Viongozi wetu na 'title' bandia

Unachotaka kusema nini unaonekana mambo ya hapa duniani hujui kabisa pengine tukusaidie hebu sema unachotaka ni nini hasa?
huu ukali wote sababu unajua tunakuja kumshukia dokta feki jakaya kikwete anayelobby kutunukiwa udaktari...
 
Mkuu pamoja na maswali yako unayo yahoji ila mimi nataka uzitendee haki PhD za watu hapa kati ya wote uliowaorodhesha hapo kuna mmoja hastahili kutumika kama mfano ktk bandiko lako kwasababu hakuna chuo chochote kilichobainishwa kamba alisoma nakupata hiyo PhD hivyo tafadhari kwaheshima ya PhD za watu unatakiwa kumwondoa haraka hapo

Sikazi yangu kubainisha ni nani bali hata matendo yake hubainisha elimu ndogo Aliyonayo na tayari kesha shindwa kuongoza nchi ipoipo tu inajiendea kanakwamba haina kiongozi.

BACK TANGANYIKA

Ubarikiwe mkuu kwa kutokupepesa macho
aondolewe haraka hapo
 
Unachotaka kusema nini unaonekana mambo ya hapa duniani hujui kabisa pengine tukusaidie hebu sema unachotaka ni nini hasa?


Nilivyoelewa mimi anataka kujua, ni kwa nini mtanzania au baadhi ya watanzania wakiwa na elimu kubwa i.e Phd, wanapenda saana kutukuzwa (kusifiwa) na elimu yao...!? nipo tayari kukosolewa ikiwa nimemwelewa vibaya.
 
Tatizo mnashindwa kutofautisha honorary awards na awards za kusotea. Ulaya wanasiasa wengi wenye honorary PhDs wanafuata masharti ya honorary hasa lile la kutolitumia kwenye official addressing. Hapa bongo ni foul tu, mtu ana honorary kama JK, Mengi, Karume etc halafu kila siku wanaitwa ma Dr. hadi kwenye vyombo vya habari. Mtu aliyeusotea uDr. au uProf. wake hata akijiita hadi chooni sioni shida yoyote mie.
 
NI kweli Mkuu. Ukweli ni kwamba huko ulaya na Marekani hata wakiwa katika mazingira ya vyuo hawahusudu hizi title, utakuta maprofessor wanataka waitwe tu kwa majina yao ya kwanza. KUna watu kule wanakasirika ukiwaita Prof., lakini huku kwetu Prof linakuwa jina la mtu, watu wanalikubali bila hata kutaja Prof na jina lake halisi. Unakuta mtu anasema, "naomba kukuona Prof", na jamaa anakubali kuitwa hivyo.

Tatizo hapa kwetu ni malimbukeni wa title. Watu wanaona ujiko sana kuwa na hutu tu-degree walitotupata kwa shida sana, na ndio maana wanataka kutukuzwa na hizi title wakati hawana lolote la maana wanalochangia katika maendeleo ya nchi na jamii.
Swadakta mkuu..Hizo ni academic title, zinafanya kazi tu pale unapokua mazingira ya universities. Sio mtu bungeni ni prof, dr, dah......ulimbukeni wa hali ya juu.
 
Kuna wakina profesa Maji marefu, Nasikia Stella Manyanya ana elimu ya fundi mchundo lakini naye anajiita Injinia Manyanya.

Inabidi tufike wakati tuseme ukweli kuhusu hili,Sijawahi kusikia Nyerere sehemu yoyote akijiita profesa Nyerere japokuwa alikuwa alikuwa profesa,alipenda kuitwa mwalimu. viongozi wa sasa wamejaa sifa na kufikiri akiitwa profesa ama dr basi ataogopwa.
 
Mimi nimemwelewa vizuri ila wewe ndiye huelewi au hutaki kuelewa. Hata Hillary Clinton sijawahi sikia akiitwa Dr Hillary Clinton, au Dr Gordon Brown etc etc. Ukweli ni kwamba vyeo vya kisomi vinatumika tu unapokuwa kwenye mambo ya academic na siyo kwenye siasa au mitaani. Ndiyo maana ukienda UN watu wengi ni ma Phd holders na hutakiwi kutumia hizo title, wengi ni former professors ila huruhusiwi kutumia vyeo vya academic kazi ambayo siyo ya academic.
Kwa hiyo niseme hapa Tanzania ni ulimbukeni ndio unawasumbua na nadhani wenzetu uwa wanatucheka sana. Mfano hata zile degree za heshima za akina Kikwete eti naye anashadadia kuitwa Dr Kikwete!!

Unaonekana hujui kitu sijui usaidiweje mkuu.
 
Hivi ni kwa nini hapa nchini kwetu (TZ) huwa ni muhimu sana au tuna mazoea ya kumuita mtu mwenye PhD, Dr. fulani au Prof. fulani kama vile Dr.Magufuli, Dr.Slaa au Dr.Kikwete, Dr.Lamwai au Prof. Muhongo au sijui Prof.Kapuya au Prof.Magembe n.k?
Mbona nchi nyingine hasa za Wazungu hakuna hayo mambo?
Kwa mfano Raisi wa Marekani Baraka Obama ni prof. lkn sijawahi kusikia hata siku moja Mtu akisema Prof. Obama kwanza wanasiasa wengi sana wa Ulaya na Marekani wana PhD lkn sijawahi kusikia Mtu akiwaita Dr.!

Kwa Wazungu au Nchi za Ulaya na Marekani Mtu ataitwa kwa kutumia Dr. au Prof. pale tu anapokuwa yuko kwenye mambo ya kielimu, kwa mfano Raisi Baraka Obama akienda Chuo kikuu cha Harvard basi watamuita Prof.Obama lkn sio mitaani kama hapa kwetu, utakuta hata mitaani kama mtu ana PhD ukimuita bila ya kuweka hilo Dr. ni ugomvi sasa ni kwa nini?
 
Mrema naye siku hizi anaiwa Dokta Augustine Lyatonga Mrema, msiniulize kasomea wapi, jibu ni sijui.
 
  1. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
  2. Dr. Mary Nagu
  3. Dr. Makongoro Mahanga
  4. Dr. Emmanuel Nchimbi
  5. Dr. David Mathayo David
  6. Dr. Diodorous Kamala
  7. Prof. Steven Ngonyani
  8. Dr. Hussein Mwinyi (hakufanya intern to qualify to be MD)
  9. Dr. Mary Mwanjelwa
  10. .....
Endelezeni hapo chini

Hii ni aibu
 
Back
Top Bottom