Viongozi wetu oneni haya!

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Sikutegemea hata siku moja kuwa Tanzania itafikia mahali ambapo viongozi wenyewe kwa wenyewe tena wa chama kimoja kile kinachotawala wataanza kurushiana makombora ya shutuma, matusi na kejeli!
Hivi kuna collective responsibility tena siku hizi? Inakuwaje viongozi wa ngazi za juu wenye dhamana ya kuhakikisha tunakuwa na maadili.. wao ndio wamekuwa wa kwanza kukiuka? Inanifanya niwaze - Nyumbani baba na mama wenyewe kuheshimiwa wanapoonyesha kuparaganyika kinachofuata ni vurugu kwenye familia na kila mtu kuanza kujifanyia kila anachotaka bila woga.
Hivi Tanzania Twenda Wapi?
 
Mimi nakwambia sasa hivi ni kuhakikisha kwamba Kikwete hagombei tena 2010 maana hastahili tena kuwa Kiongozi wa nchi angekuwa na mapenzi ya kweli kwa nchi yetu wala asingesubiri 2010 angejiuzulu sasa labda tukawa na Serikali ya muda hadi 2010. Matatizo yte ndani ya chama na Serikali yanasababishwa na udhaifu na woga wake mkubwa kama kiongozi. Alidhani kuongoza nchi ni lelemama.
 
Nashangaa Kikwete kushindwa kuwafunga gerezani akina chenge, rostam, lowasa, sofia paka n.k

Kwa upande mwingine nafurahi kwamba next time kikwete ataogopa kutumia pesa za watu ili aingie madarakani.
 
Ukweli ni kuwa kikwete na serikali yake wanahitaji maombi ya nguvu
inabidi watu wafunge na kusali,,,vinginevyo..
Ni kama wana pepo la upumbavu....kikwete anafikiri this is just a joke..
Anatakiwa kuombewa....
 
hakuna unafuu wowote hapo.......kwani mbali ya ccm na kikwete hakuna chama ambacho kinaweza kuleta mapinduzi ya kweli katika nchi hii.. kwani vyama vyote pinzani falsafa zao ziko mlengo mmoja na za ccm.... ikiwa demokrasia haipo ndani ya chama unategemea wataweza kushika hatam,u ya nchi... UONGOZI WA TAIFA HILI UMEKUWA WA kupokezana vijiti.. amini nawaambia.. hata wakae chadema au cuf... i would be the same story... watakachokifanya miaka yote mitano.. ni kuwafungulia kesi viongozi waliopita.. wakati wanajua kuwa kuna wakati unalazimika kukumbatiana na adui yako ikiwa kufanya hivyo kutamaanisha usalama wenu wote wawili.....

I am not gud in politics.. and vere will coz its disgusting but i think the only way out.. is torn aprt those vyama kwanza... yaanji wanamapinduzi wa kweli anatakiwa ahakikishe anang'oa mizizi ya ccm kuanzia ndani kwenyewe na ya CUF na ya Chadema.. kuleta demokrasia ya kweli.. huwezi kutegemea kwenda kwa wananchi wakati unapractise the samedrama kama ya mpinzani wap...

Kitendo cha wanasiasa kuacha kutuambia na kufanya kwamatendo yale tunayoyataka kufanyiwa na kujigeuza wao ndio wasemaji wetu wakuu na kwa kupoteza mda wa kutaka kumuumbua wenzie huyo kiongozi hatufai..

kila kitu kina sehemu na nafasi yake .. pelekeni maswala hayo kunakohusika then fanyeni mengine... sio kukimbilia kwenye magazeti na kuonmyeshana AaAH!.. nishachoka....... samahani nina hasira nahisis nitaanza kutoka nje ya mada... bora nikae kimya

*****************************
If You think You know all the Answers, then you havnt been asked all the Questions
 
Ni utovu wa nidhamu na ukiona dalili hio jua kabisa nyumba haina amani hata chembe
What is next ??
 
Ukitaka kuona kuwa nchi yetu inaendeshwa kihuni fikiria ishu ya richard monduli. Serikali na Bunge waliahidi kuwa litafikia ukomo November lakini wapi? hakuna mwananchi wala wabungu wanaojua kila mtu amepigwa na butwaa. kwakweli inasikitisha sana.
Jamani mimi napenda nitoe challengi moja, kama kila mwanajamii ataweza kushawishi vijana ambao huwa hawapigi kura wakajiandikishe na kupiga kura tutakuwa tumepata watu wangapi? Tusikae maofisini jamani usomi wetu tuutumie kuelimisha jamii ili waweze kujua ubaya wa mkubwa wetu na watafanya mabadiliko tusiwaachie wapinzani tu. tukiendelea kulalamika kwenye net hatusaidii kitu kwani kuna watanzania wangapi wanajua kuna jamii.com? na ni percent ngapi ya watanzania wenye access ya umeme na vyombo vya habari? Hao ndo watakao mpatia tena madaraka na tutakuwa tunaishi maisha ya wasiwasi tusijue kinatokea nini tena kesho. HIMA HIMA JAMANI TUMIA ELIMU YAKO KUSAIDIA WANANCHI
Kumbukeni usemi wa baba wa taifa "Mtu aliyesomeshwa na wananchi masikini na akashindwa kuwasaidia ni mhaini"
 
Sikutegemea hata siku moja kuwa Tanzania itafikia mahali ambapo viongozi wenyewe kwa wenyewe tena wa chama kimoja kile kinachotawala wataanza kurushiana makombora ya shutuma, matusi na kejeli!
Hivi kuna collective responsibility tena siku hizi? Inakuwaje viongozi wa ngazi za juu wenye dhamana ya kuhakikisha tunakuwa na maadili.. wao ndio wamekuwa wa kwanza kukiuka? Inanifanya niwaze - Nyumbani baba na mama wenyewe kuheshimiwa wanapoonyesha kuparaganyika kinachofuata ni vurugu kwenye familia na kila mtu kuanza kujifanyia kila anachotaka bila woga.
Hivi Tanzania Twenda Wapi?

Actually swali lingekuwa tupo wapi????, Navyoona mimi jibu lingekuwa tumepotea, safari tulianza 1961 somewhere in between we missed a turn and took the wrong way mpaka sasa hatujui tulipo na hata tulikotoka hatujui. Tupo tupo tu.

Veracity, tunahitaji mtu/watu kuturudisha mahali ili tuendelee na safari vinginevyo tutakuwa kwenye haze amabamo tutazunguka tuu mpaka tutachoka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom