Vita ya democracy Tanzania

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
VUGUVUGU HILI LA KUTAKA DEMOCRACY IACHWE KUKANDAMIZWA SIO KWA TUNDU LISSU WA CHADEMA AU ZITTO KABWE WA ACT-WAZALENDO TU

HATA KIPINDI CHA UKOLONI NYERERE PIA ALISHTAKIWA NA WAKOLONI MWAKA 1958

Na Comred Mbwana Allyamtu

Watu wengi hawajui kuwa uhuru wa Tanganyika na baadaye Tanzania Desemba 9, 1961 ulipatikana kwa mapambano makali hata kama damu haikumwagika.

Miongoni mwa wapambanaji wakuu wakati huo alikuwa ni Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliamua kuacha kazi ya ualimu na kujikita kwenye siasa akiwa kiongozi wa Chama cha Tanu alijikuta matatani.

Mwalimu Nyerere alistaafu ualimu Machi 23, 1955 akiwa anafundisha Shule ya Sekondari ya Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ili ajikite zaidi kwenye siasa.

Wakati huo, Tanganyika kama nchi nyingine za Afrika ilikuwa na Serikali halali ya kikoloni iliyokuwa ikiongozwa na Gavana Richard Turnbull.

Kesi ya Nyerere

Mwandishi wa kitabu cha Kesi ya Julius Kambarage Nyerere 1958, Simon Ngh’waya anaeleza sababu ya Mwalimu Nyerere kushtakiwa kuwa ni kutokana na maandishi yake kwenye gazeti la ‘Sauti ya Tanu’ la Mei 7, 1958, baada ya kusema wakuu wa wilaya wanakihujumu Chama cha Tanu kwa kuyafunga baadhi ya matawi yake na pia kuwachukulia hatua kali machifu waliokuwa wanaunga mkono.

Katika makala hayo, Mwalimu Nyerere aliwaita wakuu hao wa wilaya kuwa ni ‘washenzi na maharamia’. Katika ukurasa wa saba wa kitabu hicho, Mwalimu Nyerere anaandika:

“Naiomba Serikali ya kibeberu, itamke wazi kwamba inaishambulia Tanu kwa sababu tumetangaza bila woga kuwa Serikali ya kimabavu tutaipiga vita. Tutaishambulia bila kupumua mpaka tumeiangusha …ndugu wananchi, jihadharini, adui anashindwa, anaanguka kwa sababu hana njia za kupinga kilio chetu. Njia yake ni moja tu nayo ni kutaka ghasia ili akatumie bunduki. Tusimpe nafasi …adui atateketea bila shaka.

“Nilipofikiria utu wa binadamu, ninapotambua kwa kuwa sijajaliwa kuwa mtu anayestahili sheria na furaha ya tabia, nachukia kutawala binadamu kwa nguvu na udanganyifu kama vile maharamia na wajinga. Naona uchungu kwa wale wanaokandamizwa.”

Kitabu hicho kinafafanua kuwa maneno kama Gavana wa msituni, washenzi, maharamia yalitafsiriwa kuwa ni kashfa kwa Serikali ya kikoloni, hivyo Mwalimu Nyerere alishtakiwa kwa kuikashifu Serikali.

MY TAKE:
Nilazima tutambue kuwa nchi yetu ni ya kidemokrasia kikatiba na kisheria hivyo mtu yeyote hapasi kuichezea haki hiyo ya kitatiba. Sio busara kuifanya nchi sehemu ya fikra za mtu tunapaswa kuwa sehemu bora ya kutejeleza maazimio ya katiba yetu.

Ndimi
comred Mbwana Allyamtu.

+255765026057
+255689555526.
Mbwanaallyamtu990@gmail. Com
1469685152766.jpg
 
Back
Top Bottom