Vita ni vita

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Siku moja nilisikia Rijamaa Rimoja Rinasema , "VITA NI VITA MURA", sikujua huyu jamaa alikuwa na maana gani?. Kumbe vita ya maneno ndiyo mbaya kuliko hata ile ya kushika SILAHA. Nadhani hii inatokana na ukweli kwamba, kabla ya vita ya kushika mtutu ni lazima ianze ile ya maneno ambayo madhara yake ni makubwa.

Ni vita hii ya maneno mengi yakiwa ya uongo kutoka vyama vya upinzani na nyingine ndani ya CCM wenyewe ndiyo inasababisha watanzania wengine tudanganyike na kuamini eti Serikali ya JK haifanya kitu na hakuna jambo la msingi la kufanya vita hii iwepo bali tu RAIS wangu JK awe ndiye wa kulaumiwa na lengo haliishii hapo bali eti mwisho wake na wengine wapate kuingia IKULU baada ya kushinda vita hii ya maneno.

Kuna nini jipya katika vita ya maneno inayoendeshwa na makundi ndani ya CCM kama siyo chuki inayotokana na baadhi ya watu hao kukosa nafasi walizoaidiwa huku wengine wakiwa na hasira ya kupoteza nafasi zao baada ya kuonekana wazi hawakujiandaa kwa moyo wa dhati kuwatumika watanzania bali matumbo yao. Tujiulize swali hapa, hivi kweli wote wangeweza kupata kazi kwa ujumla wao? aidha kwa wale waliopoteza nafasi zao wanataka kutuambia kwamba walionewa au ni chuki ya kunyang'anywa tonge mdomoni? na kama walionewa si waseme wazi sisi tulionewa na ukweli ni huu.
Nikija upande wa UPINZANI una macho mawili lakini umefunga jicho moja lillokuwa linaona mazuri yaliyofanywa na RAIS wangu KIKWETE na kubakiza jicho lile ambalo si kwamba linaloona mabaya tu bali linadiriki hata kukonyeza watanzania kuwa kataeni kufanya kazi zinazoelekezwa na Serikali ya JK. Yapo mambo mengi ambayo yamesemwa na wapinzani kuhusu Serikali na bila hatua tunazoshauriwa na wapinzani hawa kuchukua ni kuandamana, kugoma, kukataa kushiriki shuguli za maendeleo, kukataa kutii kuheshimu sheria na taratibu za nchi, kuwazomea viongozi kila wanapopita na pale wanapokuwa na wananchi kutekeleza majukumu yao. Je ndilo suluhisho? ama ni njama za kutaka tupoteze muda bila kufanya kazi ili lawama zizidi kumwendea Rais wangu?

Sitaki kusema sana kuhusu hili la wapinzani kwa vile najua wao malipo yao yapo. Masema malipo yao yapo kwa vile tayari wameshatufundishwa kuwa Rais hatakiwi kusafiri, kazi ya kuwaletea maendeleo ni ya Serikali na siyo wananchi wenyewe, migomo ni haki ya kila mtu, maandamano ni haki bila kujali ni halali au la. Wameshatufundisha kuwa ni marufuku kuheshimu sheria za nchi na zaidi wameshatufundishwa kuwa kuwazomea/kuwakashfu/kuwadhihaki viongozi ndiyo demokrasia ya kweli. Hivyo basi watakapoingia madarakani wakatugeuka kutekeleza hayo bazi itabidi wakabiane na nguvu zaidi.


JK PAMBANA VITA NI VITA TU, TUNAKUAMINI.
 
Back
Top Bottom