Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mimi siku ya kwanza kupanda ndege nilikuwa nasafiri Dar kwenda Moshi,Mojawapo ya huduma zilizokuwepo ilikuwa mgao wa bia mojamoja kwa anayehitaji!Nikanywa kwa mapozi nilifikiri nipo kwenye bar! ghafla bia hata haijafika hata robo. Nikadikia tangazo "abiria wote fungeni mikanda ndege inatua"kumbe ilikuwa safari ya nusu saa -dk 45.Niliaibika.

hahhahah......poleee!
 
Mara yangu ya kwanza nilipata lift toka dar mpaka Unguja yani Kabla hata sijashangaa vizuri nikaona minazi minazi nikafikiri labda ni kasehemu tu tunatua kisha ndo tunaenda Zanzibar kumbe ndo tayari tumefika, ilikuwa ndege ndogo ya coastal travel safari ilitumia dakika 12
 
Ndege kitu ingine aisee, mimi kuna demu nimemkatia fastjet kwa 57,000 (one way) toka Mbeya anakuja tarehe 20/11/2015 nile mzigo ageuze tarehe 22/11 kuwahi usajili SAUT hapo nako nimekata 57,000 (Dar-MWZ)
 
mambo yamekwishaiva serikalini ndege mtazisikia kwenye bomba Ngosha ndo kashalianzisha kwa miaka 10 mtaishia kupanda MABASI kwenda TABORA MANISPAA au wilaya mpya ya NANYAMBA kusikiliza shida za wananchi
 
Ndege tutababia promosheni za FASTJET tu mengine ndo tusikilizie kwenye bomba. Aisee hii nchi ililiwa miaka 10 iliyopita
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...

ha ha ha ha....
 
TANGAZO: Kwa wafanyakazi wa Umma unapaswa kukaa mita 200 toka airport ilipo yaani in short usikaribie uwanja wa ndege. Hapa MABASI tu
 
Niko Primary dadangu akapata safari ya uingereza.(Kipindi hicho tunasema ulaya v haijalishi hata kama umeenda Marekani). Hakuna yeyote alowah kusafir na ndege kwetu mpk muda huo achilia mbali kwenda nje ya nchi tu. Bana weh,
1.Alishonesha suti kwa fundi kama ya sarafina pale wakati movie inaisha.
2. Tulikodi tax tatu kumsindkiza airport.
3. Mzee alituma nauli kwa shangazi na bibi wiki moja kabla ili watoke Mbeya kuja kumsindikiza dada airport.
4. Pale airport tukajipanga warefu nyuma, wafupi wachuchumae, tukapga picha. Ni moja kati ya picha dada hazipendi sana leo akikumbuka tulivokuwa washamba.

Hahaha aisee nimecheka sana
 
Hahahahaaaa Hihihihiiiii Huhuhuhuhuhuuuh atiii nini? Ndege hahaha nimecheka sn
Stak ata kukumbuka maana nusu nijikojolee.... Hahaaahaa 2010 mweeh
 
Hahahahaaaa Hihihihiiiii Huhuhuhuhuhuuuh atiii nini? Ndege hahaha nimecheka sn
Stak ata kukumbuka maana nusu nijikojolee.... Hahaaahaa 2010 mweeh

Aaaah, kuna jamaa yangu alitapika kipindi kile cha fly540
 
teh teh teh uwiiiii mbavu zangu mie mtoto wa marehemu!!!!

Mie nilikusanya vitambulisho vyote mpk vya drs la saba, birth certificate mpk death certificate za wazazi wng nikidhania ukifika kwenye mlango wa ndege unakaguliwa!!

Nikajisemea moyoni wakikataa hiki natoa hiki!!! mweeee ama kweli ushamba mzigo...

Duuh hii kali sana hii
 
Mie mbona sitasahau,,,,,,,,,,
cku iyo nilijipodoa kama naenda harusini kufika airport parfume yng ikawekwa kwny dustibini niliumia sana.............
nilipoingia ndani sijui ni uoga nikaita air host aje kunifunga mkanda kasheshe wkt wa kushuka mkanda ukanishinda kufungua ikabidi jirani yng kk mmoja anisaidie..

tinna cute pole sana. mimi perfume na dawa za mswaki zilitupwa kwenye waste bin ile kufika kwa jamaa wa uhamiaji wananiuliza vipi mkuu unaenda kufundisha KISWAHILI ughaibuni? sijui nnimekaa kama mwalimu. Mwishoni akamalizia kwa kuomba hela ya Chai UHAMIAJI AIRPORT punguzen njaaa.

Unaruhusiwa kuchukua perfume kwenye handbag lakini isizidi 100ml
 
Mara yangu ya kwanza 2007, ndege ilikuwa British airways, dar to London, siku hio linijamba hadi nataka kulia, hadi leo hii nasumbuka sana kwani tumbo langu hujaa gasi..
 
aisee mimi nimejaribu mara kadhaa kucheck-in kupitia zile AUTO TELLER MACHINE Za pale airport lakini zinazingua au zimewekwa pale mapambo tu

Labda kwa safari za ndani wanawabania, ila kwa safari za kimataifa hizo ndo zinatumika na hazizingui
 
Mm kiukweli Swissair ndo naizimikia haswaaa

Mi pia kwa sasa nataka nipande SwissAir hata kama sio kwenda Afrika japo tu nitoke nilipo kwenda nchi nyingine ila ndani ya Europe nipaone tu na hapo Zurich maana hawa jamaa nauli zao mhhh ni juu sana ukilinganisha na KLM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom