Viongozi wetu na kushangaa mahekalu Oman

Wadau ninaangalia taarifa ya habari ITV, kilichonishangaza ni taarifa ya Raisi na viongozi wengine wako ziarani Oman,kilichonishangaza mimi ni jinsi viongozi wetu walivyokuwa busy kushangaa hekalu muda wote, sijui nini tafsiri yake ,!? kwa mlioona niambieni

Upumbavu mtupu. Jaribuni kuheshimu viongozi wenu hata kama wanautendaji mbovu. Nyie ndio mnaweza hata kucheka makalio ya baba zenu yakiwa wazi. Shenzi kweli. Those are state figures no matter how inefficient they work!
 
Hv kumbe kuangalia kitu kwa mshangao jinsi kilivyotengenezwa na nakshi zake ni ushamba!!!! Nikikwambia wewe MSHAMBA naamanisha nini.? Ni kweli kuwa ungeenda wewe usingeshangaa?
Sasa nyie mngeona video ya PM wa Zimbabwe alipokwenda Uingereza si ndiyo mngechoka zaidi. Watz bana vimaneno maneno tuuu..
Binafsi sioni aibu kushangaa kwasababu sivijui vitu vyote...unajifichaficha nini sasa si unafiki huo.

Hilo la USHAMBA umelileta wewe, tumejadili namna ambavyo viongozi wetu walikuwa wanashangaa kiasi cha kushindwa kufuatilia kilichokuwa kinaendelea
 
Upumbavu mtupu. Jaribuni kuheshimu viongozi wenu hata kama wanautendaji mbovu. Nyie ndio mnaweza hata kucheka makalio ya baba zenu yakiwa wazi. Shenzi kweli. Those are state figures no matter how inefficient they work!

state figures MY B..T, watu wachemke afu uje utuletee nyimbo zako hapo, kwanza nadhani hadi watakaporudi wengine watakuwa hawajui walienda kufanya nini kule
 
hiyo inamaana ukienda wewe ambae hukuwahi hata kupata exposure ya kufika huko utapoteza fahamu,mie pie nimeshangaa ule ushangaaji wao nadhani hata wenyeji wao wamewashangaa.
 
Hata kama kashangaa, huyo bado ni kiongozi wako. Political hatred drives you roughly guys, slow down and think BIG.
 
Wadau ninaangalia taarifa ya habari ITV, kilichonishangaza ni taarifa ya Raisi na viongozi wengine wako ziarani Oman,kilichonishangaza mimi ni jinsi viongozi wetu walivyokuwa busy kushangaa hekalu muda wote, sijui nini tafsiri yake ,!? kwa mlioona niambieni

Mweee! Bagosha! What a shame!
 
nimeangalia itv saa mbili sikuamini, nkarudia saa 4, aibu. Itv walivyowambea basi kile kipande cha Membe wamerudia kama mara 10 hv. Membe katisha nahisi atakuja na tuzo na naamini hakuambulia chochote ktk mazungumzo yale. Kwi kwi kwi
 
aisee wameshangaa bwana!jk maskini kila dk anastaajabia lile kasri, wale ndo waloitawala zenj ati. Jumba linameremeta wabongo wakaona magogoni ni km ka gesti flani huko manzese. Kweli imetia aibu
 
Kumbe tulioona hiyo comedy tulikuwa wengi nimecheka mwenzenu sijui pale darini kulikuwa na nini ngoja akija nitamuuliza.
 
Jamani labda wameshindwa kujizuia..ila nadhani walioweka zile picha walikuwa na maana yao.
 
Mkuu, dari lile ni la tanzannite tupu, tiles na kuta za hilo kasiri ni dhahabu tupu toka Bulyanhuru Kahama, madirisha na milango ni ya almasi tupu toka Mwadui Shinyanga, bustani imejaa twiga, pundamilia vifaru, simba n.k. toka Serengeti. Hivyo si kwamba wanashangaa ila wanaangalia walichokuwa wanaambiwa kama tetesi na ndiyo madhumuni ya hiyo ziara. Ila sijui wakirudi labda na sisi tunaweza fanya hivyo pale Magogoni ili kuitangaza nchi yetu!!!!
 
Hilo la USHAMBA umelileta wewe, tumejadili namna ambavyo viongozi wetu walikuwa wanashangaa kiasi cha kushindwa kufuatilia kilichokuwa kinaendelea

Kwahivyo kushangaa ni dalili ya nini..!!
 
Ivi kweli angeenda, afu mwenyeji wake anamwonyesha mahekalu, halafu mkuu asionyeshe kushangaa hata kwa kuingiza kweli? Mwenyeji wake angemwelewaje?

Chukulia wewe unamletea mpenzi wako zawadi ukiamini ni kubwa na itamsuprize mpenzi wako, afu mpenzi wako asionyesha kustuka, wala kusema asante utachukuliaje.

Mi naamini hao wakuu walikua wanaigiza kushangaa, ili kuwaridhisha wenyeji wao.
 
a very nice political excuse, lakini ukweli utabaki palepale
 
Hivi mtu anayeangalia na anayeshangaa tofauti zao zipo wapi? And don't tell me kwamba that was the first time for kikwete and other delegates to step ndani ya mansions kubwa kama hizo! Unapoteza muda kujadili KUJADILI UPUUZI WA KUSHANGAA. Sometimes sio lazima uweke comment kweli kila post, you may skip the post kama haina issue ukiwa muungwana.
 
kumbe tuko wengi tulioona,nilicheka sana tena walikuwa wanarudua rudia sana makusudi mkuu wetu na membe wakishangaa ukuta na kwenye dari,yani aibu sasa apo wakiambiwa chochote si watafata tu maagizo,yani aibu wametishaje kwa kushangaaaaaaaa
 
Jumba lenyewe hili hapa linaitwa PALACE

sultan-qaboos-palace-oman.jpg

2135645472_68eabf8560_b.jpg
 
Back
Top Bottom