Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba)

hahaha, Mzizi wa Mbuyu, kwani ulikuwa na wasi wasi na wema wake?

Honestly Junius asante kwa hints, lakini inategemea sana na mtu uwe na contacts zanzibar, lakini nitafanyia kazi hii info, meanwhile kama kuna mtu ana contacts zingine hasa kwa DSM please atuambie,,,

Unajua nini mkuu, huyu Junius mara nyingi misimamo yake nilidhani ni mtu asie na wema kabisa kwa watu... lakini hivi karibuni ninaanza kumuelewa huwa anakuwa mtu wa kupoozapooza mambo tofauti na zamani alipokuwa kama anawakilisha jitu katili kabisa!
Mara mbili, tatu, nne hivi karibuni kaongea kiungwana mno!
 
Wow wow wow
Uzee kitu chema sana, nilishajisahau ila hiko kitabu sikufanikiwa kukiweka ktk kumbukumbu za usomwaji.
Nitakipata wapi??? ntakuwa dar hivi karibuni.

Nasikia UWT walienda nyumbani kwa Musiba wakachukua kilakitu kuhusu kitabu kile (HUJUMA) hadi muswada wa kitabu! wakadai eti kilikuwa na siri za nchi hivyo ni vigumu sana kujua kilikuwa nanini!?

.....Unakumbuka sura ya ...MREMBO LINA? kwenye Kufa na kupona?
 
Wow wow wow
Uzee kitu chema sana, nilishajisahau ila hiko kitabu sikufanikiwa kukiweka ktk kumbukumbu za usomwaji.
Nitakipata wapi??? ntakuwa dar hivi karibuni.

Sidhani kama amekitoa, nadhani amekubali yaliyopita si ndwele -kitabu chake cha mwisho ndicho hicho cha Uchu alichokitoa mwaka 2000.
 
Sawa kabisa mkuu..kuna hizi pia:

No business of Mine

I will get you for This

Hand me a Fig Leaf na

Have this one on Me

Umenikumbusha mbali sana muzee...
Sinyolita umenikumbusha mbali sana yaaani nimesoma kazi za Musiba na Chase nyingi but sijawahi kuzifananisha infact it didnt even cross ma mind till now! mpaka nikawa nataka kuwa mpelelezi nikiwa mkubwa hahahhaha.......nilikuwa O'Level i was a real fan, u make me think am tooo old maaana naona ni zamaaaani sana
 
Mbona hivi vitabu vipo tele tu katika maduka ya kuuzia vitabu "book shops", ingekuwa upo visiwani ningekuelekeza kwa Farouk Karim, Masomo BookShop, Darajani.
Bytheway, Huyu muandishi wa Riwaya hizi yupo wapi siku hizi, na anafanya kazi gani?
Nilizipenda sana kazi zake kama hizo ulizozitaja, lakini iliyonisisimua zaidi ni ile ya KIKOMO.

Alaa hivi masomo bookshop ni Farouk,sina habari ati.Kuna siku nilipita pale nilikuwa natafuta vitabu vya shabani Robert,sikumbuki kuviona vitabu vya Willy Gamba.Nitajaribu kwenda kuulizia,nakumbuka kuona vitabu vingi vya Joram kiango.
 
Baada ya kusoma Uchu ambacho amekiandika 2000 nimeondokana na dhana kuwa Musiba/Gamba alikuwa anagandamizia/desa. Kitabu hicho kimetafitiwa kwa kina maana kiko katika muktadha wa mauaji wa halaiki ya Rwanda hivyo ni rahisi kulinganisha matukio ya humo na matukio halisi ya kihistoria. Kwa ujumla hakuna mwandishi ambaye ni 'orijino' 100%, kila mmoja anaazima kitu fulani kutoka sehemu fulani. Kilicho cha muhimu ni umahiri wa mwandishi - kwa mfano Uchu inaanza na mazungumzo kati ya Gamba na Bosi wake ambao wote wamestaafu, Bosi anamwambia inabidi urudi ulingoni kama George Foreman. Gamba anakataa. Bosi anamwambia kama ni hivyo basi inabidi yeye Bosi aingie ulingoni. Inabidi Gamba akubali kazi maana Bosi ni mzee kupita kiasi hivyo itakuwa aibu kwake kuiachia kazi hiyo ifanywe na Bosi. Sasa hapo utaona kuwa mfano wa Foreman kurudi ulingoni ambalo lilikuwa ni tukio la kweli ulivyotumika kuleta utamu kwenye riwaya hiyo ya Uchu. Ubunifu ni uwezo wa kuboresha kilichopo.

Nakubaliana na wewe mkuu,jamaa alikuwa anajua.Kwa sasa sijaona,labda kidogo kuna jamaa anajiita husein Tuha,ametunga kitabu kimoja kinaitwa MKIMBIZI,jamaa mzuri uwezi kumlinganisha na akina Shigongo.
 
Alaa hivi masomo bookshop ni Farouk,sina habari ati.Kuna siku nilipita pale nilikuwa natafuta vitabu vya shabani Robert,sikumbuki kuviona vitabu vya Willy Gamba.Nitajaribu kwenda kuulizia,nakumbuka kuona vitabu vingi vya Joram kiango.

Mkuu ukiviona tujulishe, ni kweli kabisa vitabu vya Joram kiango vipo sana kwenye circulation, nadhani nimeshanunua na kusoma zaidi ya kumi, lakini hivi vya Willy Gamba naona inakuwa ishu kweli kweli!
 
"Si kazi yangu kujishughulisha na makosa ya jinai,nilishangaa kidogo chifu aliponiamuru kufuatilia tatizo la upungufu wa almasi kwenye mgodi wa mwadui" ah si mchezo mambo ya "kikomo",nayakumbukumba maisha yangu ya zamani enzi hizo starehe ni sinema /disco na Riwaya.... Njama,kufa na kupona,kikosi cha kisasi,kikomo,Hofu, kweli zamani tulipata starehe.

Yeah umenikumbusha mbali sana, utamaduni wa kusoma umekufa kwa vijana wa sasa hivi, zamani vijana kutembea na novel ilikuwa dili siku hizi vijana kutembea na CD/DVD au simu mbili mbili ndo dili.
 
Nakumbuka shambulio lilofanyika pale Butiama hotel shinyanga, nakumbuka kuna mtu alikuwa anaitwa Skazwe, nakumbuka kuna mtu alikua anaitwa Kabwe makanika au Jitu kumbuka, nakumbuka kuna dada alikua anaitwa Amanda si mchezo kabisa bila kumsahau Inspector wa Polisi, nakumbuka ile ajari ambapo treni iligonga gari ambalo Gmaba alikuwa amekodi kisha yule mtu akalipwa toka serikalini. vile vitabu havisahauliki.ila kwa ufupi mmiliki wa vitabu vile sijui sio mjasiliamali? kwa sababu akivirudisha kwenye market vitalipa sana.
 
du, tumetoka mbali, kwa kweli vijana wa o level kikindi hicho kila mtu alikuwa ni mpelelezi je mnakumbuka hii "KAZI na DAWA"
 
Musiba yuko somewhere kwenye serikali hii hii ya tanzania. ana wadhifa unaokaribiana au kufanana na ule wa Tido Mhando
 
wakuu naombeni msaada wenu kama kuna anayejua ninakoweza kupata hivi vitabu ya Elvis Musiba, vikiwa na stellingi Willy Gamba.

Vitabu hivyo ni kama vile:
1.Kikosi cha Kisasi
2.Kufa na Kupona
3.Hofu.
4.Njama
5.Uchu

na vinginevyo. nimevisoma baadhi zamani lakini sasa hivi sina nakala tena ningependa kujua ninakoweza kuvipata.

shukrani!

Ukikwama huko wenzangu walipokuagizia wasiliana na huyu jamaa mwnye namba 0754086314, anaitwa Elias aka Raju ni bingwa wa used books natumaini atakuanavyo!
 
Mkuu ukiviona tujulishe, ni kweli kabisa vitabu vya Joram kiango vipo sana kwenye circulation, nadhani nimeshanunua na kusoma zaidi ya kumi, lakini hivi vya Willy Gamba naona inakuwa ishu kweli kweli!

Hakuna shaka mkuu,nitapita leo halafu kesho Mungu akipenda nitakupa jibu.
 
Jamani vitabu hivi ndivyo vilivyonifanya mimi mwenzenu nikawa ni mpenzi wa picha, novels e.t.c. za kidetective........

enzi hizo nilikuwaga nafantasize Willy Gamba duh!! acheni tu

Hasa nlipokuwa nasoma Hofu mambo ya Nyaso mtoto wa Arusha
Na Willy alivyokuwa akijua kujifagilia ah!!
hapo nakukubali mkuuu mie nilikuwa obsessed na Gamba hadi nikawa na ndoto za kuwa mpelelezi nikiwa mkubwa nikaanza mpaka mazoezi ya kareti......... hahahaha nilivyokuwa mkubwa nikagundua hata kujipeleleza mwenyewe siwezi..
 
Nakubaliana na wewe mkuu,jamaa alikuwa anajua.Kwa sasa sijaona,labda kidogo kuna jamaa anajiita husein Tuha,ametunga kitabu kimoja kinaitwa MKIMBIZI,jamaa mzuri uwezi kumlinganisha na akina Shigongo.
hapo nakuunga mguuu mkuuu Hussein Chuwa anafata nyayo za akina Musiba na Kiango nimekisoma hicho kitabu kizuri sana , jamaniiiii shigongo anabore na hadithi zake zinazofanana na picha za kinigeria na kisha kujirudiarudia nilikuwa mpenzi wa hadithi zake lakini baada ya kusoma nne tu nikajua jamaaa amefulia huyuuuuu mpaka leo sijagusa hata moja maana naona uzushi tu bora niangalie 24hrs kuliko kuangalia tafsiri za movie za kinigeria
 
Nakumbuka shambulio lilofanyika pale Butiama hotel shinyanga, nakumbuka kuna mtu alikuwa anaitwa Skazwe, nakumbuka kuna mtu alikua anaitwa Kabwe makanika au Jitu kumbuka, nakumbuka kuna dada alikua anaitwa Amanda si mchezo kabisa bila kumsahau Inspector wa Polisi, nakumbuka ile ajari ambapo treni iligonga gari ambalo Gmaba alikuwa amekodi kisha yule mtu akalipwa toka serikalini. vile vitabu havisahauliki.ila kwa ufupi mmiliki wa vitabu vile sijui sio mjasiliamali? kwa sababu akivirudisha kwenye market vitalipa sana.

Mkuu umechanganya kidogo Kabwe unyama wa mafia mkubwa.
 
hapo nakuunga mguuu mkuuu Hussein Chuwa anafata nyayo za akina Musiba na Kiango nimekisoma hicho kitabu kizuri sana , jamaniiiii shigongo anabore na hadithi zake zinazofanana na picha za kinigeria na kisha kujirudiarudia nilikuwa mpenzi wa hadithi zake lakini baada ya kusoma nne tu nikajua jamaaa amefulia huyuuuuu mpaka leo sijagusa hata moja maana naona uzushi tu bora niangalie 24hrs kuliko kuangalia tafsiri za movie za kinigeria

Pia hadithi zake hazina uhalisia.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom