vipigo CCM! Jamani vipi?

Wajumbe wengi walitabiri hapa jf kuwa hawa ccm wanaelekea kubaya iko siku watarushiana masumbwi...hata mwezi haujapita haya yanatokea.

Cha kushangaza sophia simba ni waziri wa nchi, ofisi ya raisi (utawala bora), sasa sijui hapo kikaoni ndio alikuwa anaonyesha mfano wa utawala bora.??
 
Mkuu muogope Mungu kidogo, Mama Janeti umri alionao kweli anaweza kugombea wanaume?

Wakati mwingine tuwe na heshima kidogo na viongozi wetu wa taifa na hasa watu wazima kama huyu mama.

Angekuwa na heshima asingetukanana na kupigana hadharani...
 
"Habari hizo zinaendelea kueleza kuwa baada ya Zungu kuondoka katika kikao, Waziri Simba alielekea alipokuwa ameketi Kahama lakini wajumbe waliwatenganisha ili kuepusha mzozo zaidi. "

KWANGU NAONA KUNA LILILOPO NYUMA YA HILI TUNALOLIONA.
JE,UWT IMETOA TAMKO JUU YA HILI.

MWENYE INFO ATUPATIE TUJIELIMISHE.....
 
fOOD FOR THOUGHT
..kwavile unaeshima Ukipigwa UNAPASWA KUFANYA NINI?
SELF DEFENCE MANAKE NINI WAUNGWANA?
"Habari hizo zinasema kuwa Zungu alipoona Simba amefuatwa kwenye kiti chake na kusimama mbele yake, aliamua kutoka haraka haraka na kuacha kikao."

I COULD EXPECTED MAMA KAHAMA 2 DO THE SAME.
 
Hivi waziri atapata wapi muda hata wa kuongoza jumuia ya Wanawake? Siku hizi watu ni kujilundikia vyeo tu hata kama hawana uwezo au muda wa kutimiza hayo majukumu.

Mtu anakuwa mbunge, waziri, mjumbe wa NEC, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake nk. kweli wana muda wa kutimiza majukumu yote hayo?

Ndio maana hakuna kinachofanyika.

Halafu kweli mtu mpaka amekuwa waziri, bado mpaka agombane kwasababu ya nafasi?
 
Hivi waziri atapata wapi muda hata wa kuongoza jumuia ya Wanawake? Siku hizi watu ni kujilundikia vyeo tu hata kama hawana uwezo au muda wa kutimiza hayo majukumu.

Mtu anakuwa mbunge, waziri, mjumbe wa NEC, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake nk. kweli wana muda wa kutimiza majukumu yote hayo?
Ndio maana hakuna kinachofanyika.

Labda hii ndio multi-tasking yenyewe!
 
Jamani ndani ya hiyo UWT kuna majungu ya kufa mtu. Hawa wamama msiwaone wamezeeka hivyo, wana matatizo hawa, kweli vyeo hivi vinawafanya wawe kama wendawazimu.
 
blank.gif
blank.gif

Janeth Kahama: Sophia Simba alinirushia makonde

2008-09-16 11:46:43
Na Simon Mhina

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Kahama, amedai kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alimrushia makonde kwenye kikao cha Kamati ya Siasa na kwamba haukuwa ugomvi mdogo wa maneno kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari jana.

Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kutokana na kitendo hicho, amemshitaki Waziri Sophia Simba kwa Rais Kikwete pamoja na kwenye vikao vya Chama.

Akizungumza na Nipashe jana, Janeth alisema mbali na Sophia kumtamkia maneno makali yasiyo na idadi, alidiriki kumkunja na kumrushia makonde kadhaa kabla hajakamatwa na watu.

``Alitaka kunidhuru, nilikuwa katika wakati mgumu, maana hata wanaume na nguvu zao walipomshika asije kuniumiza, bado aliwasukumiza,`` alisema mwenyekiti huyo, ambaye anatarajia kuchuana na Waziri Simba katika kinyang\'anyiro cha uenyekiti wa Taifa wa UWT katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba.

Alipoulizwa kama anawakumbuka wajumbe waliomuokoa katika sakata hilo ni kina nani, Jeneth alisema haikuwa rahisi kuwakumbuka kwani kuna wakati aliserereka na kabla hajaanguka, hajui nani alimdaka.

``Katika hali hiyo huwezi kukumbuka jina wala sura ya mtu, nilichokumbuka mimi ni msalaba,`` alisema.

Alisema baada ya kuona mwenzake (Sophia) amezidi kuwaka hasira huku hali ikizidi kuwa mbaya ukumbini, alichokumbuka ni kukimbilia msalabani na kufanya maombi na kukemea roho ya ugomvi.

Alisema anamsgukuru Mungu, kwani hadi sasa anayo amani ya kutosha na kwamba hana kinyongo na mtu yoyote. ``Nampenda sana Sophia, sina kinyongo naye,`` alisema.

Hata hivyo alisema amekusudia kumfikisha mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na kwenye vikao vya Chama.

``Siwezi kumlaumu wala kusema barabarani kama alivyosema, mimi nitamfikisha kwenye vikao vya maadili, ndivyo taratibu zetu zinavyosema,`` alisema.

``CCM hakuna jela, kwamba nikimpeleka huko atafungwa, lengo nikuhakikisha anapata nafasi ya kutoa madai yake,`` alisema. Hata hivyo, alikana kumhujumu Sophia kwa kutomwalika kwenye vikao vya UWT kama ilivyodaiwa.

Kwa upande wake, Waziri Sophia alililiambia Nipashe jana kuwa haogopi. ``Kama anakwenda kushitaki anayo haki ya kufanya hivyo, akashitaki tu,`` alisema.

Hata hivyo, Sophia alisema na yeye anayo malalamiko dhidi ya Janeth na atayafikisha kwenye Chama. ``Namimi pia nina malalamiko kwake, mengi sana tena mazito, hata mimi nitamshitaki,`` alisema.

  • SOURCE: Nipashe
blank.gif













blank.gif

blank.gif
ippmediadotcom_gr.gif
blank.gif
blank.gif
 
Huyu sophia simba si ndiye waziri wa usalama wa taifa? (I mean usalama wa taifa uko chini ya wizara ya utawala bora).

Ni waziri wa utawala bora au bora utawala?

Huko CCM ndani inaonekana hapatoshi. Mungu inusuru nchi hii.
 
Hivi waziri atapata wapi muda hata wa kuongoza jumuia ya Wanawake? Siku hizi watu ni kujilundikia vyeo tu hata kama hawana uwezo au muda wa kutimiza hayo majukumu.

Mtu anakuwa
1. mbunge,
2. waziri,
3. mjumbe wa NEC,
4. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
5. nk.
kweli wana muda wa kutimiza majukumu yote hayo?

Ndio maana hakuna kinachofanyika.

Halafu kweli mtu mpaka amekuwa waziri, bado mpaka agombane kwasababu ya nafasi?


Speaking of "sera za sisiemu".



.
 
First kawa mbogo, sasa unawatetea wanawake au ukweli, ndio mambo ya equql opp. tutaimbiwa mpaka taarabu kwenye vikao
 
Sophia Simba ni mbunge wa kuteuliwa na Janet Kahama ni mbunge viti maalum. Probability ya wao kuchuguliwa tena kuwa wabunge 2010 ni ndogo. Mwenyekiti wa UWT anaingia bungeni. Ugomvi wote huu ni kujihakikishia ubunge 2010. Hauna haja tena ya kufanya kampeni. Strategic Planning at work!!!
 
Mwaka huu JK ana mitihani mingi sana. Lakini yote haya aliyataka kwa kuwa alikubali sera za makundi ndani ya CCM wakati akiwa kwenye harakati za kutaka kuingia Ikulu.

Mama Kahama sidhani kama ni mwanamtandao. Mama Simba ana dalili zote za uwana mtandao na si ajabu kweli ametumwa na wanamtandao na wanatumia jina la JK ili kupunguza makali ya wapinzani kwenye huo uchaguzi.

Kabla JK hajamaliza sakata la Nape, tayari kuna sakata la Mama Simba.

Kitendo cha Mama Simba kupigana kwenye kikao ni sababu tosha ya yeye kujiuzulu kwa kuwa ameonyesha mfano mbaya wa utawala bora. Kila siku wanatuhubiria kwamba tusichukue sheria mkononi, yeye naona ya kwake ilikuwa kiganjani na ndiyo maana akaamua kutoa hukumu yake pale pale! Hizi ndiyo siasa za zama za JK na mtandao wake!
 
Sophia Simba ni mbunge wa kuteuliwa na Janet Kahama ni mbunge viti maalum. Probability ya wao kuchuguliwa tena kuwa wabunge 2010 ni ndogo. Mwenyekiti wa UWT anaingia bungeni. Ugomvi wote huu ni kujihakikishia ubunge 2010. Hauna haja tena ya kufanya kampeni. Strategic Planning at work!!!

Nakubaliana na wewe Heri kwa asilimia miamoja hawa wanagombea kuingia huko bungeni na NEC bwelele mwaka 2010 bila ya kupigiwa kura kama anavyofanya yule mama fisadi Anna Abdalah ambaye muda wake unaisha
 
Back
Top Bottom