Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema awamu ya kwanza ya Vitambulisho vya Taifa imekamilika na vitaanza kutolewa mapema mwezi ujao (May).
Imesema kuwa uzinduzi wa kutoa vitambulisho hivyo ulikuwa ufanyike jana katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini ilishindikana kutokana na shughuli nyingi na ukubwa wa tukio hilo.
Ofisa Habari wa NIDA, Rose Mdami alisema uzinduzi huo unatarajiwa kufanywa na Rais Jakaya Kikwete ambapo wiki ijayo watazungumza na waandishi wa habari na kuelezea utaratibu mzima utakavyokuwa.
Katika utekelezaji wa mradi huo, Mamlaka itatoa vitambulisho katika makundi matatu; Watanzania, wageni wakazi na wakimbizi.
Alisema baada ya wafanyakazi wa Serikali, watafuatiwa wanafunzi, wafanyabiashara na hatimaye Watanzania wote watafikiwa na huduma hiyo muhimu kwa Taifa bila gharama yoyote.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa, pamoja na kuwa huduma hiyo ni bure, lakini mwananchi atakayepoteza kitambulisho chake atalazimika kukilipia.