Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,877
- 2,758
Hili swali watanzania tunajiuliza? Iweje viongozi wote nchi hii wakatibiwe nje ya nchi? Hivi kuwa kiongozi ina maana unakuwa sio raia? Ni mazoea kuwa kila kiongozi wa juu akiumwa anapelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Wanapelekwa India, Uingereza, Ujerumani, Kenya na kwingineko. Siku za karibuni tumesikia Mzee Malechela kapelekwa Uingereza na sasa yuko Marekani mapumzikoni. Muda si mrefu tumeambiwa Prof Lipumba na Mark Mwandosya wako Apollo-India kwa matibabu.
hatukatai kuwa kwa kuwa ni viongozi ni lazima wapewe treatment ya hali ya juu. Tnajiuliza, hizi treatment tunazowapa (ni kodi zetu) zina tija gani kwetu sisi wananchi? Ni maamzuzi gani wayafanyayo ambayo kweli tunaona wana haki ya kupata hizi huduma?
Ni kwa nini basi kwa kuona kuna kasoro katika hospitali zetu, serikali kupitia hawa viongozi haioni kuna haja ya kuiboresha sekta ya afya nchini? Wanachojua tu ni kupitisha bajeti na kuchukua posho mbalimbali za makalio.
Tujiulize kwa mfano, mzee Malecela katika kulitumikia taifa kwake, aliisaidiaje sekta ya afya hapa nchini? Ni ushawishi gani na juhudi zipi alizofanya ili kuhakikisha kuwa sekta ya afya inaboreka. Leo hii anaeda kutibiwa Uingereza na sasa yuko mapumzikoni Marekani. Kwa nini hakutibiwa mathalani Muhimbili ama Agakhani halafu aende marekani kupumzika?
Hatupendi viongozi wetu wafe kwa maradhi yanayotibika. Wala sisi raia hatupendi kufa. Ila watuambie, kuwa kwao madarakani kuna tija gani kwetu sisi kama hadi leo kila kiongozi anaenda kutibiwa nje ya nchi? Ni nini hasa wanachofanya katika hivyo viti wanavyokalia ikiwa sekta ya afya ni mbovu, nishati mbovu, miundombinu mibovu, kilimo kibovu, elimu mbovu, siasa yenyewe mbovu... karibu kila kitu kibovu. Bahati mbaya karibu kila kitu ni kibovu kwa raia lakini kwa viongozi ni tofauti, ndio maana wanatibiwa nje n.k.
Kwani imeshindikana kujenga hospitali tatu za maana hapa nchini ambazo viongozi wetu wangeweza kwenda kutibiwa huko? Kila siku wanazungumzia vipaumbele lakini wanakuta wameshaweka vingi hadi wanashindwa kushika kipi ili kukikamilisha kwanza. Na huu usemi wa kusema 'wakati wenzetu wanatembea sisi tukimbie' ndio tatizo jingine. Si kila mbio zina baraka. Na kwa nini tukimbie? Tulikuwa tukifanya nini hadi tukapitwa hivyo? Na waliosema kuwa polepole ndio mwendo walikosea? Tatizo hawa viongozi wakikimbia, pumzi zinawaishia wanabaki kutweta kama samaki aliyebwagwa nchi kavu. Wakitembea, hata kinyonga ana nafuu. Wakikaa wanalala tu! Na huu ndio mwanzo wa matatizo ya taifa hili. Siafiki hawa viongozi kwenda kutibiwa nje kama hatuoni tija yoyote tka kwao. Bora tubanane kwenye hospitali zetu na kama ikishindikana tufe wote tu. Huo ndio uzalendo na kujibainisha na hali halisis ya watanzania wengi-Patriotism and empathy