Vipi nafasi ya mwenyekiti UVCCM ?

Godwin Mneng'ene

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
215
83
Baada ya kujiuzulu Masauni kwenye nafasi ya uenyekiti wa UVCCM taifa nafasi yake imekaimiwa kwa muda mrefu bila kujazwa pamoja na wagombea mbalimbali kujitokeza kuonyesha nia ya kuitaka hiyo nafasi. Sasa hivi naona vijana kibao wamejitokeza kutaka kugombea nafasi ya makamu Mwenyekiti UVCCM taifa. Lakini nafasi ya mwenyekiti imekuwa kimya.

Kwa wadau wa ccm naomba inijuze hii imekaavipi na kwa nini tokea masauni ajiuzulu hajachaguliwa mwingine na kwa sasa mbona vijana wengi wanajitokeza kugombea umakamu na sio uenyekiti? au muda wa kugombea uenyekiti bado. Jamaani naombeni kujulishwa nipate kuelewa haya mambo. Ni mimi Mdau wa Siasa za Tanzania nisiyekuwa na chama.

Natanguliza shukrani kwa kujulishwa vizuri na kwa ufasaha
 
mi nawahurumia sana vijana wenzang wanaokosea njia kuingia kwenye hiki chama, kilishapoteza dira zamani sana. kinafundisha vijana kuwa wataalamu wa sarakasi za rushwa kwenye uchaguzi, kinawafundisha vijana kuwa waongo kudanganya watu, kinawafundisha vijana kuwa wataalamu wa kutukana MATUSI hadharani bila aibu (rejea scene ya Lusinde kule Arumeru Mashariki kwenye kampeni), kinawafundisha vijana wizi wa rasilimali za taifa na kuzificha kule uswisi na ulaya, kinawafundisha vijana kujilimbikizia mali, kinawadumaza vijana kifikra kwani ndani ya hiki chama hakuna kukosoana tena, ni kukubali tu bora upewe nafasi ya kuchukua chako mapema, yaani hiki chama kilishapoteza uelekeo kabisa, yaliyoandikwa kwenye katiba yake hayafuatwi tena. hakuna kuwajibishana tena ni kulindana tu kwa kwenda mbele. hakuna uzalendo tena kwa nchi, ni kuwa mzalendo kwa chama. aaaaaarrrrrrrrrgggggggggg!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom