Vita ya Arumeru ni ngumu kwa CCM kuliko ilivyokuwa IGUNGA: Chadema tujipange

Kinachokutisha wewe ni mzimu wake sio kitu kingine, kifo cha huyu ndugu hakikuwa msiba kwa familia yake tu, ni msiba kwa watanzania wote wanaoheshimu democrasia na utawala unaofuata sheria.

Hii ni kumbukumbu ya ukatili wa serikali dhidi ya watu wake chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi, ni lazma tukumbushane historia hii sababu tunajijua sisi kama binaadamu ni wepesi sana kusahau.

tutaendelea kukumbushia kifo hiki na vingine vyote vya namna hii hata baada ya kukiondoa chama hiki madarakani, hata wakati wa kikomo cha furaha katika Taifa letu, tutakumbushana kwa picha hizi kwamba tulikotoka hapakuwa salama, hakukuwa na amani wala utulivu ili tusijetukaruhusu wauaji wengine kutuongoza.

Ni rahisi kujitia utukufu na kukosea wengine heshima kwa vile huna vinasaba nae

Angelikuwa baba yako usingethubutu kutamka haya
 
Crashwise!

Nakwapia ya kwamba tupo makini maradufu ya wanasisiem wanavyowaza.

Tuna uhakika ya kwamba makamanda wapo macho zaidi ya!

Huu msako ni wa nyumba hadi nyumba lango hadi lango!
 
Asante kwa kutukumbusha ukatili wa CCM!!
Mwigulu Nchemba aliongoza mauaji ya raia wasio na hatia Igunga.



Wakuu, mkimpatia site akiwa anagawa hela hebu mtieni adabu!!
Mwigulu ni hatari sana

attachment.php
 
Hawa jamaa wameisha sera aisee! Hivi mtu akiweka picha ya maiti ya Chacha Wangwe humu Jamvini akasema kauliwa na Chadema itakuwa sahihi?


Ndiyo, itakuwa sahihi kama utaweka na vidhibitisho kuonyesha kuwa si CCM ilimua kusaport hiyo picha.
 
Kampeni za Igunga zilituacha wana chadema na msiba wa kada/wakala wetu alie uwawa na wanaccm...
Natambua jukumu la kulinda watanzania ni la serikali ya CCM na si la CHADEMA lakini hatuwezi kukaa kimya tukiona wenzetu wakiteketea, kwa hali ilivyo hapa Arumeru CCM tumewazidi sana si ajabu siku za mwisho mwisho wakachukua maiti hata mochuari na kuweka barabarani ili ionekane CHADEMA tumefanya mauji kama probagada za kutafuta kura za huruma kwani hali ya CCM huku Arumeru ni mbaya mno na je tumejipangaje kulinda usalama wa makada/mawakala wetu....
View attachment 50285

Angalia unachotumwa kufanya na signature yako, ndicho hicho wenzako wanawahi kukufanyia.
 
Ndiyo, itakuwa sahihi kama utaweka na vidhibitisho kuonyesha kuwa si CCM ilimua kusaport hiyo picha.

Ulimbo,
Mbona hilo la Chacha Wangwe, lipo wazi usitake tuanze kufunguka.
 
Mwigulu mwigulu kabla hujafa yatakurudi kama si wewe basi mtu anayekuhusu kabisa
 
Mtu mwenye akili timamu huwezi kudhalilisha marehemu kwa lengo la kutafuta sifa mtandaoni.

Unafufua machungu yasiyo ya lazima kwa ndugu zake.

Sikujua uwezo wa kufikiri wa Crashwise uko chini kiasi hiki.

Hata hivyo bado hajachelewa, atakuwa amemtendea haki marehemu na ndugu zake iwapo ata-edit na kuiondoa hii picha.
 
Aisee ni ukatili wa hali ya juu, yaani wanaua kwa sababu ya tofauti za kisiasa? wananchi tuamke tukatae huu ukatili. Ila ninaimani haya mambo yao yatapita na watz tutakuwa huru again.
 
Mtu mwenye akili timamu huwezi kudhalilisha marehemu kwa lengo la kutafuta sifa mtandaoni.

Unafufua machungu yasiyo ya lazima kwa ndugu zake.

Sikujua uwezo wa kufikiri wa Crashwise uko chini kiasi hiki.

Hata hivyo bado hajachelewa, atakuwa amemtendea haki marehemu na ndugu zake iwapo ata-edit na kuiondoa hii picha.
Lazima tuangali tunakotoka ndiyo tuangalie tuendako....Ni tahadhari tu mkuu hata hivyo tunatofautiana mitazamo sitegemeei kama mimi niko 100% kwa chocho ninacho kiweka hapa....Jiulize CCM juzi walikuwa wana gawa magazeti ya kijana alimwagiwa tindikali na vijana wa nape sasa kilicho nisukuma ni baada ya kuhubiri yaliyotokea wanaweza kufanya hivyo hivyo ili kuthibitisha wanayo yahubiri....
 
Ulimbo,
Mbona hilo la Chacha Wangwe, lipo wazi usitake tuanze kufunguka.
Ndiyo maana tunataka hii serikali ya CCM tuiondoe madalakani imeshindwa kulinda wanacnhi wake inacho jua ni kuua, kumwangia maji ya kuwasha na kupiga mabomuya machozi...
 
Wakenya wana kitu inaitwa "Picha mitaani" ambapo wana specified locations(mostly city centers), ambazo kuna picha zimebandikwa za matukio ya waliopoteza maisha kwenye vuruga za kisiasa zilizochochewa na ukabila wakati wa uchaguzi wao mkuu.

Hopefuly hizo picha zitawasaidia kujuwa unyama uliofanyika na hivyo kujilinda ama kuhakikisha hayatokei tena.

Same with us, picha ni gross lakini a leson from it is worthy.
 
Wabongo kwa unafiki, wakikumbushwa dhuruma na utovu wa haki wanataka kujifanya oh haki za binadamu....
Wakati hayo yalipotokea Igunga hao hao walisema CDM ni walalamishi....
Safi CW kwa kuweka ukweli mchungu, ila aisee Arumeru yasitokee hayo ni kukaba hao mafisi wasipate hata pakupumulia
 
huyu jamaa aliuawa na cdm baada ya kuona hayuko nao wakaona atawalipua mana kwa ndani aligundua cdm wanamtumia kwa maslahi ya kisiasa af kwa kuwa ni mwislam ndio mana walimuua
 
huyu jamaa aliuawa na cdm baada ya kuona hayuko nao wakaona atawalipua mana kwa ndani aligundua cdm wanamtumia kwa maslahi ya kisiasa af kwa kuwa ni mwislam ndio mana walimuua
Kama ni kweli basi hii serikali ya CCM tuungane tuing'oe imeshindwa kulinda usalama wa watanzania wakati mwenyekiti wa CCM aliaapa kuilinda katiba ya tanzania ambao ni pamoja na usalama wa Tanzania...
 
Chadema bana sasa hii ndio nini kuweka maiti kama mtaji wa kisiasa.
Nawapenda cdm na naombea washinde jimbo lakini ukweli sijaona mantiki ya hii picha/maiti kuwekwa hapa. Crashwise unataka kumaanisha nn?unaihusisha maiti hii na kampeniarumeru kivipi? marehemu ninani na aliuawa/fariki wapi?
 
Mkuu itoe hiyo picha maana haijakaa vizuri inatisha. Kutisha siyo sababu kuu ila kimaadili haifai mtu aliyekufa tena katika hali ambayo hata hajaifadhiwa ni kama kumdhalilisha. Pls Crashwise fanya hivyo kama utaona inafaa.
 
Kama aliuliwa ndio inaondoa heshima anayotakiwa kupewa yeye na jamaa zake?

Jiulize angekuwa baba au kaka yako ungefurahi picha yake itumike hivi?
Laana za maiti kama huyu na wengine wengi ndizo zinazokipeleka kaburini chama cha Magamba. Mungu hatawasamehe kamwe kwa ukatili kama huu, na hata Shetani naye ameshaanza kuwakataa!
 
Back
Top Bottom