Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitamini na madini

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 29, 2010.

  1. MziziMkavu

    MziziMkavu JF-Expert Member

    #1
    Oct 29, 2010
    Joined: Feb 3, 2009
    Messages: 38,339
    Likes Received: 2,412
    Trophy Points: 280
    Ni vibaya ya kwamba kwa sababu ya kukosa fedha watu wengi katika nchi za joto wanateseka

    kwa kutokana na njaa. Lakini pia ni vibaya zaidi ya kwamba wanateseka ya kuwa jibu la
    kupata matangazo yanayoshawishi kununua vitu vilivyotengenezwa kama “kiamsha hamu”
    (appetizer)”juisi ya vitamini nk. Vitu hivi havina faida na sio lazima. Nyama ni rahisi na

    inakupa nguvu zaidi kuliko kichupa cha “sana-vita-liver extract”. Vitamini za kurutubisha za

    E”majani yake yana nguvu zaidi kuliko “Paradiaso –impotex”vidonge vyake.
    Mama mmoja kutoka kijiji chetu D.R. Kongo alitumia mshahara wake kwa wiki nzima, kwa

    ajili ya chupa moja ya sirapu nyekundu iliyotengenezwa bandia, akiamini itamsaidia binti
    yake kumwimarisha damu. Mwanamke huyu alikuwa kirahisi mwanakijiji? Hebu tuangalie
    kwa karibu katika jiji na Hospitiali za kanisa, hata katika miji mikubwa.Kuna ufujaji katika

    bajeti, katika bajeti vitu kama hivyo kama “sindano za vitamini””vitamini B za vidonge”,
    “vitamini E torte”“haemo-vit-orange”na vingine vitolewavyo na kupendwa kwa majina.
    Watu wahusika wangefanya vizuri zaidi kuweka machungwa na karanga katika mashelfu yao
    maduka ya madawa!

    a)Vitamini A: Muhimu kwa ajili ya macho na kwa ajili ya utando na ngozi (skin).
    Inapatikana katika rangi zote nyekundu na rangi ya manjano, matunda na mboga; Mapapai,

    Karoti, Nyanya na Maembe; katika mayai na katika matunda ya mchikichi. Mafuta ya
    mchikichi ni tajiri sana katika vitamini A. Huko Afrika ya magharibi, mahali ambako kuna
    wingi wa mafuta ya mchikichi, watu wachache wanateseka na upofu. Katika mashariki na

    kusini mwa Afrika ambako mafuta ya mchikichi ni haba, tunapendelea kukuza na kula
    machungwa, viazi vitamu, kuepuka mahitaji ya vidonge vya vitamini A.

    b)Vitamini B komplex: Muhimu kwa ajili ya wale wenye matatizo ya usumbufu wa mishipa
    na kudhoofika. Vitamini hizi ni za lazima kwa ajili ya kuyeyusha na kufyonza kabonhaidreti
    kama sukari, unga. Vitu vilivyotengenezwa kienyeji vipatikanavyo, kama Karanga,

    Maharage
    ya soya, Maharage, Nyama, Samaki, Hamira, mboga za majani na mchele makapi au maziwa
    ya mama yaliyo na kiasi kikubwa cha vitamini hizi. Ni kosa kubwa , kwa sababu hii kuuza
    Karanga ili kununua “vitamini B”biskuti.


    c) Vitamini C: Kinga asili ya mfumo wa miili yetu, ambayo inatukingia maambukizo
    alimradi vitamini C. Watoto wa umri hadi miezi 6 wanapata ya kutosha maziwa ya mama zao.
    Zaidi ya umri huu mmoja ni lazima ale aina zote za matunda (hasa machungwa, matunda ya

    karakana na malimao) na mboga za majani (mboga za majani, vitunguu na viazi n.k). Mtunda
    yasiyopikwa na mboga ni bora zaidi kwani yakipikwa yanapoteza vitamini C. Tofauti yake na

    vitamini A, vitamini C haiwezekani kuhifadhika mwilini, kwa sababu hiyo ni lazima kula
    matunda na mboga kila siku.

    d) Vitamini D: Inasaidia katika kukua kwa mifupa. Mwili wenyewe unatengeneza kutoka
    jua. Mayai na mafuta pia ni chanzo kizuri toka vitamini D.

    e) Vitamini E: Inapatikana kutoka majani mabichi na mafuta ya chakula. Utendaji kazi
    kiafya bado haueleweki kamili. Katika utangazaji inaitwa “vitamini ya uzazi wa watoto “
    lakini hata hivyo, hakuna mgumba aliyepata watoto na kushukuru vitamin E kimadawa!
     
  2. MziziMkavu

    MziziMkavu JF-Expert Member

    #2
    Oct 29, 2010
    Joined: Feb 3, 2009
    Messages: 38,339
    Likes Received: 2,412
    Trophy Points: 280
    g) Vitamini K. Inasaidia mambo ya damu kuganda. Inapatikana katika aina zote za
    mboga za majani pia hutengenezwa katika viini tumboni. Kuna mila zisizofaa ambazo
    hutumiwa na wakunga kwa kuwapa wakina mama waliojifungua sindano za vitamini K
    kila mmoja mara baada ya kujifungua. Hii inaidhinishwa tu kama kuna ukosefu wa
    vitamini K.

    h) Foliki Esidi: Ni muhimu kwa upungufu wa damu. Inapatikana kwa kiasi kikubwa
    katika maini na mboga za majani.

    i) Kalisiamu: Kalisiamu ina nafasi muhimu kutengeneza chembechembe mwilini kipekee
    katika mishipa na mifupa. Kidonge cha Kalisium toka kwenye famasia kina uzito wa
    mg 200 za kalisiamu ni kama g 10 za samaki mkavu, g 30 maziwa ya unga, g 100 za
    mboga za majani, g 200 maharagwe.

    j) Chuma: madini ya chuma husaidia kutengeneza hemoglobini, chembechembe kamili
    nyekundu za damu. Kujaribu kutibu upungufu wa damu na wekundu kwa limao ni
    bure! Ni vizuri zaidi kula aina zote za mboga za majani. Fanya kila liwezekanalo

    kukinga sababu za upungufu wa damu, kama Malaria, kuharisha muda mrefu, na
    minyoo. Matumizi ya vikaangio na sufuria za chuma zinapendekezwa-bali sio zile
    zinazotengenezwa kienyeji kutoka mabaki ya vyuma vya magari vya zamani, kwani

    hivyo vina aina nyingine ya chuma yenye sumu.
    Ili kupata utajiri wa vyakula vyenye chuma, kila siku unaweza kuweka vitu vyenye
    kutu (lakini safi !) Misumari kwenye sufuria wakati wa kupika. Kwa njia hii kiasi

    kidogo cha chuma kinaingia kwenye chakula na hivyo mwili wetu unanyonya kiasi
    fulani cha madini ya chuma kwa siku. Au unaweza kuingiza msumari wenye kutu ndani
    ya chungwa au limao. Baada ya siku tatu utoe na kula au kamua juisi yake. Juisi

    itakuwa imebadilika kuwa madini ya chuma ambayo yana dawa (asili iliyobadilika
    katika matunda, madini yaliyo na myeyuko wa madini ya chumvi abayo yameyeyuka
    katika matunda

    k) Madini ya joto : Katika umbali na mikoani kutoka baharini watu wengi wanapata
    Ugonjwa wa Goita kutokana na ukosefu wa madini ya joto, ambayo yanapatikana
    kipekee toka mazao ya baharini. Kwa hiyo tunatoa ushauri kununua mg 30 za “Ingol
    0.1 % kutoka famasi na ongeza matone 1-10 kila siku kwa mtu katika chakula chake.

    Mwongozo wa famasia: changanya mg 100 za madini ya chuma pamoja na mg 200 za
    potasiumu iodide, na yeyusha mchanganyiko huo katika ml.100 kwenye maji
    yaliyochemshwa na kuchujwa. Hifadhi na gawanya katika chombo cha glasi, nasiyo
    cha plastiki wala chuma
     
Loading...