vipigo CCM! Jamani vipi?

Hii nayo kali ama kweli madaraka ni matamu!mtu waziri bado unataka tena uenyekiti!si ungeridhika tu na nafasi ya uaziri ili ufanye kazi zako kwa ufanisi!sasa UWT nako anataka!

FL, Mafisadi na uroho wao hawajali kujirundikia vyeo chungu nzima hata kama kazi za hivyo walivyo navyo zinawashinda. Mjumbe wa NEC, Mjumbe wa CC, Waziri wa utetezi wa mafisadi, Mbunge wa kuteuliwa, n.k. n.k. Mafisadi hawatosheki!!!
 
.....Ndio laana za Nyerere nini hizo??? Watu kushindwa kuheshimu taratibu za kupata uongozi kwa hiyo kilichobaki ni ubabe tu...na bado watavuana mpaka nguo hadharani hao kwa kupenda vyeo!!!!!!!!!! Ndio matatizo ya kufanya siasa ni ajira....
 
Ikiwa Mwalimu wa kiume harafu darasani kwake kuna msichana ambaye anaweza piga kwezi wanafunzi wenzake mbele yake na hata adhabu ya mwalimu huyo haimtishi basi kwa asilimia 99% mwalimu huyo ana mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo.

Simba Vs Kikwete kunani?? Ni mahusiano gani wanayo zaidi??

Wenda Rais mbovu kuliko wote Duniani akawa JK.
 
Halafu sofia mimi sioni hata sifa zilizomfanya akateuliwa kuwa waziri wa wizara nyeti kiasi hicho!sasa yeye anaonyesha mfano gani?yaani ukiona kama vile hutendewi haki wewe rusha ngumi na maneno!kma yeye alivyodai kutoshirikishwa kwenye vikao vya UWT mkoa!basi akajichukulia maamuzi mkononi!
 
Ikiwa Mwalimu wa kiume harafu darasani kwake kuna msichana ambaye anaweza piga kwezi wanafunzi wenzake mbele yake na hata adhabu ya mwalimu huyo haimtishi basi kwa asilimia 99% mwalimu huyo ana mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo.

Simba Vs Kikwete kunani?? Ni mahusiano gani wanayo zaidi??

Wenda Rais mbovu kuliko wote Duniani akawa JK.

Mkuu hayo uliyoyasema yamezungumzwa sana kwenye Corridors za Ofisi za serikali..Inawezekana kwamba kuna ukweli,Huyu Mama amekuwa na sauti kubwa,na ana uwezo na ushawishi mkubwa kwa JK.Mwanzo ilifikiriwa kwa sababu ya Wizara anayoshika (Usalama wa Taifa),lakini sasa nafikiri kuna kubwa zaidi ya hilo..kulikuwa kuna maneno yasiyokuwa ya kawaida kipindi ambacho Mama Simba alikuwa Mgonjwa,kwa sababu Muungwana alifanya ziara nyingi kumjulia hali Hospitalini.Kabla na baada ya kurudi kutoka Afrika kusini.Hali ambayo si ya kawaida sana kwa Mkuu wa nchi.

Ugomvi huu na Mama Kahama utakuwa mkubwa mno.Mama Kahama ni Dada Mkubwa mno na labda pengine ni Mama kwa Sophia.Kama ni kweli kwamba alidiriki kumtupia ngumi ni jambo la aibu na lisilo la kiistarabu kwa watu wazima.Jakaya atakuwa na wakati mgumu kuamua kesi hii,Sasa amekuwa Judge wa kuamua ugomvi kwa ajili tu ya uchu wa baadhi ya wana-CCM kutafuta madaraka.Inasikitisha,kwani Chama kimejaa uhuni na Utoto wa Mjini,kila mtu ni Bingwa kuliko mwingine.Kuna ugomvi wa Nape na Nchimbi,leo tunaona Kahama na Simba na kesho Capt.Komba atamshitaki Makamba kwa kumtuhumu ni mwizi.Hii CCM inaporomoka taratibu.
 
..capt komba ..will fight back ..kwa sababu yeye alipiga kampeni kwa kuimba...pesa akalamba ..lakini na yeye anajuwa kuwa kina makamba ,kikwete na mtandao wao waliiba pesa nyingi ya hizo kwa ajili ya kampeni na wakala hakuna wa kumfunga paka kengele..

sophia simba anawakilisha mtandao wa kikwete ..na wana malengo ya kujiimarisha ili kuwazuia wanaotaka kumpinga jk 2010....

mama janet..anaungwa mkono na viongozi wastaafu wa ccm,na wana ccm wote wasiokuwa mtandao[ie sumaye,warioba,salim,msuya,malecela,salim,mwandosya..] ambao idadi yao inaendelea kuongezeka..uwezekano wa wajumbe kupiga kura za chuki kwa wagombea chaguo la kikwete ni mkubwa..na hii itadhibitisha kama bado kikwete anadhibiti chama au la....
 
Kwanini JK hakumwambia agombee ccm WAZAZI?
EPA AND MORE EPA...Kuna vigogo wanaojuwa wazi kuwa kama wakipoteza madaraka ndani ya chama kina Nape wanawanyemelea na hapo shughuli ipo.
Upinzani nao wawagawanye ccm kama ccm inavyowagawanya.
 
Kwanini JK hakumwambia agombee ccm WAZAZI?
EPA AND MORE EPA...Kuna vigogo wanaojuwa wazi kuwa kama wakipoteza madaraka ndani ya chama kina Nape wanawanyemelea na hapo shughuli ipo.
Upinzani nao wawagawanye ccm kama ccm inavyowagawanya.

..jk ni mtu wa visasi sana..huko jumuiya ya wazazi mbona akishawafukuza tu mara baada ya kuingia mwaka 2005....kama mnamkumbuka A.MAREGESI.....huyu ni yule mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ambaye mwaka 2004..alitamka hadharani akiwa ziarani kilimanjaro ..kuwa haoni mtu anayefaa kwa nafasi ya urais zaidi ya sumaye.....

baada tu ya kikwete kuingia ..aliundiwa zengwe tena akasimamishwa na uwanachama kwa tuhuma za ubadhirifu..na siku hizi hata hasikiki.....huyu hakupewa nafasi...na nafasi ya mwenyekiti wa wazaazi mtandao ...waanataka kumpa ZUNGU..,,,NIMROD MKONO ...pia anaitaka ..lakini sidhani kama ana baraka za mtandao...au yupo matumaini...

mtu..mwingine aliyeamua kustaafu haraka...[pamoja na kuwa muda ulikuwa unakaribia]..ni stephen mashishanga...ambaye wakati wa ugombea 2005...alimpokea sumaye na kumuadress kama rais mtarajiwa...na siku kikwete alipopita morogoro akamkaukia.......huyu alipoingia tu jk...alipeleka barua ya kuomba kustaafu mapema ........

kuna watu kama kina nagu ...na wengine waliachwa [kimkakati]....lakini inaonekeana bado makundi yanaitafuna nchi.....
 
Inaonyesha kuwa very powerful kwenye system dalili zake ni ruksa kuwavurumishia wapinzani masumbwi popote unapowakuta, bila kujali kuwa nao wamechaguliwa kushika nafasi walizonazo! What a system we have got! Is this the real power?!?
 
Huyu Mhe. Sofia Simba mlimtetea sana alipomjia Juu Wazir Mwenzake Ghasia ktk Public ktk Masuala ya Mavazi...Leo mnakubali kuwa Huyu Mheshimiwa Hamna kitu kichwani...

Kama Ilivyoripotiwa itakuwa Ndivyo...Basi huyu Mwanamama inabidi ajiuzulu nafasi yake....otherwise JK mfukuze kwani hawakilishi the so called UTAWALA BORA...

Mwenye Faili la ELIMU yake naomba...maana ninawaswas na elimu yake...
 
Hivi waziri atapata wapi muda hata wa kuongoza jumuia ya Wanawake? Siku hizi watu ni kujilundikia vyeo tu hata kama hawana uwezo au muda wa kutimiza hayo majukumu.

Mtu anakuwa mbunge, waziri, mjumbe wa NEC, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake nk. kweli wana muda wa kutimiza majukumu yote hayo?

Ndio maana hakuna kinachofanyika.

Halafu kweli mtu mpaka amekuwa waziri, bado mpaka agombane kwasababu ya nafasi?

Hiyo ndio GREEDY na hii imetawala sana CCM watu wana vyeo kumi kidogo na ukiangalia how effective & efficient they are; is may be 2% or less, why don't we let other people work for the better of our country? jamani tutaishia wapi na ulafi huu? ni aibu hata wanawake wamekuwa majasusi tu hakuna penye afadhali, phuuuuuuuuu
Shame on you Sophia Simba.
 
Hiyo ndio GREEDY na hii imetawala sana CCM watu wana vyeo kumi kidogo na ukiangalia how effective & efficient they are; is may be 2% or less, why don't we let other people work for the better of our country? jamani tutaishia wapi na ulafi huu? ni aibu hata wanawake wamekuwa majasusi tu hakuna penye afadhali, phuuuuuuuuu
Shame on you Sophia Simba.


Hali itabadilika maana wanaozitaka hizo nafasi ni wengi. System yao hii ya kupeana haiwezi kukidhi tena - tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma kipindi ambacho wahitimu walikuwa wachache ambapo sisiemu na serikali yake viliwameza wote.

Kadiri muda unavyokwenda ndivyo kazi ya akina Dr. Slaa itakavyokuwa ikipungua ugumu.



.
 
Back
Top Bottom