Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Asante Dark City, kwa vile ni kweli, niliendesha kipindi cha 'KitiMoto' na ni kweli kilisitishwa na ni kweli sikuwahi kusema kilichonifanya hadi nisitishe kipindi kile, hivyo pia inaweza kuwa ni kweli nitaendesha kipindi hiki, na ni kweli kinawezxa kusitishwa na ni kweli kabisa sitasema kwanini kimesitishwa.
Kwa wasio jua, walifikiri labda mimi ndiye ninaye rusha kipindi hewani, mimi ndie ninayemiliki hizo stesheni, na mimi ndiye ninaamua nirushe kipindi au nisirushe!. Kwa taarifa tuu, kazi yangu mimi ni kuandaa tuu kipindi na kupeleka kwenye vituo vya TV ambao wao ndio huamua ama warushe, ama wasirushe. Kwa waliosoma attachment nimeeleza majukumu yangu ni kuandaa tuu na sio kurusha. Ili kipindi kirushwe, lazima niwaombe, na watarusha wale tuu watakao kubali. Kunauwezekano wote wasikubali hivyo kipindi hakitarushwa. Watakapo kataa kukirusha, wanaweza kukueleza sababu kwa kwanini wamekataa, ama wanaweza kukataa tuu bila kukueleza sababu. Kiti Moto kilipokufa tulieleza sababu loud and clear, wenye TV zao walikataa kukirusha na hawakutuambia sababu. Hata hiki kipindi kipya kinaweza kurushwa na baadae kikakataliwa kurushwa bila mimi kuambiwa sababu!.Hivyo sababu yako ya kukataa kuniunga mkono kwa sababu hii ni valid!, na kwa sababu kila kipindi kikisimamishwa huwa watazamaji lazima muambiwe!. Funga macho kumbuka vipindi vingapi viliwahi kuwepo na viliposimamishwa kama uliambiwa sababu!.
Kama kuna sheria ya jf kuwa ukishajiunga, lazima upost mabandika kadhaa kwa interval ya siku kadhaa, na baada ya kipindi fulani kupita lazima angalau uwe umefikisha mabadiko kadhaa, hapo naikubali kuwa hii ni sababu valid, kwa nini usiniunge mkono, na pia mwana jf akiadimika, anawajibika kueleza alikuwa wapi, mbona tangu nimejiunga nimekuwa nikiposti from time time, labda mnisaidie na mimi hizo rules ili nizifuate nisije kukosa uungwaji mkono wa Dark City maana michango yako ndio muhimu kweli, ukikataa wewe tuu, baas, kipindi hakiwezekani bila michango yako!.
, kumbe issue ni kuanzisha mtandao wangu?, kusema kweli hili ndilo haswa lengo langu, yaani kuanzisha mtandao wangu, halafu niitumie michango ya watakaochangia mtandao wangu ndio nitumie mawazo yao kwenye hiyo programu yangu, kama utaweza kunisaidia kwa hilo nitakushukuru, hata kunianzishia page tuu kwenye fesibuku, watu watachangia na mimi nitawataja, si unajua tena nilivyo mtupu, hivyo mimi nikiwa mwenyewe, siwezi kutangaza kitu ndio maana nikatafuta humu jf, hivyo kama utanisaidia kuanzisha mtandao wangu, utakuwa umenisaidia sana, please help!.
Kwenye program one hiyo ya mgomo wa madaktari, nimeweka pale script, hata ukiipitia utaona wazi, bila michango ya jf, sitaweza kufanya hivyo program, nisaidieni jamani, niko chini ya miguu yenu!. Tena naombeni niwape siri, nafanya hivi vipindi ili nipate pesa, si nitalipwa na naninihii.. nisaidieni mwenzenu nisife njaa!.
Kusema kweli Dark City, nakuomba ukubali, yaani hata wana jf wengine wote wakikubali na wewe ukataa, then siwezi kutengeneza program bila wewe maana maoni yako ndio yananiletea pesa nyingi!. Ila pia nitauheshimu msimamo wako!.
I wish I had all the powers to say NO...na ikawa hivyo hivyo!
Maoni yangu na msimamo wangu nimeweka wazi...Hata kama wengine watakubali na kukupa ruhusa ya kutumia mabandiko yao....ni sawa tu. Ila mabandiko yangu hapana...Iwe unatengeneza pesa au unatoa offer!
Kwani sina haki ya kukatalia maoni yako??
DC!!