Vitanda vya Sita kwa Sita: Chanzo cha ndoa kuvunjika

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,193
515
Enzi zetu sisi ndoa zilikuwa hazivunjiki! Mimi na bibi yako tumekuwa tunagombana lakini usiku ilikuwa lazima tupatane! Tukiamka asubuhi tu wapya mapenzi yanaendelea kama vile hakuna lililotokea jana.

Pamoja na mapenzi ya dhati yasiyo angalia kitu kama yenu kitanda chetu cha kamba cha futi tatu kwa tano kimetufanya tumekuwa karibu sana! Tunagusana hata kama tumeudhiana, bibi yako anasikia harufu ya jasho langu na mimi nasikia la kwake, akiguna namskia akigeuka ananigusa, usiku kucha joto lake joto langu. Maisha yamekuwa ya raha mustarehe.

Nyie ndoa zenu hazidumu kwa sababu ya vitanda na sio wavumilivu, lakini wengi wenu mnaingia kwenye ndoa mkiwa tayari mmesha wahi kupenda sana watu wengine kuliko mlio waoa na hivyo inawawia vigumu kuwasahau kirahisi.

BABU HAPA KWENYE VITANDA PAKOJE?!

Nyie vitanda vyenu ni sita kwa sita, ama tano kwa sita! Hivi vinamkaribisha shetani! Mwenyezi mungu anasema "wawili wakishikamana yeye anakuwa kati yenu" vitanda vyenu vinavunja ndoa zenu!

Unakuta mmeudhiana, vitanda vyenu vya sita kwa sita wakati wa kulala mmoja yuko kule mwingine yuko huku katikati nafasi! Hapo katikati analala "shetani" upande wa kule mke anamuwaza mtu wake (john/ally) upande wa kule mume ana muwaza mtu wake (maria/asha), hawagusani, hawapeani joto, hawapeani harufu za kimahaba maana nafasi ya kitanda inawapa jeuri. Hata wakati wa kugeuka una weza kugeuka bila hata ya kumgusa mwenzako! Hili ni tatizo kwa ndoa, ndio maana mnaachana maana hamko pamoja na Mungu mnapo kuwa vitandani. Mnamruhusu shetani katikati yenu! (Hapa nikakumbuka kale ka mstari ka umombo kanako sema 'nearest is dearest')

Nakushauri mjukuu wangu! Kama unataka kuendelea kuishi na mkeo hadi uzee kama wangu achana na uleo! Haraka sana fanya hima ubadirishe kitanda.

** Haya yalikuwa ni masimulizi ya babu yangu mmoja niliyekwenda kumtembelea kijijjini kwetu Lushoto, pamoja na hayo nikagawa neno la mabadiliko, ameniambia hana hamu tena na ccm, ilibidi nimpatie kadi ya chadema na bendera atundike sehemu anayo otea jua**

Source: wavuti.com - wavuti
 
Attachments

  • 154203956.jpg
    154203956.jpg
    67.1 KB · Views: 330
hili nalo neno!tena neno kuntu!shurti mkilala mgusane sasa na haya mavitanda yetu ya jumbo sijui nini haaya yanafanya mambo yasiwe murua!mambo ya ''bulging from behind'' huyasikii sasa!ahhaahhahahh wapi Kaunga na pacha wangu SnowBall!kujeni huku muone ''bulging from behind'' inavonyimwa eneo la tukio sababu ya ukubwa wa vitanda!
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaa! Saivi vipo 8 by 8. Ujue zamani style ilikuwa moja missionary, aka kifo cha mende aka mbwa kachoka, hivo basi 4 by 6 ilikuwa inatoshea KABISAAAAA! Ila na hizi design za KICHINA sijui Doggy Doggy, Mbuzi Kagoma, Fungua Dirisha, Blackberry, sijui Kipetite NK NK, Hata hicho cha 8 BY 8 kinakuwa kidogo atiiii, hakitoshelezi kabisaaaa! Ndo maana unakuta watu wana 8 by 8 , ZULIA, KOCHI CHUMBANI NA KIBENCH BAFUNI!!!!!! Kazi kweli kweli!!!!!!!!!!
 
hakuna aliyenuna i hope!hizi style hizi mweh! lara 1 upo dogo?umeamkaje?
 
hii ni kweli kabisaaaaaa, unakuta likitanda likubwaaaaa, mpaka mkigombana mnatenganishana na mito kabisa, na bado kila mtu anatoshea kulala! hili nalo neno wallah!
 
hili nalo neno!tena neno kuntu!shurti mkilala mgusane sasa na haya mavitanda yetu ya jumbo sijui nini haaya yanafanya mambo yasiwe murua!mambo ya ''bulging from behind'' huyasikii sasa!ahhaahhahahh wapi Kaunga na pacha wangu SnowBall!kujeni huku muone ''bulging from behind'' inavonyimwa eneo la tukio sababu ya ukubwa wa vitanda!

Mapenzi ya siku hzi yamegubikwa na mambo mengi sana... haya ya size ya vitanda yanaweza yakawa sababu ndogo sana kama tone la maji baharini...Kikubwa moody unayoingia nayo kitandani ndio jambo la muhimu aisee..Mkishaudhiana hata mkilala 8*2 ngoma hainogi!..Any ways babu anaongelea zama gani?..Mbona kule kijijini kwetu wameanza kulalia 5*6 long tyme....Nadharia za mapenzi haziiishi...lol!
 
kunguru afugiki mkuu...hata uweke kitanda cha mbili kwa mbili sijui....binafsi sipendi kubanana...baada ya game tupeane nafasi ya kuinjoi usingizi....
 
Jaman maisha bila kugombana hayana fleva,,, sometime mnazinguana bana,,,
 
ndoa hujengwa na vitu vingi sio kitanda pekee...

Ila na kitanda imo coz ngoz kwa ngoz joto jotolile lazima kipigike hata kama mmenuniana kesho ni vicheko na kukumbushiana extra time kafunga goli la OFFSIDE, Utasikia "Nilikaba vizuri sana sema ile ilikua umeotea la sivyo penalt ndo zindeamua"......
 
Enzi za zamani zipi anazozizungumzia huyo babu?

Hawa sio waliokuwa na wake wengi, mke anakutana na mume mara moja kwa wiki?!
 
Na huu uwingi wa vyumba pia unachangia, wanandoa wakigombana basi mmoja wao atahamia chumba cha watoto au wageni.
 
Ila na kitanda imo coz ngoz kwa ngoz joto jotolile lazima kipigike hata kama mmenuniana kesho ni vicheko na kukumbushiana extra time kafunga goli la OFFSIDE, Utasikia "Nilikaba vizuri sana sema ile ilikua umeotea la sivyo penalt ndo zindeamua"......

sio kila mnuno au ugomvi unamalizwa na kitanda..........
 
Sidhani kama kitanda kinaweza kuwa kichocheo cha wawili kutopatana pindi wakiudhiana...
Tamanio la mwili li ndani ya moyo vivyo hivyo hasira ya mpumbavu hufura kifuani mwake...
Najua babu yako kakisifia sana kitanda cha 3x5 na kukipamba kuwa kilikuwa kinahusika katika kurejesha upya uhusiano pindi kadhia ya hasira inapochukua hatamu.
Ninadiriki kusema kuwa Babu yako kama sio kuwa anajifaragua basi amesahu kuwa kwa ukubwa huo huo wa vitanda vyao bado wenzi wa wakati wao walikuwa wakilala ilhali wana hasira.
Kwa kumkumbusha tu, naomba umuulize babu yako, nini asili ya neno "KULALA MZUNGU WA NNE"
 
Kitanda kikiwa kidogo mwingine anakubali kulala chini, hao babu zetu wenyewe walikuwa wanahama mpaka vitanda maana vile vya kamba vilikuwa vingi chumba kimoja unavikuta mpaka vinne. Pia vipo vitanda vya kamba ambavyo ni vya ghorofa yaani juu na chini.
 
Enzi za zamani zipi anazozizungumzia huyo babu?

Hawa sio waliokuwa na wake wengi, mke anakutana na mume mara moja kwa wiki?!

Lakini si kulikuwa na upendo wa dhati pamopja na hizo ndoa za mitala mwl?
 
Lakini si kulikuwa na upendo wa dhati pamopja na hizo ndoa za mitala mwl?

Basi hapa tuambiwe kilichopelekea mapenzi ya dhati na sio kitanda.

Na juu ya hivyo, hayo mapenzi ya dhati hatuna uhakika kama yalikuwapo kweli. Kuwa watu hawakuachana haina maana kuwa walikuwa wakipendana sana.

Inawezekana kukawa na sababu nyengine zilizowafanya watu kubakia kwenye ndoa, kama kuogopa kunyanyapaliwa na jamii, kuogopa kukosa haki za msingi kama umiliki wa mali na kuishi na watoto.

Ikiwa leo hii watu wanakomaa kwenye ndoa hata kama wanateseka, itakuwa enzi hizo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom