMA alibambikiziwa uchawi nyumbani kwake huko Kijijini Kisana. Wanakijiji wakakusanyika na kutaka kumpiga akakimbia. Tangu kipindi hicho amekuwa akijificha. Watu walidai kipindi hicho kwamba mpango ulisukwa na Mwigulu ili kumchafua na kuharibu taswira ya CHADEMA kwa kuonyesha kwamba viongozi wa CHADEMA ni wachawi! Watu hawakuamini sana.

Sasa mhe Mwigulu amerudi juzi Bungeni na ameanza mikutano katika Jimbo lake. Juzi Mwenyekiti aliitwa akaambiwa kama anataka atulie nyumbani aache kutangatanga kama kunguru arudishe majeshi na yeye Mwigulu atamsafisha kwa sababu mpango mzima anaujua. Kweli, kijana wa watu amejisamisha leo kwenye mkutano na kutangaza kwamba, kwa maneno yake, 'anarudi kwa baba'. Kwa hivyo Mwenyekiti wa Wilaya wa Iramba Magharibi, Bwana Sembe, leo amesalimu amri kwa vitimbi vya Mwigulu na kukamata kadi ya magamba.

Nawapa angalizo CHADEMA: Katibu wenu wa wilaya pia yupo njiani. Actually huyu alikuwa CCM siku zote na amekuwa akitumiwa kuwachota CHADEMA. Sasa inasemekana CHADEMA wamesimamisha ruzuku kwa muda kwenda wilayani, na leo ameripoti kwa mabosi wa CCM hapa wilayani akidai kwamba kama ruzuku hamna hana haja ya kuendelea kubaki CHADEMA. Anasema bora yeye aondoke arudi rasmi na kuwazika CHADEMA hapa wilayani. Hii nimeipata mwenyewe kwa viongozi wa CCM waliokuwa wanaongea kwa kucheka na kutusema sisi tunaoshabikia CHADEMA hapa Kiomboi.

Kwa kifupi: CHADEMA ina watu wengi sana hapa Iramba Magharibi lakini haina VIONGOZI. Viongozi wengi wilayani wapo mfukoni wa Mwigulu na anawakatia kila akija. Ni vizuri kumuwahi huyu katibu mkampiga chini kabla Mwigulu hajamrudisha rasmi. Ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom