Visigino kuuma

Dandaj

Member
Apr 16, 2009
73
2
Tafadhali naomba mnisaidie, Visigino vyangu vinauma na nikinyanyua unyayo kwenye kisigino pana vuta kwenda chini kama pamefungwa kajiwe kadogo.

Naomba msaada wenu wa kitabibu.
 
Nilishawahi pata maumivu kama hayo. Lakini sasa wewe unafanya kazi gani? au huwa unatembea umbali mrefu au kupanda ngazi/mlima very often?

Kwa upande wangu nilipopatwa na maumivu haya nili-ignore kutokana na kazi niliyokuwa nafanya kwa hiyo automatically I knew it was a cause...na maumivu yalitoweka yenyewe.
 
Tafadhali naomba mnisaidie, Visigino vyangu vinauma na nikinyanyua unyayo kwenye kisigino pana vuta kwenda chini kama pamefungwa kajiwe kadogo. Naomba msaada wenu wa kitabibu.

...jaribu kupunguza uzito,...fanya mazoezi, kimbia, cheza mpira...nk

nilikuwa na matatizo kama hayo kwa muda mrefu, nilidhani ni kutokana na majira ya baridi, lakini tangu nimeanza mazoezi, ni mwaka sasa sijasikia tena maumivu.
 
Check viatu unavyovaa - vya msonge vyaweza kusababisha visigino kuuma

Ukosefu wa mazoezi, au kufanya mazoezi makali bila "warm up"

Matatizo ya ki-anatomy ya miguu kama "flat feet" na deposition ya calcium stones - unaweza ukawaona wataalamu, X-rays zinasaidia ku-diagnose matatizo haya.

Matatizo ya mishipa ya fahamu, pia ongea na wataalamu; jaribu kula multivitamins zaweza kusaidia.

MAUMIVU YAKIZIDI .....?
 
Tafadhali naomba mnisaidie, Visigino vyangu vinauma na nikinyanyua unyayo kwenye kisigino pana vuta kwenda chini kama pamefungwa kajiwe kadogo. Naomba msaada wenu wa kitabibu.

Umeshamwona daktari? Amekupa ushauri gani?

Kama bado unetegemea utatibu wa kwenye www, unacheza wewe.
 
Nimeheshimu mchango wa kila mtu na nimeuchukulia katika mtizamo chanya. Asanteni sana kwa michango yenu.
 
Kijana punguza ile kitu roho inapenda....the KTM......kwikwikwi(joke)!

Piga zoezi morning & jioni itaisha......achana na minyama uzembe!
 
Mkubwa njia rahisi ya kukusaidia weka mafuta ya mgando kwenye kisigino then koleza jiko la mkaa au chemsha maji kwenye birika then weka mguu ulopakwa mafuta kwa juu ili mvuke uchome kisigino maumivu yakizidi unatoa na unarudisha tena several times baada ya muda yataisha mie ni footballer na mara nyingi inatokea hasa kama navaa viatu vyenye njumu katika uwanja mkavu jaribu pia kuvaa viatu flat mara nyingi zaidi unapopata nafasi
 
mkubwa njia rahisi ya kukusaidia weka mafuta ya mgando kwenye kisigino then koleza jiko la mkaa au chemsha maji kwenye birika then weka mguu ulopakwa mafuta kwa juu ili mvuke uchome kisigino maumivu yakizidi unatoa na unarudisha tena several times baada ya muda yataisha mie ni footballer na mara nyingi inatokea hasa kama navaa viatu vyenye njumu katika uwanja mkavu jaribu pia kuvaa viatu flat mara nyingi zaidi unapopata nafasi
Nitajaribu hii kitu
 
Jaribu mambo mawili. Kwanza cheki uzito wako, kama wewe ni obese au overweight ujue mifupa ya miguu inashindwa kubeba uzito wa mwili wako. So solution hapo ni kupunguza uzito. Pili aina ya viatu unavyovyaa.

Kama tatizo ni uzito mkubwa basi kwa muda huu unapopunguza uzito, tafuta aina ya viatu vyenye soli ya kubonyea upande wa kisiginoni. Usiavae sendoz kama zile za wamasai zenge soli isiyobonyea. Bora hata uvae yebo yebo zinasaidia.
 
Back
Top Bottom