Vitendo hivi vya udanganyifu vinaipeleka elimu yetu pabay

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
KATUNI%28589%29.jpg

Maoni ya katuni




Jana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilitangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la saba, yakionyesha kuwa kiwango cha ufaulu kwa mwaka huu kimeongezeka kwa asilimia tano.



Akitangaza matokeo hayo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema kuwa kiwango hicho kimeongezeka kutoka asilimia 53.52 ya mwaka jana hadi asilimia 58.28 kwa mwaka huu.


Kati ya wanafunzi 983,549 waliofanya mtihani huo, wanafunzi 567,567 wamefaulu wavulana wakiwa 289,190

(asilimia 62.49) na wasichana wakiwa 278,377 (asilimia 54.48). Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa ufauli wa masomo ya Kiingereza, Hisabati na Sayansi umeongezeka.


Itakumbukwa kuwa watoto wengi katika shule zetu za msingi na sekondari wamekuwa wakifeli katika masomo hayo mwaka hadi mwaka.

Kwa mujibu wa matokeo ya mwaka huu, kiwango cha ufaulu wa Hisabati kimeongezeka kwa asilimia 14 kutoka asilimia asilimia 24.70 mwaka jana hadi asilimia 39.36 kwa mwaka huu; kwa upande wa Kiingereza ufaulu imeongezeka kwa asilimia 10 kutoka asilimia 36.47 ya mwaka jana hadi asilimia 47.70 mwaka huu, wakati

ufaulu wa Sayansi umeongezeka kwa asilimia 5.28 kutoka asilimia 56.05 mwaka jana hadi asilimia 61.33 mwaka huu.



Kuongezeka kwa idadi ya ufaulu wa jumla na kuongezeka kwa ufaulu katika masomo ya Hisabati, Kiingereza na Sayansi ni habari njema kwa Watanzania kutokana na idadi kubwa ya watoto wetu kufeli kati masomo hayo.


Hatunabudi kuwapongeza waliosababisha mabadiliko hayo na tunawaomba waendeleze jitihada hizo ili kufuta

kabisa aibu ambayo imekuwa ikiwapata watoto wetu ya kufeli masomo hayo ambayo ni ya msingi na ya muhimu sana kwao.



Hata hivyo, kitu cha kusikitisha ambacho pia ni aibu kwa taifa ni kitendo cha idadi kubwa ya watoto 9,736 sawa na asilimia 1.0 kufutiwa matokeo yao kutokana na kubainika kwamba walifanya udanganyifu wakati wa mtihani huo!.



Waziri Mulugo alitangaza kuwa watoto hao kutoka shule mbalimbali wavulana wakiwa ni 4,943 na wasichana ni 4,793 walijihusisha na vitendo hivyo vya udanganyifu ambavyo vimesababisha kufutiwa matokeo. Hali hiyo inatisha kwa sababu idadi hiyo ni kubwa sana.



Kati ya mikoa iliyofutiwa matokeo kwa baadhi ya shule, mkoa wa Manyara ndio umeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya vitendo vya udanganyifu vilivyosababisha watahiniwa wapatao 1,573 kufutiwa matokeo, ukifuatiwa

na mikoa ya Arusha 1,012, Dar es Salaam 752, Iringa 737, Morogoro 725, Tanga 717 na Kilimanjaro 575.


Mikoa mingine iliyofutia ni Dodoma 493, Kagera 483, Mara 377, Mtwara 354, Mwanza 333, Pwani 279, Shinyanga 228, Mbeya 216, Ruvuma 203,Rukwa 181, Singida 148, Tabora 174, Kigoma 113 na Lindi 63.

Miongoni mwa mambo ambayo yaligunduliwa na kusababisha kuwafutia baadhi yao matokeo ni kukutwa na karatasi za majibu katika chumba cha mtihani, kuandika miandiko zaidi ya mmoja, kukariri darasa la saba kinyume na taratibu pamoja na kuwa na mfanano usio wa kawaida katika kukosa.



Hali hii haipaswi kuvumiliwa na ni lazima serikali kupitia wizara husika kufanya uchunguzi wa kina kubaini hali

hiyo, vinginevyo huko mbele tuendako vitendo hivyo vitaongezeka. Uchunguzi huo unaweza kusaidia kubaini kama ni watahiniwa wenyewe wanaofanya vitendo hivyo ama nyuma yake kuna watu wengine kama walimu na wazazi.


Katika miaka ya hivi karibuni zilianzishwa shule za sekondari za kata kwa lengo la kuongeza idadi ya watoto wanaopata elimu ya msingi nchini. Hata hivyo, hatua ya kuanzisha shule hizo imekuwa ikikosolewa vikali

kwamba imechangia kuporomosha kiwango cha elimu nchini.


Wanaojenga hoja hiyo, wanasema kuwa shule hizo zinachukua watoto wengi waliofeli katika mtihani wa darasa la saba na kwamba mazingira duni ya kutoa elimu katika shule za sekondari za kata pia yanachangia wafanye vibaya katika matokeo ya kidato cha nne.

Waziri Mulugo ametoa matumaini kwa kuahidi kwamba, watoto wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza watafanyiwa mtihani wa kuwapima uwezo wao wa kusoma na kuandika baada ya shule hizo kufunguliwa na kwamba watakaoshindwa itawapasa kurudia.





CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom