Viongozi wetu wanayaweza haya!

grndossy

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
311
80
Rais wa Uruguay Jose Mujica (77) ametajwa kuwa kiongozi maskini duniani. Rais huyo ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la utani la "el presidente mas pobre" maana yake Rais maskini alichaguliwa machi 2000. Rais huyu analipwa mshahara wa $12,500 (saw na shs.19.3mil) lakini 90% ya fedha hizo anazitoa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi maskini hivyo anabakia na $1,250 (sawa na shs.1.9mil). Mali ya thamani kubwa anayomiliki ni gari aina ya Volkswagen Beetle yenye thamani ya $1,945 (sawa na shs.3,069,210 - current rate). Rais huyu amekataa kukaa Ikulu anaishi kwenye nyumba yenye jina la mkewe iliyoko shambani kwake. Mke wake Lucia Toplansky ni Seneta naye pia amekuwa akitoa sehemu ya mshahara wake sadaka kwa maskini.

Katika uongozi wake ameweza kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la rushwa. Uruguay ilikuwa nchi ya pili kwa rushwa katika nchi za Latrin Amerika.

Rais huyu wa ajabu hana Account bank, hana madeni na anapenda kuzunguka mitaani na mbwa wake anayeitwa Manuela.

Haya wana JF kazi kwenu. Hapa kwetu inawezekana????????????


Source:Uhuru Newa paper 04/10/2012
 
Duh ametisha

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nani anataka shida Tanzania.................!
Kila siku wenzio tunasafiri kwenda Ulaya kupunga upepo.................!
Tunajenga ma -estates mijini mwetu.........!
Akaunti za shilingi hatuzitaki tuna ma-akaunti ya midolaz na mi-yuroz tena nje ya nchi...................!!
Acha kabisa.....!
Labda kwa Kagame wanaweza..............
 
Back
Top Bottom