Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Sababu ya kwanza ni utawala wa kidikteta wa idd amin uganda kubomoa daraja la mto kagera mtukula na maneno ya kebehi kwa baba wa taifa pia alitangaza kwamba kagera ni sehemu ya uganda na alichoma bendera ya taifa na ya chama cha mapinduzi hadharani vilevile alisema anataka jeshi lake lifike mpaka dar es salaam yaani liiteke dar jamaa alikua anajiamini sana kwasababu alikua anaona tu kwamba sisi watanzania ni wapole sana kumbe uwezo tunao na nguvu tunayo nadhani waganda mpaka leo wanatuogopa maana tulipiga mpaka tukatokezea ethiopia!

Hakuna ukweli hata chembe ktk hili unalolisema.
 
Mwaka 1977/78 wewe ulikuwa uzaliwa? Kuna sababu gani ya vita zaidi ya nchi kuivamia nchi ingine?

Amini aliivamia Tanzania, akatangaza mpaka mpya kuwa ni mto kagara kiasi cha kilomita 25 hivi ndani ya mipaka ya Tanzania, wananchi watanzania wenzetu waliokuwa wanaishi maeneo yaliyotekwa walifanyiwa unyama na wengine kuuawawa bila makosa.

Jina sahihi la vita ya kagera ni "Vita ya Ukombozi wa Kagara" Ndiyo maana Nyerere alipounganisha vita ya ukombozi na vita ya kumwondoa Amini Madarakani Uganda Umoja wa Mataifa haukumlaani kama ilivyo kuwa kwa G W Bush na Sadam Hussein. Actually, Waamerika walii copy Tanzania kama precedent ya nchi kumwondoa madarakani raisi wa nchi ingine wakati wa sakata la iraki huko UN.
Ukweli wa vita ya kagera unaujua ila hapa umeuliza tu kiunaafiki, una ajenda yako mwenyewe ambayo unaona aibu kuiweka wazi.

Kama ungekuwa siyo mnafiki ungeuliza ni kwa nini Amini alikimbilia Saudi Arabia au ni kwa nini Gadaffi alileta majeshi kumsaida Amini

Acha uongo wewe! Nyerere alilaaniwa na mataifa mengi ya dunia kwa uvamizi wake Uganda na ndio maana TZ haikupata msaada wowote baada ya vita na gharama zote za kulinda amani Uganda na ndio chanzo cha kuporomoka kwa uchumi wetu.
 
Hidi Idi Amin alichaguliwa kwenye uchaguzi gani kuingia madarakani uliompa uhalali wa kuwa Rais wa nchi huru?

Acha upotoshaji wewe mzee. Unahoji Idd Amin aliingiaje madarakani ili uhalalishe kung'olewa kwake?!!! Mbona huyo Obote ambaye alikuwa kipenzi cha Nyerere aliingia madarakani baada ya kumpindua kabaka?!!! Soma vizuri historia ya Uganda utaona kuwa mara baada ya kupata uhuru wake mwaka 1962 Obote alikuwa ni Waziri Mkuu na Rais alikuwa kabaka ambaye sikumbuki jina lake kwa sasa.
 
Kwanini Obote alikuwa Tanzania?
Kabla ya kuja Tanzania Obote alikuwa na cheo gani kabla huko Uganda na alikipotezaje hicho cheo?

Kwahiyo TZ ndiyo ilikuwa sehemu ya kuja kushtakia kesi yake?!!! Mbona Nyerere hakwenda kumkomboa Lumumba alipokamatwa na wanajeshi wa Kasavubu na mwenzake Shombe?
 
narudia kusema kweli ata mi sikuipenda vita ya mkoa wangu lakini wazee wangu na shangazi zangu ambao hata walikuwa wanajeshi wanathibitisha kuwa Idi alikuwa jitu mbaya sana. Kwa kuwatelekeza mtoni wasio na hatia ilinikwaza sana. Nichoomba ni kuwa ile vita isingehusishwa na udini. Pia idi ndo aliyetungua daraja la kagera na ghafla wanajeshi wa Tz kwa kutumia vifaru na vyuma walijenga jipya ndani ya masaa na kuvuka mpaka,apa idi ndo aliposhtuka na kukimbilia kijijini Arua. Mambo yako wazi ila wachangiaji wanaedit history ili iendane na 'market' demand ya sasa ya wasikilizaji.

Maneno ya mtaani haya.
 
Wakuu huu ndio ukweli kuhusu Idd Amin, mkumbuke kwamba katika miaka ile ya 70, Tanzania chini ya Mwl Nyerere ilikuwa nchi mstari wa mbele katika ukombozi wa Afrika. Idd Amini Dada yeye ndiye aliyemsaidia Dk Milton Obote kuingia lkulu, baada ya kuchukua kikosi cha Jeshi na kwenda kumpindua Kabaka katika Ikuru ya Uganda ambapo Kabaka aliwekwa na waingereza na alikuwa kibaraka wao, baada ya Amin kuchukua ikuru alimkabidhi obote na yeye akawa mkuu wa majeshi ya Uganda kwa kuwa yeye obote alikuwa na shule wakati huo, na mjue kuwa Amini na Obote walikuwa ni marafiki wakubwa na Amini alikuwa anapendwa na wanajeshi wote, baada ya muda mwaka 71, Obote alimtuhumu idd Amin kwamba ni Mla rushwa, ndipo Amin alipohisi hatari na kwa kuwa jeshi lote lilikuwa mikononi mwake, alimvizia Obote alipokwenda kwenye mkutano wa Commonwealth country's akampindua. Obote alikuwa rafiki wa Nyerere sana, kitendo cha kupinduliwa Obote kilimuuzi sana Mwl na akampa hifadhi Obote, haikuishia hapo Mwl akawa anamsaidia Obote ku train askari gollilar fighters ili kwenda kumwondoa Amini, kitendo hiki kilimuuzi sana Amini mpaka akamwandikia Telegram Mwl ya kumtukana, hayo maneno siyasemi, chokochoko hiyo ilianza miaka hiyo ya 72, baada ya Amin kuchoshwa na vitendo vya Gollila fighters kuvamia Uganda kutokea Tz ndipo mwaka 78 alipotangaza kwamba atapiga mpaka DSM, na kweli alivamia Kagera kwa jeuri aliyopewa na Gadaffi kwamba atamsaidia mpaka mwisho, ikumbukwe pia mwaka 72 vita ilipiganwa kidogo na mkuu wa Polisi kituo cha mpakani TZ aliuwawa na kuchukuliwa na Amini na kuwekwa kwenye jokofu, mwili wake ulikuja kupatikana baadae...endelea kuwa na mimi kwa simulizi yote ya vita vya Kagera itaendelea.......
Mkuu endeleza iyo story
 
Kilimasera ukiona mdogo wakoa anampiga ngumi mwezio na mwenzi akarudishia mkorofi ni yule aliyeanza kurusha ngumi??

Tafuta Literatures, uliza waganda, nenda kulia nenda kushoto......

Uganda mpaka leo wanamkumbuka Amin! ambaye wewe unamwona dictator

Amin aliua makumi
Obote kaua maelfu
Museven kaua makumi elfu.......

Kwa kufupi mkuu, Nyerere alikuwa na mtu ambaye anatakwa sana na Amin..Mr.Obote,

kwa kifupi ulikuwa mpango wa Nyerere kumuweka Obote madarakani!!! yale ya kagera n.k ni hasira za Amin, ukweli NYERERE NDIYE ALIKUWA MKOROFI!!!!!
Nimechelewa sana kusoma hii thread ila kama bado upo active basi nina mashaka na uraia wako
 
Vita ya Kagera na sababu za KIDINI. Nitafafanua. Idd amin alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao ni mwiba kwa mataifa ya Marekani na Uingereza. Alikopa fedha WB kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake alijenga msikiti ambao unakadiriwa kuwa ni mkubwa ktk A.Mashariki. Na alikuwa mbioni kutangaza Uganda kuwa nchi ya kiislam kitendo kilichowakasirisha mabwana hao wa ulaya.

Ilikuwa ngumu kwa wao kujiingiza 1kwa1 ktk kumuondoa madarakani na badala yake wakaamua kuitumia tz km walivyofanya kule NJUWANI huku wao wakiwa nyuma ya tz kwa kutoa silaha za kivita. Pia Nyerere alikabidhiwa eneo lote la A.Mash.kuusimamia ukristo na kuuendeleza. Hivyo ilikuwa ni lazma awajibike ipasavyo.

Kwa kusema ukweli Tz hatukuwa na uwezo wa kumng'oa Idd Amin wala kule NJUWANI. Pia kuhusu kula nyama za watu, hakuna kitu km hicho hata hizo filamu wametengeza haohao(marekani na uingereza) ili kunakshi uongo wao watu waamin kile walichofanya. Mifano mingine ni sudani na angola (huu ni mjadala unaojitegemea).

Nyerere hakuwa na 'UWEZO' wala 'NIA' Na huo ndio ukweli wenyewe mkuu.
Huo Ni uongo nchi za magharibi ziliitenga coz ujamaa
 
Sababu ya kwanza ni utawala wa kidikteta wa idd amin uganda kubomoa daraja la mto kagera mtukula na maneno ya kebehi kwa baba wa taifa pia alitangaza kwamba kagera ni sehemu ya uganda na alichoma bendera ya taifa na ya chama cha mapinduzi hadharani vilevile alisema anataka jeshi lake lifike mpaka dar es salaam yaani liiteke dar jamaa alikua anajiamini sana kwasababu alikua anaona tu kwamba sisi watanzania ni wapole sana kumbe uwezo tunao na nguvu tunayo nadhani waganda mpaka leo wanatuogopa maana tulipiga mpaka tukatokezea ethiopia!
Iddi amin alifanya mambo gani mpaka aitwe dictator? Mbona hata mwalimu alifanyya mambo mabaya tuu
 
Vita ya Kagera na sababu za KIDINI. Nitafafanua. Idd amin alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao ni mwiba kwa mataifa ya Marekani na Uingereza. Alikopa fedha WB kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake alijenga msikiti ambao unakadiriwa kuwa ni mkubwa ktk A.Mashariki. Na alikuwa mbioni kutangaza Uganda kuwa nchi ya kiislam kitendo kilichowakasirisha mabwana hao wa ulaya.

Ilikuwa ngumu kwa wao kujiingiza 1kwa1 ktk kumuondoa madarakani na badala yake wakaamua kuitumia tz km walivyofanya kule NJUWANI huku wao wakiwa nyuma ya tz kwa kutoa silaha za kivita. Pia Nyerere alikabidhiwa eneo lote la A.Mash.kuusimamia ukristo na kuuendeleza. Hivyo ilikuwa ni lazma awajibike ipasavyo.

Kwa kusema ukweli Tz hatukuwa na uwezo wa kumng'oa Idd Amin wala kule NJUWANI. Pia kuhusu kula nyama za watu, hakuna kitu km hicho hata hizo filamu wametengeza haohao(marekani na uingereza) ili kunakshi uongo wao watu waamin kile walichofanya. Mifano mingine ni sudani na angola (huu ni mjadala unaojitegemea).

Nyerere hakuwa na 'UWEZO' wala 'NIA' Na huo ndio ukweli wenyewe mkuu.
Rubbish

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile ni vita ya kidini nilivyosikia mimi kwa wakongwe!mambo yale yalikuwa ya kivatcan against muslim ndo mambo mengine tukadanganywa oooh anakula nyama za watu yote ile ni kujastify tu ili wamvamie. Ila angekuwepo mpaka sasa hivi uganda ingekuwa nchi ya kiislam. baba wa taifa alikuwa mroman karibu sana na papa!
Na ule urafiki na Gadaffi uliwatishia amani sana.
haya na mimi niliyasikia tu
Takataka za kale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom