Vipaumbele vya bajeti vya kambi rasmi ya upinzani mwaka wa fedha 2012/2013.

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
***VIPAUMBELE KATIKA BAJETI YA
KAMBI YA UPINZANIA Katika Bajeti
Mbadala ya 2012/2013***
1. Kuendelea kushinikiza
kupunguzwa kwa misamaha ya
kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa.
Hivi sasa
misamaha ya kodi ni sawa na
misaada yote kutoka nchi
wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni
sawa na 3% ya
Pato la Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha
kwenye maendeleo vijijini hasa
kujenga miundombinu kama
barabara za
vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha
kukarabati Reli ya Kati na kufufua
njia za Reli za Tanga, Moshi na
Arusha.
4. Kuongeza wigo wa kutoza tozo
la ujuzi (Skills Development Levy)
ambapo sasa waajiri wote
walipe ikiwemo Serikali na
mashirika ya umma. Pia
kupunguza tozo hili mpaka 4%
ambapo 1/3
itaenda VETA na vyuo vya Ufundi
na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili
kukabili changamoto ya
mikopo kwa wanafunzi.
5. Kushusha kima cha chini cha
kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9%
ili kuwezesha wananchi wa hali
ya chini kubaki na fedha za
kutumia na kukuza uchumi.
6. Kuongeza mapato ya ndani na
kupunguza mikopo ya kibiashara
kwa kuhakikisha mapato ya ndani
yanafikia 20% ya pato la taifa,
kuongeza nguvu za kisheria na
udhibiti ili TRA ikusanye mapato
zaidi
kwenye kampuni za simu na
kwenye shughuli za uchimbaji wa
madini, mafuta na gesi.
7. Kutayarisha Taifa kuwa na
uchumi wa Gesi.
8. Kupunguza /kufuta kodi
kwenye bidhaaa za vyakula kwa
muda maalum ili kushusha
mfumuko wa
bei.
9. Kuweka mfumo mpya wa elimu
kwa kushirikisha sekta binafsi
katika kutoa elimu kwa ubora
zaidi,
ikiwemo kuundwa kwa chombo
cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory
authority)
10. Kutoa vipaumbele na unafuu
vya kikodi kwa viwanda vya ndani
vinavyotumia malighafi za nchni
hasa za kilimo na zenye kuongeza
ajira kama Korosho,Pamba na
Mkonge.
 
Back
Top Bottom