VIP Airport kuna maslahi ya taifa?

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Nimesoma habari hii halafu nikawaza masuala muhimu ambayo tumewatuma wabunge wetu kwenda Dodoma kuyawasilisha na yakakosa muda na nikalinganisha na hili ambalo wabunge wetu nusura wapitilize hata ustaraabu wao wakijadili kuhusu chumba cha VIP pale Mwalimu Nyerere International Airport hapa Dar. Hakika sijaona la maana hapo. La msingi hata kimemo kilitosha sana kumjulisha Waziri Membe kuhusu hali hiyo lakini kupoteza muda na kujadili suala hilo ni kuonyesha kwamba hapo Dodoma mmeenda kupiga soga wakati mwingine.


Cassian Malima, Dodoma
Daily News; Saturday,August 23, 2008 @00:03

Wabunge jana walielekeza mashambulio kwa wanaosimamia chumba cha watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, kwamba wamesababisha kishuke hadhi na kuwa kama daladala kutokana na kuruhusu wasio na hadhi kuingia humo holela.

Kwa mujibu wa wabunge, licha ya VIP wa nchini, kero kubwa ni ya raia wa kigeni na hasa wenye ngozi nyeupe ambao wote wanadai kuwa ni VIP. “Sisi tumekuwa wakarimu mno, tunawapa hadhi ya VIP, kwao hawatupi,” alisema Ramadhani Maneno (Chalinze-CCM), ambaye alilidokeza Bunge kwamba kuna wakati wageni wanaostahili husimama mle kama wako kwenye daladala.

Mwenzake, Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Mashariki-CCM), alisema hali ilivyo kwenye chumba hicho cha VIP ni “vurugu tupu.” Alisema wakati fulani alikerwa wakati akitoka safarini Ulaya aliposhuhudia wafanyakazi wa Kampuni ya Saskatel inayojihusisha na TTCL, wakiingia mle huku wakiwa wamevaa kaptula.

“Ati nao wakapita VIP. Wazungu wamefanya pale kuwa ni mahali pa kuvutia sigara, fanyeni ili pale pawe na heshima,” alisema Nsanzugwanko. Kabla ya hoja hiyo kujibiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye hotuba yake ya bajeti ilikuwa ikijadiliwa, Spika aliingilia kati baada ya Nsanzugwanko kuzungumza na kusema chumba kile hakistahili kuwa VIP, bali kilijengwa ili kiwe Ofisi ya Meneja wa Uwanja.

“Mimi nilikuwa Waziri wa Ujenzi wakati uwanja ule unajengwa (miaka ya mwanzo ya 1980). Ile ilipaswa kuwa Ofisi ya Meneja wa Kiwanja. Cha muhimu kwa serikali kutoa fedha ili ijengwe (VIP) nyingine,” alisema. Akiwajibu wabunge, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema hatua zitachukuliwa kurekebisha hali hiyo. Alihoji; “Hivi jamani, kama Membe ni VIP na ndugu zake ni VIP? Alijibiwa “hapana” na hapo akaahidi kukaza kamba wasiostahili wasiingie katika chumba hicho.

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=11551
 
Kuna haja gani ya kuwa na VIP room? Kwa nini kisiondolewe na wale wanaotaka kudekezwa walipie na watumie First Class Lounge. Mheshimiwa Rais aondokee kwenye uwanja wa kijeshi ambako ndege yake itakuwepo. Hivi viji privilege visivyo na maana ndivyo vinavyoturudisha nyuma. Tangu lini mbunge awe VIP?
 
wabunge wamesahau ukweli kuwa tiketi ya kuingia huko bungeni imetolewa na wapiga kura wao matokeo yake badala ya kuwatukuza wapiga kura wao kwa kupigania na kusimamia kwa nguvu zote maslahi ya wananchi wanabaki kujitukuza wao.
Ama kweli demokrasia inaleta ghasia.
 
Mibunge mingine ni kuya ...........sijui kuyafanyeje jamani.

Hebu tafuteni namna. Wana bore kweli hii mijamaa isiyo na point
 
jamani hao ni manafiki watupu kwanza hata huyo membe akiwa ansafiri anafwatana na familia nzima inapita V.I.P makamba nae akisafiri na familia nzima v.ip na wasivyo na adabu wala heshima kama watoto utakuta wanasimama kama wanasubiri matatu pale nairobi wakati kuna siti za kukaa na kuongea

LINGINE WALA WSITUFICHE HII IMEKUWA SEHEMU YA KUPITISHIA MADAWA YA KULEVYA NA WENGINE KUFIKIA KUTOTAKA KUSACHIWA KABISA E.G..UNAJUA WAKIINGIA NA GARI HAWAPITII KWENYE MACHINE SO INAKULA KWA WATANZANIA.......

SWALA LA CHUMBA NA KISCHEKESHO HUYO BWANA ANADIRIKI KUSEMA ALIKUWA WAZIRI WAKATIKIKIJENGWA AKUKIONA AU ANATULETEA UNAFIKI BUNGENI NILISHASEMA MULE NDANI WEHU WATUPU WAMEJAZANA LABDA SASA HIVI KUNA AMBAO WANACHIMBUKIA KIDOGO WAKINA KILANGO NA WENZAKE SILAA NA ZITOO WENGINE MADOIDO MATUPU
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom