Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Mzalamo nani kakwambia kuwa wakati wa vita vya kagera hatukuwa na silaha nzuri, kawaulize jamaa wa kule Msumbiji na Angola watakwambia habari zake. Tulikuwa na vifaa vizuri na magari ya deraya yaliyokidhi hali ya wakati ule, tena naweza kusema ni vifaa bora kabisa vya kijeshi. Kwani tulikuwa na mkusanyiko wa siraha kutoka Burgaria, China, Urusi na Iraq.
Isitoshe pia Jeshi lilikuwa na uzowefu tayari, ndio maana hata Jeshi Kaburu lilikuwa linahara kila vijana anapotia timu kule kusini mwa Afrika.
Vita vilitokea wakati nchi za magharibi na mashariki zipo kwenye vita baridi. Hivyo zana nyingi zilikuwa zinatolewa kama pipi. Hata majeshi ya rebels kama ya Savimbi na Afonso Dhlakama yalikuwa na vifaa bila kuwa na revenue yoyote hile.