vipi naweza kuachana na mpenzi bila lawama?

Msenyele

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
338
86
Nina mpenzi wangu mmoja ambaye nimekaa naye takribani miaka miwili. Mpenzi huyu pamoja na kukaa naye muda ule, ukweli ni kwamba simpendi na yeye ni king'ang'anizi kiasi kwamba nashindwa kupumua. Nitumie njia zipi ili tuachane bila lawama? Nisaidieni jamani.
 
Hapo penye nyekundu, umewezaje kukaa na mtu usiyempenda kwa muda wote huo wa miaka 2? Kwa nini nisiamini kuwa ulimtumia kukutimizia haji zako binafsi? Kama ndivyo, hujui kuwa umempotezea muda ambao pengine angeutumia kutafuta mtu mwingine?

Anyway, kwa kuwa imetokea, mtafute muongeee naye, na umwambie ukimaanisha kuwa umeamua kutokuwa naye kabisa. Muombe msamaha kwa muda uliokuwa naye ili asiendekee kuinvest moyo wake sehemu ambayo hata pata faida yeyote!
 
Nina mpenzi wangu mmoja ambaye nimekaa naye takribani miaka miwili. Mpenzi huyu pamoja na kukaa naye muda ule, ukweli ni kwamba simpendi na yeye ni king'ang'anizi kiasi kwamba nashindwa kupumua. Nitumie njia zipi ili tuachane bila lawama? Nisaidieni jamani.

je,unawezaje kuishi miaka miwili na mtu usiye mpenda!acha ulimbukeni utakuja juta....onyesha heshima kwa kuthamini hisia zake lkn maamuzi nijuu yako fanya uwezavyo Ila mungu huwa pamoja na wanaonyanyasika bila hatia!
 
u need psychology help ma friend! how can u spend 2 years with some one u don lov? jichunguze wewe kabla ya kuomba ushauri! kaa miaka miwili ndio umwambie humpendi.
 
Kuachana inawezekana tena bila nguvu nyingi kuhitajika

ila kwa miaka miwili kukaa na mtu usiempenda ni jambo la ajabu sana

ongea na huyo mwenzi wako na uliweke wazi hilo uone mtazamo wake

kama uliweka mbeli masilahi yako , ipo gharama utailipa
 
Bila shaka wewe ni kirukanjia. ulikuwa unamhadaa unampenda kumbe wapi. sasa unaweza kuachana naye lakini kwa mtazamo wangu, sioni namna unavyoweza kukwepa lawama kutoka kwake.
 
Kijana,kua muungwana japo kwenye kauli Kama sio muungwana kwenye akili, ivi ingenue huyo mdada anasema hayo unayosema wewe ungefurahi? Miaka miwili ulokaanae ulikua unamchukuliaje,na vp una fanya mapenzi na mtu usompenda? Mie naona wewe hata nafsi yako huipendi....
 
inawezekana.....ila ungesema.....mapenzi yamepungua juzi juzi....huwezi kuwa umekaa nae miaka 2 leo useme hukumpenda.....huwa haipo hii....
 
King'ang'anizi, si sababu tunaona ving'ang'anizi wangapi wanapigwa chini. Utakuwa umemtumia au ndo kafulia jamaa
 
Nina mpenzi wangu mmoja ambaye nimekaa naye takribani miaka miwili. Mpenzi huyu pamoja na kukaa naye muda ule, ukweli ni kwamba simpendi na yeye ni king'ang'anizi kiasi kwamba nashindwa kupumua. Nitumie njia zipi ili tuachane bila lawama? Nisaidieni jamani.
Wewe inaonyesha mpenzi mmoja hakufai, lazima uwe nao wengi.
 
Najitahidi kufikiri 1year=365 days :- 2 yers=730 days. Unaamaanisha siku 730 au unatania ?
 
Unatafuta laana ww, yaan umchakachue miaka yote hiyo, halafu umwambie humpendi, imagine ungekuwa ww mwenyewe ungefanyaje unataka kuambiwa hivo?
 
Back
Top Bottom