Shairi: Vipi nijikwamue

Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,848
58
Nawauliza malenga, wa bara na visiwani,
Kwa tungo mnazotunga, majibu nipatieni,
Mwenzenu ninatanga, moyo wangu pepeeni,
Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.

Nanasa nikijiona, niokoe nisizame,
Naogopa hiki kina, cha ulimbo nikiseme,
Nakihisi ni kirefu, msitake nijipime,
Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.

Ulimbo wanivutia, unang'ara rangi yake,
Jasmini wanukia, si haba harufu yake,
Zeze unanipigia, napenda sauti yake,
Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.

Nikipima kwa mizani, niko fifti fifti
Wajuzi jibu nipeni, ulimbo wajizatiti
Ulimbo kwangu mwilini, nitoeje watafiti
Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.
 
Back
Top Bottom