Viti Maalumu vyadhibitiwa

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,754
HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya CCM imesema kuanzia sasa ukomo wa viti maalumu vya ubunge, uwakilishi na udiwani ni vipindi viwili, baada ya hapo watatakiwa kwenda majimboni kugombea.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama katika Mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), katika makao makuu ya CCM. “Kuanzia sasa wanaojiona wametumikia vipindi viwili, ifikapo uchaguzi mkuu wa 2015 waanze kujiandaa kwenda majimboni kugombea,” alisema.

Aliongeza kuwa, NEC imefikia kuwa na ukomo katika uongozi wa viti maalumu kutokana na uamuzi wa Baraza Kuu la UWT katika mkutano wake uliopita. Mukama alisema uamuzi huo ni mzuri, kwani wabunge wanapotumikia vipindi viwili, tayari wanakuwa na ujasiri, uzoefu na wanaweza kusimama majimboni kugombea.

“Watakuwa na uzoefu ni vizuri wakasimama majimboni kugombea au kufanya kazi za kuimarisha chama,” alisema.

Mukama alisema hata hivyo, Kamati ya Wabunge wa CCM ilikataa uamuzi huo na kutaka utazamwe upya na akaurudisha Baraza Kuu la Wanawake ili waujadili tena. Baada ya kauli hiyo, wajumbe wa mkutano huo walipiga kelele wakisema uamuzi huo ni msimamo wao na hawataubadilisha.

“Hapana hatutaki na sisi tunataka iwe vivyo hivyo … wakagombee majimboni,” walisema baadhi ya wajumbe ambao walimfanya Mukama kusitisha kuzungumza hadi walipomaliza kauli zao.

Aidha, Mukama alisema wakati umefika kwa UWT kutumia vitegauchumi walivyonavyo ili kuwa na ufanisi. Alisema ni muhimu wakawa na mipango ya mapema kuendeleza viwanja vya UWT kwani ni rasilimali yenye thamani kubwa kwa sasa.

“Tuimarishe mali tulizonazo, tuhakikishe zinakuwa na hati, hasa ardhi … zikiwa na hati ni vizuri zaidi,” alisema na kuongeza: “Huwezi kuendesha uongozi bila kuwa na timu ya wanawake kwani hata kwenye familia mama asipokuwa imara familia itayumba na watoto watahangaika.

Awali, Mwenyekiti wa UWT, Sofia Simba, alisema mkutano huo una mambo mazito ya kuzungumza kutokana na kuwa kwenye maandalizi ya uchaguzi na ya mabadiliko ya Katiba na tayari kuwa vikundi vimeanza kupitapita kupotosha.

Alisema wapinzani wana mbinu nyingi, kwani wanapandikiza maneno na mtu kuonekana wa CCM “kumbe wamempandikiza kwani wanatafuta mbinu ya kutuvuruga. Tuwe makini na wapinzani kwani wanaweza kutuletea mapandikizi,” alisema.

Chanzo: Gazeti la Habari Leo
 
Hii nayo ni nzuri, ni vipi kwa wale wanaotoka majimboni harafu wakishashindwa wanapewa viti maalum?
 
Hawa CCM they are still LIVING IN STONE AGE. Wakati sisi (Watanzania Wazalendo) tunataka hivi viti maalum viondoshwe kwenye katiba mpya i.e. 2015 tusiwe na wabunge wa viti maalum, wabunge wa kuteuliwa na Rais. Wenyewe (CCM) bado wanaweka mikakati ya kupata wabunge wa viti maalum 2015?

Hii inanikumbusha ile PICHA YA GURUDUMU LA MAENDELEO wakati sisi (Wazalendo) tuna PUSH upward kuelekea kileleni wao (CCM) wana PULL downward. This is only possible in Tanzania of CCM
 
viti maalumu ni mzigo kwa taifa, vingefutwa kabisa. kwani inaonekana wanapeana ulaji tu. Wengi wao hakuna wanacho ongea. Hiyo nafasi Ingekuwa muhimu kama wangewekwa watu wa maana. Viti maalumu ingekuwa kwa walemavu na wazee tu
 
Kinachopiganiwa kwa sasa ni kufutwa kabisa kwa viti maalumu. Ubunge wa kuchaguliwa ndio uwe term mbili mwisho. Hawa CCM vipi? Wananchi tunaangalia mbele wao wanataka kuturudisha nyuma.

Kwanza kama wangekuwa na busara nilitegema wangeachana na hili suala wasubiri kuona Katiba itasemaje unless tayari wanayo Katiba tarajiwa. Hawa CCM vipi?
 
HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya CCM imesema kuanzia sasa ukomo wa viti maalumu vya ubunge, uwakilishi na udiwani ni vipindi viwili, baada ya hapo watatakiwa kwenda majimboni kugombea.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama katika Mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), katika makao makuu ya CCM. “Kuanzia sasa wanaojiona wametumikia vipindi viwili, ifikapo uchaguzi mkuu wa 2015 waanze kujiandaa kwenda majimboni kugombea,” alisema.

Aliongeza kuwa, NEC imefikia kuwa na ukomo katika uongozi wa viti maalumu kutokana na uamuzi wa Baraza Kuu la UWT katika mkutano wake uliopita. Mukama alisema uamuzi huo ni mzuri, kwani wabunge wanapotumikia vipindi viwili, tayari wanakuwa na ujasiri, uzoefu na wanaweza kusimama majimboni kugombea.

“Watakuwa na uzoefu ni vizuri wakasimama majimboni kugombea au kufanya kazi za kuimarisha chama,” alisema.

Mukama alisema hata hivyo, Kamati ya Wabunge wa CCM ilikataa uamuzi huo na kutaka utazamwe upya na akaurudisha Baraza Kuu la Wanawake ili waujadili tena. Baada ya kauli hiyo, wajumbe wa mkutano huo walipiga kelele wakisema uamuzi huo ni msimamo wao na hawataubadilisha.

“Hapana hatutaki na sisi tunataka iwe vivyo hivyo … wakagombee majimboni,” walisema baadhi ya wajumbe ambao walimfanya Mukama kusitisha kuzungumza hadi walipomaliza kauli zao.

Aidha, Mukama alisema wakati umefika kwa UWT kutumia vitegauchumi walivyonavyo ili kuwa na ufanisi. Alisema ni muhimu wakawa na mipango ya mapema kuendeleza viwanja vya UWT kwani ni rasilimali yenye thamani kubwa kwa sasa.

“Tuimarishe mali tulizonazo, tuhakikishe zinakuwa na hati, hasa ardhi … zikiwa na hati ni vizuri zaidi,” alisema na kuongeza: “Huwezi kuendesha uongozi bila kuwa na timu ya wanawake kwani hata kwenye familia mama asipokuwa imara familia itayumba na watoto watahangaika.

Awali, Mwenyekiti wa UWT, Sofia Simba, alisema mkutano huo una mambo mazito ya kuzungumza kutokana na kuwa kwenye maandalizi ya uchaguzi na ya mabadiliko ya Katiba na tayari kuwa vikundi vimeanza kupitapita kupotosha.

Alisema wapinzani wana mbinu nyingi, kwani wanapandikiza maneno na mtu kuonekana wa CCM “kumbe wamempandikiza kwani wanatafuta mbinu ya kutuvuruga. Tuwe makini na wapinzani kwani wanaweza kutuletea mapandikizi,” alisema.

Chanzo: Gazeti la Habari Leo

Sasa nyumba ndogo za watu zitakula wapi? Ukuu wa wilaya huo utakua dili sasa

Naunga Mkono kikomo cha viti maalum- siyo tunajenga tabaka la watawala milele na watawaliwa milele. Hii ieende hata kwa wabunge wote through katiba mpya
 
Ni wazo zuri litaongeza uwajibikaji si kwa CCM tu bali vyama vyote ingawa wazo limetoka CCM.
 
Wananchi wanapatikana majimboni hivi viti maalum vikiachwa bila ukomo wabunge hawa hawatawajibika kwa wananchi ipasavyo.
 
Kukosa ukomo kwa viti maalum kulitengeneza tabaka la ubunge wa kudumu viti maalum. Haikuwa kazi rahisi kumng,oa mbunge wa viti maalum aliyekaa muda mrefu hadi pale atakapacha mwenyewe. wengi walitumia fursa ya kukaa muda mrefu kujiimarisha na kuwaweka sawa wajumbe wa mkutano, wapo waliosema huyu ni mwenzetu tumchague tena.
 
Viti maalumu ni mzigo kwa Taifa.

Viti maalumu pamoja na viti kumi vya upendeleo vya rais inabidi vifutwe KABISA na hili lazima tulitekeleze, wakati watu tunafanya mchakato wa kufuta viti hivi na nafasi hizi za upendeleo, wenzetu wanabadilisha goli, hapana hili lazima tulisimamie.
 
Wapo waliokaa muda mrefu na kuzijua mbinu za ushindi matokeo yake wagombea wapya wa viti maalum hawakuweza kuwa na nafasi ya kupata ushindi. Utamu wa nafasi ulipozidi wapo waliolazimika kutoa rushwa ili wabaki kwenye madaraka.
 
VITI MAALUM NI KEEERO...............kuna baadhi ya viti maalumu hadi bunge linaisha wananuka midomo kwa kukaa kimya tu.
 
Bravo, Intelligent Mukama! kuna watu wanazaidi ya vipindi vitano vya ubunge wa viti maalumu na hawataki kwenda majimboni hivyo ni bora waende kugombea majimboni.
 
HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya CCM imesema kuanzia sasa ukomo wa viti maalumu vya ubunge, uwakilishi na udiwani ni vipindi viwili, baada ya hapo watatakiwa kwenda majimboni kugombea.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama katika Mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), katika makao makuu ya CCM. "Kuanzia sasa wanaojiona wametumikia vipindi viwili, ifikapo uchaguzi mkuu wa 2015 waanze kujiandaa kwenda majimboni kugombea," alisema.

Chanzo: Gazeti la Habari Leo

Afadhali, labda kitakachofuata ni kuvifuta kabisa
 
Na hii ya kuleta wapya inaweza kutoa nafasi ya kuongezeka kwa rushwa na hasa ya ngono
 
Bora wavifute kabisa kwani tokea mke wangu ateuliwe kuwa mbuge wa viti maalum mimi nakosa haki yangu ya ndoa hususani unyumba!
 
Well, mimi naona ni wazo zuri. Ukomo utatoa fursa zaidi kwa wanawake wengine kuja na mbinu mbadala za kuwaletea wananchi maendeleo katika jamii wanazoziwakilisha kupitia siasa za kibunge.

Natofautiana nao kitu kimoja, kwamba ukomo usiishie kwenye viti maalum pekee uendelezwe pia kwa wabunge wa kuchaguliwa na wananchi na wale wa kuteuliwa na raisi. Hoja yangu ni kwamba ubunge uwe na kikomo bila kujali aina ya mbunge.

Kama tumeweza kuweka ukomo kwenye uraisi kuna hoja gani ya maana ya kuwaacha wabunge. Kwa mtazamo wangu tunahitaji kupata watu wapya na mawazo mapya kila baada ya miaka kumi.
 
Back
Top Bottom