mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,960
- 2,464
hapo jyfranca umenikumbusha uhondoo wa grisham ana novel inaitwa the client hakika ilinifurahisha mnomi nimesoma vitabu vyote vya james hadley chase na erle stanley gardner. Nimesoma pia vitabu vya musiba. Kwa kifupi sidhani kam vitabu vya chase vinafanana hata kidogo na vya musiba. Chase ni 3w- women, wealth and wine. Vitabu vyote vya chase vinafanana. Mwanamke mzuri anasababisha mtu afanye mambo ya kipuuzi ikiwepo kuiba pesa na mwisho anakamatwa. Willy gamba ni tofauti vitabu vyote ni kuhusus hujuma ya mabeberu wa kimagharibi.sidhani kama anaiga hata kidogo, ila kuna jambo muhimu moja. Ukiwa unasoma vitabu vingi unajikuta unakuwa mkosoaji sana wa vitabu na iyo ndo njia inaweza kukufanya kuandika vizuri au kuwa na mawazo mapana. Kwa mfano tanzania nani mtunzi mzuri kati ya musiba, mtobwa au shingongo? Ntampa asilimia kubwa musiba kwa kuwa anjua namna ya kuvutia msomaji kila mara awe anajikuta ameingia kimawazo, mtobwa na joram kiango wake kwa kiasi anajitahidi ila ana tatizo moja la kuchanganya mambo mengi. Kuhusus shingongo, kwanza hana kipaji cha kuandika, analazimisha uku akisaidiwa na majarida yake, ila upeo wake ni mdogo wa ubunifu, na watu wataofurahia uandishi wake hawajasoma vitabu vya waandishi wazuri kama grisham. Shingongo ana tabia ya uandishi wa kuandika maneno mengi akifikiri kuandika sana ndo uzuri ila hawezi kuunganisha matukio kwa njia itakayo vutia msomaji