Wadau, kuna tangazo hapa jamiiforums linasema: "Buy for only 30,000 Tsh and get free internet for 6 months. Visit any airtel shop." Naona hili tangazo linasema uongo maana jana nilinunua modem kwa 30,000/-, nikalipia bundle ya wiki moja lakini sikupata hiyo "free internet". Badala yake hela nilizolipia kwa bundle ya wiki moja 2,500/- ziliisha muda mchache baada ya kuweka. Sasa hiyo "free internet" kwa miezi sita iko wapi? Je, hawa njemba wanatudanganya ili watulie hela? Pia kuna offer ya Vodacom Tsh 7500 kwa 500MB. Je, waliokwishatumia mnashauri nini hapa? Nihamie Vodacom?