Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
UPDATES
========
- Ndege za kivita za Marekani zimeteketeza kiwanda cha kuunda magari ya kutumia kwenye vita kichokuwa kikitumiwa na magaodo wa ISIS na hakuna kilichosalimika.
- Magaidi wa ISIS wamenza kutumia mabomu ya kujitoa mhanga na kuwashambulia majeshi ya kikurdi.
- Kuna uwezekano mkuwa magaidi wa ISIS wakatumia silaha za kikemikali pamoja na mabomu ya kujitoa mhanga.
- Tayari vijiji kadhaa vimekwishakombolewa na vikosi vya Peshmerger ambavyo vinasogea kuelekea katikati ya mji wa Mosul, bado hakuna majehi yaloingia ndani ya mji.
Operesheni mpya kubwa kabisa kufanywa ndani ya nchi ya Iraq inaanza leo na majeshi ya Iraq yanajianda kwa vita tarakitu ndani ya mji wa Mosul iliopo magharibi mwa nchi hiyo.
Peresheni hiyo inahusisha vikosi vya majeshi visivyopungua 30,000 vikiwa ni vikosi vya waasi wa kikurdi kiitwacho Peshmerga, vile vya mgambo vya Iraq na jeshi lenyewe la Iraq.
Lengo kuu la operesheni hii ni kuwandoa wapiganaji wa ISIS ambao wanakisiwa kuwa kati ya 8,000 na 10,000 mbao waliuteka mji huo mwaka 2014 mji wenye wakazi wanaokisiwa kuwa ni milioni 1.5
Mji wa Mosul ni mji wa kimkakati na unapakana na nchi ya Syria kwa upande wa mashariki operesheni hiyo itahusisha ndege za kivita za Marekani, Australia, Itali, Ufaransa na Uingereza pamoja na vikosi maalum vya ardhini vikiwemo vile vya majini vya Marekani, vikosi maalum vya Italia na Uingereza, Ujerumani na Canada.
Usiku wa jana vipeperushi vilikuwa vikiangushwa kwa wakazi wa mji huo kuonywa kujiandaa na vita hiyo ambayo haijawahi kutokea kwenye miaka ya hivi karibuni.
Lengo kuu ni kuwashambulia ISIS kadari inavyowezekana kwa mashambulizi yanayotokea kusini, mashariki na kaskazini ambapo upande wa magharibi utaachwa wazi ili kuwaruhusu magaidi wa ISIS kuelekea huko.
Upande wa magharibi mwa mji wa Mosul utaachwa wazi ili kuwanusuru magaidi wa ISIS ambao watataka kuelekea upande huo.
Mkuu wa majeshi ya nchi shirikishi Luteni jenerali Stephen Townsend amesisitiza kwamba vikosi vya ardhini vya Iraq ndivyo vitakavyokuwa vikiendesha operesheni hiyo.
Inaaaminika kwamba Marekani na nchi wahisani watatumia ndege zisizo na abiria yaani drones na ndege zeingine za kawaida za kivita kusaidia operesheni hiyo.
Waziri mkuu wa Iraq bwana Heider- al- Abadi alitangaza juu ya operesheni hiyo jana jioni nchi humo na kuwataka wananchi wawe watulivu kusubiri mji huo wa Msul kukombolewa.