Vitambulisho kuamua mikopo ya wanafunzi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amesema serikali itatumia vitambulisho vya taifa kubaini wanafunzi wa vyuo vikuu wanaostahili kupewa mikopo. Nahodha alisema wapo baadhi ya wanafunzi ambao hawastahili kupewa mikopo hiyo, lakini wamekuwa wakipewa.

“Kuna wanafunzi ambao wanachukua mikopo wakati hawastahili kupewa, hivyo basi kwa kutumia vitambulisho vya taifa, itasaidia kubaini wasiostahili kupewa mikopo,”alisema. Nahodha aliyasema hayo juzi katika kipindi cha dakika 45 kilichorushwa kituo cha televisheni cha ITV na kufafanua kwamba suala la kutengeneza vitambulisho vya taifa limefikia kwenye hatua nzuri.

Alifafanua kwamba Aprili 21, mwaka huu serikali ilisaini mkataba na kampuni ya Malaysia kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho hivyo na kwamba sasa wanatafuta fedha ili kuanza shughuli hiyo.

Alibainisha kuwa utekelezaji wa mradi huo ni mgumu kwa kuwa Tanzania ina watu 26 milioni ambao wanastahili kupewa vitambulisho. Alisema vitambulisho hivyo vitaanza kutolewa kwa wafanyakazi, wanafunzi na wafanyabiashara kwa sababu taarifa zao zinatambulika.

Waziri huyo alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa polisi endapo watabaini kuna wahamiaji haramu katika maeneo yao ili wachukuliwe hatua za kisheria. Katika hatua nyingine, Nahodha alisema serikali inaanza kuwarudisha kwao zaidi ya wakimbizi 37,000 wa Burundi walioko kwenye kambi ya Mtabira, mkoani Kigoma.

Alisema Serikali itaawaondoa nchini wakimbizi hao kwa awamu na kila mwezi wataondoka wakimbizi 10,000 na kwamba hadi kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wameondoka wote.Alisema tayari wamefuata sheria zote stahili za kuwaondoa wakimbizi nchini na kwamba endapo watagoma kurudi kwao hatua za kisheria zitafuatwa.
 
hizi hadith za vitambulisho nimezisikia zamani sana sijui lini zitaisha, au mpaka cdm iingie madarakani?
 
Back
Top Bottom