Viti maalumu 100 CCM vya nini?

kichenchele

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
539
176
Ama kweli jana nilikuwa nikiangalia Taarifa ya habari saa 2 za usiku kupitia TBC1 na kumuona Kapt.John Chiligatti akisema viti maalum vimeongezwa hadi kufikia 100, sasa mimi naomba kuuliza hivi hawa nao wanategemea kulipwa posho na mishahara kutoka ktk kodi zetu? wingi wao unanitia shaka na kunifanya niamini huu ni mkakati wa kupeana ulaji wa baadhi ya watu wanaokosa mvuto na kutokubalika kwa wapiga kura, 100 special seats for what?
 
Nadhani special seats huwa zinaendana na uwiano wa kura ambazo chama kimepata kwenye nafasi ya urais. Naona wanawafariji wanachama wao tu lakini ukweli ni kuwa kulingana na moto aliouwasha Dr Slaa CCM hawawezi kupata kura nyingi za kuwaruhusu wawe na wabunge wa viti maalum wengi kihivyo. Labda kama wakichakachua kura
 
FUNGU la kuendesha bunge na mambo mengine yote tuwekewe hadharani sasa kwani siasa sasa imechukua mkondo na nchi kutaka kuifananisha nchi kama India kwa ukubwa.

Ivi kweli kuna haja ya kuwa hivyo au? sijapata sababu ya kutosha kwanini 100 seats??? inamaana hawa CCM walisha jua ushindi wao ukoje? unajua tuko ndani ya CCM lakini mambo mengine yanaenda kinyume na tunavyo oona tu haina haja ya kwenda hata shule.

Kuwepo kwa viti maalum 100 vinaisaidia nchi vipi kuendelea au ni kutaka serikali kupitisha mambo yao hadhalani watakavyo wao au?? Jamani mimi nakalibia kujiaanda kuihama nchi hii najua sasa tunapo kwenda siko kabisaaaa
 
Hivi viti havitolewi kwa uwiano wa wabunge wa kuchaguliwa?
Kama vinatolewa kwa uwiano, ccm wakipa wabunge wachache itakuwaje?
Wametumia vigezo gani kuongeza hizo nafasi?

Naomba anayefahamu anijuze.
 
hapa kwenye attachment ndio kuna majina 100 ya viti maalumu,naomba wenye Ujuzi wayaweke wazi kutoka kwenye attachment.
 

Attachments

  • 35919233-Viti-Maalum-CCM-2010.pdf
    35.7 KB · Views: 166
Huwa nakosa energy ya kuchangia habari kama hizi......

Hivi viti maalum ni upuuzi mtupu......
Viwe viwili au viwe mia mbili ni upuuzi mtupu.....

Havifai na vinapaswa kufutwa..........
 
Hii listi kiboko. Kuna mtu nimeona jina lake sikutegemea kabisa kuwa ni mwanasiasa. Ila nimeshajiambia, no more surprises!
 
Kwani Bunge bila ya viti maalum haliwezi kuendesha mambo yake?
Nadhani wakati umefika wa kubana matumizi makubwa ya Bunge.
Pesa wanayolipwa wabunge wa viti maalum wapewe nyongeza
ya mishahara wenye kima cha chini.
 
Asante sana kwa mada, mie ndio navurugwa kabisa na the so called viti maalum, wataalam wa siasa na uongozi tunaomba mtusaidie. Kwenye mkoa mmoja ninaamini kuna wilaya/majimbo ya uchaguzi kadhaa ambayo yatatoa wabunge (aka wawakilishi wa wananchi bungeni). Kisha, kila mkoa tena unapewa nafasi ya uwakilishi kwa kofia ya viti maalum bungeni, ambao hawa wanakuwa wabunge nao! Sasa huyu wa mkoa anaenda kusema nini tena bungeni jamani wakati wapo waliotoka kwenye wilaya/majimbo kede kede! Kama wabunge wote wa kuchaguliwa ndani ya mkoa mmoja wakakaa kama kamati hawawezi kuuwakilisha mkoa?

Hivi kweli si ndio maana wanazidi kutukandamiza na kodi ili ikawalee watu wote hawa, ili hali tungepewa fursa ya kuchagua tungesema hiyo kodi iende kwenye miundo mbinu/mahospitali!

Hii mifumo mizigo tunaitoa wapi au tuliirithi wapi toba yarabi?
 
THANX MWAWADO KWA LIST..NAJARIBU KUIWEKA KTK WORD NADHANI ITASOMEKA NA WENGI KAMA ULIVYOOMBA...



WanaCCM Waliopendekezwa Kugombea Nafasi ya Viti Maalum Tanzania
(i) Viongozi Wakuu wa UWT

1.Ndg Sophia Mnyambi Simba (Mwenyekiti)
2.Ndg Amina Nassoro Makilagi (KatibuMkuu)

(ii) Kundi la nafasi mbili (2) kila Mkoa (nafasi ya kwanza)

Mara 3.Ndg. Gaudentia Mugosi Kabaka
Tanga 4.Ndg. Ummi Ally Mwalimu
Mtwara 5.Ndg. Agness Elias Hokororo
Manyara 6.Ndg. Martha Jachi Umbulla
Shinyanga 7.Ndg. Lucy Thomas Mayenga
Kusini Pemba 8.Ndg. Faida Mohamed Bakari
Dodoma 9.Ndg. Felista Alois Bura
Kaskazini Unguja 10. Ndg. Kidawa Hamid Saleh
Ruvuma 11. Ndg. Stella Martine Manyanya
Mwanza 12. Ndg. Maria Ibeshi Hewa
Mbeya 13. Ndg. Hilda Cynthia Ngoye
Kigoma 14. Ndg. Josephine Johnson Genzabuke
Simiyu 15. Ndg. Esther Lukago Midimu
Kaskazini pemba 16. Ndg. Maida Hamad Abdalla
Kusini Unguja 17. Ndg. Asha Mshimba Jecha
Dar es Salaam 18. Ndg. Zarina Shamte Madabida
Arusha 19. Ndg. Namalok Edward Sokoine
Tabora 20. Ndg. Munde Tambwe Abdallah
Kagera 21. Ndg. Benardetha Kasabago Mushashu
Geita 22. Ndg. Vick P. Kamata
Njombe 23. Ndg. Pindi Hazara Chana
Lindi 24. Ndg. Fatuma Abdallah Mikidadi
Morogoro 25. Ndg. Getrude Rwakatare
Kilimanjaro 26. Ndg. Betty E. Machangu
Singida 27. Ndg. Diana Mkumbo Chilolo
Mjini Magharibi 28. Ndg. Fakharia Shomari Khamis
Pwani 29. Ndg. Zaynabu Matitu Vulu
Rukwa 30. Ndg. Abia Muhama Nyabakari
Katavi 31. Ndg. Pudenciana Kikwembe
Iringa 32. Ndg. Lediana Mafuru Mng'ong'o

(iii) Kundi la Vijana T/Bara (nafasi
tatu)
33. Ndg. Sarah Msafiri Ally
34. Ndg. Catherine V. Magige
35. Ndg. Ester Amos Bulaya
36. Ndg. Neema Mgaya Hamid
(iv) Kundi la Vijana T/Zanzibar (nafasi 2)
37. Ndg. Tauhida Galos Cassian
38. Ndg. Asha Mohamed Omari

(v) Kundi la NGO's (nafasi 2)
39. Ndg. Rita Louis Mlaki
40. Ndg. Anna Margreth Abdallah

(vi) Kundi la Vyuo Vikuu (nafasi 2)
41. Dkt. Fenella E. Mukangara
42. Ndg. Terezya Lwoga Huvisa

(vii) Wanawake wenye Ulemavu (nafasi 2)
43. Ndg. Al-Shaymaa Kwegir
44.Ndg. Margreth Mkanga

(viii) Kundi la Wafanyakazi (nafasi 2)
45. Ndg. Angellah Jasmin Kairuki
46.Ndg. Zainab Rashid Kawawa

(ix) Kundi la nafasi mbili (2) kila Mkoa (nafasi ya pili)

Kusini Pemba 47.Ndg. Mwanakhamis Kassim Said

Lindi 48.Ndg. Riziki Said Lulida

Ruvuma 49.Ndg. Devotha Mkuwa Likokola

Morogoro 50.Ndg. Christina Ishengoma

Dodoma 51.Ndg. Mariam Salum Mfaki

Tabora 52.Ndg. Margreth Simwanza Sitta

Pwani 53.Ndg. Subira Khamis Mgalu

Iringa 54.Ndg. Rita E. Kabati

Singida 55.Ndg. Martha Moses Mlata

Kaskazini Pemba 56.Dkt. Maua Abeid Daftari

Kagera 57.Ndg. Elizabeth Nkunda Batenga

Shinyanga 58.Ndg. Azza Hillal Hamad

Mbeya 59.Ndg. Mary Machuche Mwanjelwa

Geita 60.Ndg. Josephine T. Chengula

Kaskazini Unguja 61.Ndg. Bahati Ali Abeid

Kusini Unguja 62.Ndg. Kiumbwa Makame Mbaraka

Rukwa 63.Ndg. Roweete Faustine Kasikila

Mtwara 64.Ndg. Anastazia Wambura

Tanga 65.Ndg. Mary Pius Chatanda

Mara 66.Ndg. Rosemary Kasimbi Kiligini

Dar es Salaam 67.Ndg. Mariam Nassor Kisangi

Mwanza 68.Ndg. Kemilembe Julius Lwota

Mjini Magharibi 69.Ndg. Asha Abdalla Juma

Katavi 70.Ndg. Anna Richard Lupembe

Simiyu 71.Ndg. Tinner Andrew Chenge

Njombe 72.Ndg. Rosemary Staki Senyamule

Kilimanjaro 73.Ndg. Shally Josepha Raymond

Arusha 74.Ndg. Halima Mohamed Mamuya

Manyara 75.Ndg. Dora Heriel Mushi

Kigoma 76.Ndg. Amina Butoye Kanyogoto

(x) Kundi la Vijana – Tanzania Bara (nafasi 3)

77.Ndg. Happyness Elias Lungiko
78.Ndg. Kaslida Jeremia Mgeni
79.Ndg Mboni Mohamed Mhita

(xi) Kundi la Vijana – T/Zanzibar (nafasi1)
80.Ndg. Rabia Abdallah Hamid

(xii) Kundi la Vyuo Vikuu 81.Ndg. Rukia S. Mselem
(xiii) Kundi la Walemavu 82.Ndg. Hidaya Mjaka Ali

(xiv) Kundi la Kapu – (nafasi 18)
83.Ndg. Janet Maurice Masaburi
84.Ndg. Sifa Amani Swai
85.Catherine Peter Nao
86.Ndg. Moshi Kondo Kinyogoli
87.Ndg. Janath Mussa Kayanda
88.Ndg. Zulfa Abdalla Said
89.Ndg. Asha Ramadhani Baraka
90.Ndg. Aziza Sleyum Ally
91.Ndg. Mwaka Abdurahamani Ramadhani
92.Ndg. Esther Kabadi Nyawazwa
93.Ndg. Fatuma Hassan Toufiq
94.Ndg. Mwantum Haji
95.Ndg. Florence E. Kyendesya
96.Ndg. Aisha Matembe
97. Ndg. Raya Talib Ali
98.Ndg. Rukia Masasi
99.Ndg. Nemburis Kimbele
100.Ndg. Fatuma Hamza Mohamed

(i) Kiongozi Mkuu wa UWT
1. Ndg. Asha Bakari Makame (Makamu Mwenyekiti)

(ii) Kundi la nafasi mbili (2) kila Mkoa (nafasi ya kwanza)

Mjini Magharibi 2. Ndg. Amina Iddi Mabrouk

Kusini Pemba 3. Ndg. Shadya Moh'd Suleiman

Kusini Unguja 4. Ndg. Salma Mussa Bilali

Kaskazini Pemba 5. Ndg. Bihindi Hamadi Khamis

Kaskazini Unguja 6. Ndg. Panya Ali Abdalla

(iii) Kundi la Vijana nafasi mbili (2)
7. Ndg. Wanu Hafidh Ameir
8. Ndg. Viwe Khamis Abdallah

(iv) Kundi la Vyuo Vikuu (Nafasi ya
kwanza)
9. Ndg. Mgeni Hassan Juma

(v) Kundi la Walemavu (Nafasi ya
Kwanza)
10. Ndg. Raya Sleimani Hamadi

(vi) Kundi la nafasi mbili (2) kila Mkoa (nafasi ya pili)

Mjini Magharibi 11. Ndg. Mwanaidi Kassim Mussa

Kusini Pemba 12. Ndg. Zainab Omar Moh'd

Kaskazini Unguja 13. Ndg. Mwanajuma Kassim Mkame

Kusini Unguja 14. Ndg. Nashide Hijja Abdullah
Kaskazini Pemba 15. Ndg. Sharifa Humuod Rashid

(vii) Kundi la Vijana nafasi tatu (3) 16. Ndg. Asha Juma Khamis

17. Ndg. Riziki Khamis Pembe

18. Ndg. Nadra Gulam Rashid

(viii) Kundi la Vyuo Vikuu (Nafasi ya
pili)
19. Ndg. Sabaha Salehe Ali
(ix) Kundi la Walemavu (Nafasi ya pili) 20. Ndg. Mwantatu Mbarak Khamis
 
Unajua kuna kabila fulani huku Pwani ni watu wa kuridhika sana. Akiwa na kibanda chake cha udongo cha chumba na sebule na mnazi mmoja na baiskeli basi anaongeza mke wa pili na kitambi kinanawiri. Mtu kama huyo anapokuwa madarakani kama Rais hupima maendeleo ya nchi kwa wingi wa magari ya serikali na ongezeko la majengo jijini Dar es Salaam.

Rais wa namna hiyo anaamini miaka mitano iliyopita amefanya makubwa mno na sasa ni wakati wa kulipana fadhila. Huyu ni mtu aliyepita bila kupingwa kwa sababu tu watanzania ni waoga, wanamjua ni mlipa fadhila mzuri na mlipa kisasi mzuri pia.

Anaifananisha Tanzania na Somalia na kuona tuko mbaali sana kimaisha. Then.....why not adding more ulaji positions....hata viti maalumu milioni...poa tu. si mnamuita Dr... Doctor wa kitu gani au unafiki na uoga.

Safari hii atatuletea watu wenye kofia ishirini.....mbunge + mkuu wa mkoa + waziri+ second first lady +.....

Hii nchi haiendi kokote na upuuzi huu. Hatuwezi kuwa na chama tawala na mwenyekiti wake wanaofikiri nchi hii imebakiza miaka mitano tu ya kuwepo duniani.

CCM na JK wao hawatufai.
 
Sioni hata wanachokifanya bungeni zaidi ya kutengenezeana ulaji tu. Na huu ni upuuzi. Mimi nadhani hata hivyo vya majimbo tu sioni chamaana sana wanachokifanya pia kwani wengi wanaenda kwa ajili ya masilahi tu. Mimi nadhani bungeni kungepunguzwa ulaji kama yule mbunge alieteuliwa wa CUF kutoka kule zanzibar alipoingia tu bungeni na kutoa hoja hiyo ya kupunguziwa mishahara na marupurupu haya yote yasingetokea.
Hebu tujiulize, kama mtu anauza gari la mil 50 na nyumba, huyu mtu atarudisha vipi hivi vitu? atakuwa amekalculeti na kuona kuwa gharama hizo zinarudi ndani ya mwaka mmoja tu na mingine iliyobaka ni faida, huyo ameenda kuchumia tumbo ni si kutetea maslahi ya taifa.
Kwahiyo hayo mapato yakipungua tutabaki na watu wenye wito tu ndo watakaoenda bungeni. Hapa profesa pale mlimani hataacha kazi yake ya kulecturer na kufanya research kukimbilia bungeni kama hana wito.
 
viti maalum 50 tu basi ni vingi kwa vyama vyote vikijumuishwa pamoja! hawa pesa ya mlipa kodi hawaithamini hata kidogo! agggr
 
CCM Wanaota kuchukua bunge 100%......how much of a nightmare that will be isn't ny guess :peace::peace::A S 103:
 
amah ndio maana aliyekuwa mbunge wa jimbo letu la kawe bi rita mlaki alisema hagombei tena kumbe akula kona na kwenda kupata ubunge kwa urahisi kupitia ngo's haha haha ama kweli siasa za tanzania zina mambo,mimi kwa upuha wangu nilifikiri rita ndio hataki tena mambo ya ubunge,kumbe alisoma nyakati za wakati ,mtu kama huyu bungeni ni wanini si anaenda kuji -enjoy tu ,ndio maana i hate politics
 
Back
Top Bottom