VIP Prisons coming soon in TAnzania

Kwa ufupi ni kuwa jamaa wametoa hizo fedha wajengewe/karabatiwe sehemu watazoishi kwa miaka michache, kisha wanakata rufaa na kutolewa.

Ngoja nitafute njia nami niibe Visenti nikafungwe "nyumbani"
 
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani Lawrence Masha akihojiwa na TBC1 amesema kuwa kinachojengwa Ukonga ni "interview area".Akifafanua amesema kuwa itakuwa ni sehemu ambapo wafungwa watakuwa wakikutana na kuongea na ndg zao,ambapo amesema kuwa kwa sasa wafungwa hao wanakutana/wanaongea na ndg zao wanaofka kuwatembelea "kienyeji".Pia ameeleza kwamba hii ni katila uboreshaji wa hali za magereza ya hapa nchini.
 
Mheshimiwa nipe jibu,
Gereza la Tunduru nalo litafanyiwa hivyo hivyo?
 
Sasa hapa tunaanza kukubali waziwazi kuwa we are not equal under the law. Kama mhalifu anyeiba kuku anafunngwa kwenye mazingira mabaya, na kama mwizi mkubwa anafungwa kwenye mazingira mazuri, au kwa maana nyingine mhalifu mkubwa anatumikia adhabu kwa raha na mhalifu mdogo anatumikia adhabu kwa mateso, kila mtu atachagua kufanya uhalifu mkubwa. God bless Tanzania.
 
God forbid tusifike huko!
 
Letz hope so mkuu,kwamba wameanzia dsm(Ukonga?) then wataendelea na sehem nyingne za nchi hii.Lakini cha kustaajabisha,nimeona kwenye taarifa huo ukarabati,ni pamoja na vitanda(kama vya banko vle) na kuta naona zmeng'aa!!Sasa cjui mh. Alisahau kueleza pia kuwa kuna sehemu nyingne pia znakarabatiwa sambamba na huo ukarabati wa hyo interview area au huko kunakokarabatiwa nako ni extension ya hyo sehemu ya kuongea na wafungwa.
 
kuna gereza lipo morogoro kwa ajili ya vigogo kati kati ya moro na chalinze..huko ndipo yule katibu mkuu wa wizara ya ujenzi alifungwa kwa rushwa kabla ya kuachiwa mwaka juzi...hilo gereza alijenga mwalimu ...ili kuwaweka maafisa au viongozi wanaokosa..akiamni kuwa kuwachanganya na wengine kunaweza kuhatarisha usalama wao..ie hakimu,,afisa wa polisi ,jeshi ets......hiyo jela ya morogoro angalau wanalala vitandani....wanapewa magazeti..,hakuna msongamano..ets..pia mchana hufanya kazi ndogo ndogo kwenye bustani ya mboga.......nafikiri mafisadi watapelekwa huko..na wala sio magereza ya wakorofi kama .....dodoma,karanga,mwanza,ukonga..ets

mahabusu mastafu kama kina mtikila,zombe ,dito ets pia ukienda ukonga au keko wana sehemu maalumu..wanakaa chumba vya peke yao..wanaogopa wasidhuriwe na mahabusu wakorofi......kazi kwa tusiokuwa na status uraiani....ina maana ukishindwa kuwa kiongozi ..basi angalau kuwa fisadi ..ili bahati mbaya ukiingia jela..usiolewe!!!
 
Baada ya watuhumiwa wa EPA kukosa dhamana na kwenda rumande, nani anaweza kutuhabarisha wako wapi? Isije ikawa wako VIP prisons/remands!
 
Hivi kuna wezi ambao wana haki kuliko wezi wengine? Kwa nini hao watengenezewe mazingira mazuri huku wengine wakiwa kwenye mazingira mabaya. hata kama ni kweli watakamatwa na kuwekwa ndani, naanza kupata hisia kuwa kukamatwa kwao itakuwa ni sehemu ya mchezo wa kuigiza kuhusiana na vita hii dhidi ya ufisadi

Ndiyo kuna wenye haki zaidi na wengine hawana haki. Mifano iko wazi.
Mlala hoi wa kawaida kabisa anaposhtakiwa polisi kwa kosa lolote hata kama polisi wanaelewa hivyo(Nasema wanaelewa hivyo kwa sababu mtu asemaye uongo utamjua tu), polisi bila hata kufanya upelelezi watamuuliza mlalamikaji, Una usafiri, unafikiri saa hii atakuwa wapi,,hao wanakukamata, bila hata kuambiwa kuwa unakamatiwa nini. Unaishia rumande hadi siku ya pili,,, biashara inaanzia hapo. Lakini kwa mkubwa eti anachunguzwa kwanza, na akisha chunguzwa anaenda kupewa taarifa polisi mkubwa sio hawa wadogo wadogo sijui sgt! Na anawaambia nitakuja baadae kidogo nina kazi namalizia. Anafanya appointment na Afisa wa polisi as if yuko juu ya sheria. Hii ndiyo nchi yetu ya wasomi wachache wenye hela wanaojua haki zao,,,, sisi wengine hata haki zetu tunabahatisha. Tunaishia kuwekwa mbuzi wa kafara.

EE Mungu tubariki sisi waja wako, utupe neema na rehema ya haki zetu, utuepushe daima na mafisadi wa nchi, ili tuamke na kuitumikia nchi hii kadiri ya mapenzi ya wananchi wenye mapenzi mema,,, AMEN
 
Hivi hakuna watu wamewatembelea hawa jamaa kule Ukonga wakaona kama wanakaa kwenye zile cell walizofanya renovation? Nani yuko updated atuambie?
 
Hivi kuna wezi ambao wana haki kuliko wezi wengine? Kwa nini hao watengenezewe mazingira mazuri huku wengine wakiwa kwenye mazingira mabaya. hata kama ni kweli watakamatwa na kuwekwa ndani, naanza kupata hisia kuwa kukamatwa kwao itakuwa ni sehemu ya mchezo wa kuigiza kuhusiana na vita hii dhidi ya ufisadi

Nimependa sana swali lako na jinsi usivyoamini kwamba kuna "categories" za wafungwa. Ukweli ni kwamba katika nchi yetu kuna tabaka la wafungwa. Kuna wewe na mimi ambao tukikamatwa kwa wizi wa Tsh 10,000 tunawekwa mahabusu for years without being prosecuted. Na verdict ikitolewa ni kifungo cha 35 years. Sasa hapo unajiuliza kwamba, kuna usawa wowote kati ya gharama za kumhudumia mfungwa for 35years kwa wizi wa Tsh 10,000 au kwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi?

Then kuna kundi lingine la wenye nazo ambao wao kukamatwa kwao ni mpaka tume ziundwe. Tena wapewe nafasi ya kukiri makosa yao kwanza bila prosecution. Then wakikamatwa, masharti ya dhamana huwa ni marahisi sana, maana hawa wanacash tayari. Then prosecution yao huwa ni fasta fasta na verdict huwa kama utani vile. Kama hiyo haitoshi, msamaha wa raisi ukija wanatolewa.

Upo hapo?
 
Jibu ni kuwa ukiwa mhalifu mdogo adhabu yako ni kubwa na ukiwa mhalfu mkubwa adhabu yako ni ndogo. This is life ndugu yangu get used to it. Kama unanja ukiiba soda unaweza kupigwa hadi ufe, lakini ukituibiwa wananchi mabilioni au ukiwa mkuu fulani ukiua mlala hoi tutakupa ulinzi. Inaonekana kama ni utani, lakini ukiangalia hali halisi utaona hivyo.
 
Hivi kuna uwezekano wa serikali kubinafsisha magereza ili wazawa tujikusanye tujenge yetu ambayo wataingia MAFISADI na kupata adhabu kali yenye mateso hata kama ni mahabusu....bila kusahau viongozi wala rushwa
 
hamjui kusoma alama za nyakati.. mlipoona magari mazuri ya kubebea wafungwa wanaletwa tena dar tu mlijua ni ya nini? ni wakati wa wakubwa nao kusafiri katika decent buses kuliko karandinga....muda wao umefika
 
Kama ni kweli, basi hizo V.I.P. facilities ziwe ni za kulipiwa. Mfungwa au mahabusu atakaetumia hizo facility alipie kama vile guest house au hoteli. Magereza wakifanya hivyo wataongeza kipato cha fedha na wataweza kuboresha mazingira yote ya jela.
 
good idea!, lakini hiyo ifanyike sambamba na kuboresha huduma kwa wafungwa wote
 
Ukonga prison cells being prepared for `VIP` guests?
-Anticipated influx of high-profile prisoners charged with grand corruption

But despite denial from the prisons chief, various other government sources have confirmed a link between the ongoing renovation work at Ukonga prison and the looming prosecution of prominent corruption suspects.

’’In fact, the repair work has been speeded up, possibly because of the expected arrival of VIP prisoners at the Ukonga prison soon,’’ said one source.

Apart from the pending indictments related to the EPA scandal, the PCCB is understood to have already been given consent by the Director of Public Prosecutions (DPP) to proceed with the prosecution of several other grand corruption cases involving politicians and retired senior public officials.

The PCCB Director-General, Dr Edward Hoseah, is on record as saying the government’s corruption watchdog has concluded investigations on at least five cases of grand corruption.

Major graft investigations that the Bureau is understood to have been conducting include dubious tax exemptions extended to the Alex Stewart Assayers gold auditing company, the Buzwagi mineral development agreement, the radar purchase, and the related TANGOLD/Meremeta and Deep Green Finance deals.

This has now been confirmed!( kwa wenye kuweza kusoma magazeti ya TZ someni magazeti ya leo)
Washtakiwa wa EPA na wengine high profile kama Zombe "wamehifadhiwa" VIP prison .......
 
Watuhumiwa wa EPA waponda raha Keko

2008-11-13 10:21:29
Na Joseph Mwendapole

Washitakiwa 18 wanaokabiliwa na mashitaka tofauti ikiwemo kughushi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wanaishi katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko tofauti na mahabusu wengine.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa, baadhi ya washitakiwa hao wamewekwa katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko ambapo wametengwa kabisa na maabusu wa kawaida maarufu kama walalahoi.

Chanzo cha gazeti hili kilielezwa kuwa, Jayantkumar Patel maarufu kama Jeetu Patel na Jonson Lukaza, wanaishi katika vyumba vya VIP, ambapo Jeetu Patel inadaiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu huku Lukaza akidaiwa kuwa na maradhi kama hayo pia.

Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omari Mtega aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu jna kuwa, katika magereza yote hapa nchini, hakuna vyumba vya VIP.

Kamishna Mtega alisema ni jukumu la Magereza kuhakikisha ulinzi na usalama wa wahalifu hivyo ni muhimu walindwe kwa utaratibu waliojiwekea.

Aliongeza kuwa, jamii nzima inawachukia watuhumiwa wa EPA hivyo jeshi hilo haliwezi kufanya uzembe kwa kuwachanganya na watuhumiwa wa makosa mengine.

``Unasikia mwandishi, `EPA is EPA`kwa hiyo sio jukumu la vyombo vya habari kujua usalama wa watuhumiwa na wanalindwaje na hatuwezi kuwachanganya na watuhumiwa wengine kwa kuwa wanaweza wakauawa na lawama zikaenda kwa jeshi,`` alisema.

Aliongeza kuwa, mahabusu ambao ni watuhumiwa sugu kwa makosa tofauti, hawachanganywi na wale wanaofikishwa gerezani kwa mara ya kwanza.

``Kwa mfano, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watuhumiwa gerezani, jeshi haliwezi kufanya makosa kwa kuwachanganya na Abdallah Zombe kwa sababu wanaweza kumdhuru au hata kumuua hasa wale waliokamatwa kwa tuhuma mbalimbali kabla Zombe hajakamatwa kwa tuhuma za mauaji,`` alifafanua Kamishna Mtega.

Baadhi ya masharti ya dhamana ambayo wamekuwa wakipewa ni pamoja na kulipa nusu ya fedha wanazodaiwa kuiba BoT au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Sharti lingine ni kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali, kuwasilisha hati za kusafiria na kuripoti polisi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama.

Hivi karibuni, gazeti moja liliripoti kuwa, serikali ilikuwa ikifanyia ukarabati vyumba vya VIP kwa ajili ya vigogo waliotarajiwa kufunguliwa mashitaka kutokana na wizi uliotokea BoT.

Hata hivyo, baada ya taarifa hizo, serikali ilikuja juu na kukanusha kuwa ukarabati huo haufanywi kwa ajili ya vigogo bali ni taratibu za kawaida wamewekwa katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko ambapo wametengwa kabisa na mahabusu wa kawaida maarufu kama walalahoi.

Chanzo cha gazeti hili kilielezwa kuwa, Jayantkumar Patel maarufu kama Jeetu Patel na Jonson Lukaza, wanaishi katika vyumba vya VIP, ambapo Jeetu Patel inadaiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu huku Lukaza akidaiwa kuwa na maradhi kama hayo pia.

Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omari Mtega aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu jna kuwa, katika magereza yote hapa nchini, hakuna vyumba vya VIP.

Kamishna Mtega alisema ni jukumu la Magereza kuhakikisha ulinzi na usalama wa wahalifu hivyo ni muhimu walindwe kwa utaratibu waliojiwekea.

Aliongeza kuwa, jamii nzima inawachukia watuhumiwa wa EPA hivyo jeshi hilo haliwezi kufanya uzembe kwa kuwachanganya na watuhumiwa wa makosa mengine.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom