Visa vya wasafiri ndani ya mabas. Hebu kama unacho kisa ulichokiona/sikia ndani ya dasii hebu jotdwn

Joack

Member
Jul 2, 2012
31
7
Nilikuwa nasafiri kutoka Msata - Pwani kuja Dar, Tulipofika Kongowe, alipanda jamaa mmoja akiwa ameongozana na mwanamke mmoja mrefu kiasi na unene kiasi. Walipokaa kwenye siti wakawa wanaendelea na stori zao na kuonyeshana mapenzi na kutufanya wengine tuvutiwe na kuanza kugeuza shingo zetu huku kama mimi nikisema moyoni mh! kuna wengine wamejaliwa kipawa cha kupendana kama ni mke wake basi wamependelewa ndoa si ndio hii. kwa ujumla walionyeshana mahaba ya hali ya juu.
Zilipopita dakika chache tu, simu ya yule dada ilianza kuita mara tukamsikia "nakuja niko njiani, nilipitia kwa fulani (alitaja jina la shemeji yake wa kike) nakuja. Walipomaliza tu maongezi na huyo mtu ambaye mimi nilihisi kuwa alikuwa ndio mume wake wa ndoa akampigia simu mdogo wake tulisikia hivi " Mambo? Za leo, Sasa Shemeji yako akikupigia simu kukuuliza kuhusu mimi, mwambie nilikuwa kwako na nimeondoka saa mbili usiku. Haya kwa heri" Basi wote ikabidi tunyamaze kimya naona hapo kila mtu alikuwa akiwaza lake. Walipofika eneo moja baada ya Kibaha Maili 1 kituo sikifahamu kwajina wakashuka sijui walikoelekea. Basi hicho ndio kisa tulichokishuhudia siku hiyo
 
hahahah nimepanda daladala leo kuja job knalijamaa linapiga makelele bas nzima linajifanya linafanya mipango ya kazi yaani nimekereka hadi mwisho.hal;afu siku moja pale kinondoni kuna mdada alimuaga mumewe anaenda kwa shangazi yake akalala siku 3 huko siku hiyo anaendelea nna swaga zake mara mumewe kapanda daladala siti ya nyuma na dada (mkewe)yuko mbele,kampigia simu mkewe akamuuliza ukowapi mkewe bila kujua akajibu nipo kwa dada we ule mwanamme akanyanyuka akaenda kumkwida kamwabia konda weka gari pembeni nimshushe huyu malaya mpaka anasema hayo teyari dada alikuwa anatoka damu uso mzima
 
Mizani- madukani- kwa komba?

malipo ya ukware hayo
 
Dah, mimi siku moja natoka huko kijijini Nzera - Geita, niko ndani ya basi akaja mama mmoja na watoto watatu ikabidi nimsaidie mtoto mmoja.
Kumbe yule mtoto alikua hajavaa hata ch*pi, c ndo akaachia kojo, nilioga kojo unaambiwa nikawa chapachapa.
Yaani mpaka leo naogopa kumsaidia mtu kwenye gari..
 
Ngoja nianze kupanda daladala sasa just for fun. Ila unaweza kutinga viwalo vyako vya hela ndefu ukishuka kwny daladala ukajikuta umechafuka siyo uchafu wa konda na hawa ndg zetu wamasai wachafuu siyo mate ya ugoro wao ptuu kila mahali ngoja nijaribu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom