fige
JF-Expert Member
- Jul 4, 2010
- 376
- 61
wakuu fuatilieni hii habari maana itv walisema kuwa hivi vitabu vimeshakubaliwa na vimeingizwa kwenye mitahala ya shule za msingi ambapo vitatumika kuanzia darasa la V - VII (darasa la tano mpaka saba). Na pale miongoni mwa waliokuwepo ni Nyambari Nyamgwine, kwa hiyo msishangae hivi vicheko vyenu vikaishia kwenye vilio maana sina uhakika ni taasisi gani iliyo hakiki na kuthibitisha kuwa hivi vitabu vinaweza kujenga vision za watoto wetu.
Kikubwa hapa ni kuwa watu wako kwenye biashara maana zikichapwa nakala milioni 2,000,000 na nimeona wanasema bei yake ni 5,000/- @ nakala!
Mzee Makamba kawa wazi kabisa kwani kaomba vinunuliwe ili kumsaidia apunguze umaskini wake .
Nina wasiwasi kama kitakochozingatiwa ni ombi hilo au ubora wa vitabu