Vitendo 19 vya kifisadi vya blandina nyoni....

jozzb

Member
Jun 30, 2011
87
20

Hivi ni baadhi ya vitendo vya kifisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-


1. Amekuwa akilipwa mshahara wa ziada na Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)



2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.



3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na
Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.


4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani
kama Katibu Mkuu.


5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict of Interest’


6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi
yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara


7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj)


8. Amenunua vingamuzi vya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko
Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa na madeni lukuki.


9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi 1,968,475,931
mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010


:A S 465:NIMEYAKUTA HUKU << BLANDINA NYONI>>
 
wengine ndio tunaiona kwa mara ya kwanza. Thanx mdau kwa kuileta tena.
 
Aisee....kweli kama haya ni kweli na kamati au vyombo vya dola vilivyopewa kazi yakumchunguza vikithibitisha haki ya nani asipowekwa segerea yatupasa watz tuandamane....serious...hii inauma sana wanaume jf @ Asprin acha irudiwe tuu hii ni tuhuma mzito.nilikuwa sijaiona....kumbe mtoto wa mkulima aliiona hii .....duh mulika mwizi jf big up.
 
Back
Top Bottom