Viongozi wetu na Kingereza

ndio aina ya viongozi ambao wengine pia hutuwakilisha nje.Hawa ndio hutupiga longolongo kwa kiswahili, halafu wakiwa nje hawalewekei wala kuelewa wenzao,mwishowe akipigiwa .Okay..?wanasema okay.wanpewa mikono na ahsante kwa kumalizia deal haraka.Then wakirudi wanajisifu kuwa mamabo yalikwenda vizuri na walisifiwa sana kwa kufanya mambo haraka.Kabla hawajamalizia kushangilia bongo ndipo hawa wabongo wasio na vyeo ila wapo smart wanaanza lia kuwa kimenuka.
 
Kuna haja ya watanzania kukubaliana namna ya kuwapata viongozi wenye uelewa lakini pia wenye kufahamu lugha gani watumie kwa njia ya mawasiliano hembu angalieni viongozi wenu wa CCm wanavyowasiliana kwa lugha ya kingereza

Hiyo barua nimeiona, ngoja niangali uwezekanom wa ku upload. Shame on nyinyiem
 
Jamaa katisha. Nimefurahi aliposema, "all people they supposed to be accoutable"

Mimi kanimaliza APo aliposema ( remember the government of republic union of Tanzania)Tehe Tehe Tehe kingine ni jina la domokaya na jinsi anavojua kutafuta dodoso jamaa nu mkali
 
Hata ujumbe katika barua una utata! Aya ya pili " All people must answer this question"
Hapakuwa na swali moja tu katika sensa. Kama kiingereza hakipandi tusione haya wala
kujisikia vibaya kutumia kiswahili kwani ndio lugha ya taifa!
 
Kitu kizuri katika hiyo barua.. kwenye content, maneno yote hapo ndani ni ya Kiingereza. Amefanya 'spell check' ya kufa mtu!!

Nimeangalia upande chanya zaidi.
 
Turudi nyuma kidogo, hivi tukiambiwa baadhi yetu humu JF tuirekebishe hiyo barua, ni wangapi watathubutu? Mushi amethubutu, ameweza na anasonga mbele. Ujumbe umefika kwa walengwa.

Mitazamo kama hii ya akina Kashaijabutege ya kutetea na kuahalalisha UZEMBE ndio imekwamisha Bongoland!! Ujumbe gani umefika kwa walengwa? Kwanza ninafikiri hii barua ni feki - sidhani kama kuna mtu ameandika bali ni mchezo wa kunogesha jukwaa!
 
ndio aina ya viongozi ambao wengine pia hutuwakilisha nje.Hawa ndio hutupiga longolongo kwa kiswahili, halafu wakiwa nje hawalewekei wala kuelewa wenzao,mwishowe akipigiwa .Okay..?wanasema okay.wanpewa mikono na ahsante kwa kumalizia deal haraka.Then wakirudi wanajisifu kuwa mamabo yalikwenda vizuri na walisifiwa sana kwa kufanya mambo haraka.Kabla hawajamalizia kushangilia bongo ndipo hawa wabongo wasio na vyeo ila wapo smart wanaanza lia kuwa kimenuka.

Aisee kwakweli inachekesha sana! inafaa jukwaa la Burudani,lakini message imefika bwana,hata hivyo siyo lugha yetu ya mama. Angalizo siku nyingine ajitahidi kupeleka kwa wajuzi au wakubwa wake wanaojua vizuri lugha hiyo ili waipitie!
 
Censer - ni nini?
Kwa vile hakuzungumzia census basi huenda maudhui ya barua ya J. Mushi ni sawa. Ole ni kama alikuwa amekusudia sensa (kiingereza census).

Living visitors ndio nini?
Iko kama anazungumzia mambo ya sayari za Mars na Jupiter. Kama ndivyo basi ni sawa. Ole! Kama anazungumzia mambo ya sayari hii ya dunia!

IF YOUR REFUSE TO BE COUNTABLE...
OR STOP CENSER OFFICER TO DO THE JOB OF COUNTING PEOPLE FROM 26.08.2012....
AND 7 DAYS MORE ITS IS CRIMINAL CASE.....
THEN YOU WILL BE CHARGED IN COURT AND FINE SENTENCED IN PRISON FOR 6 MONTH.

Hebu fikiria umekwenda kwenye ofisi ya umma kupata huduma kisha unakutana na huyu mzembe tena akiwa katika lugha aliyoizoea ya kiswahili.....pata picha itakuwaje?

Zipo sababu nyingi sana za ni kwanini Tz ni maskini!
 
Mitazamo kama hii ya akina Kashaijabutege ya kutetea na kuahalalisha UZEMBE ndio imekwamisha Bongoland!! Ujumbe gani umefika kwa walengwa? Kwanza ninafikiri hii barua ni feki - sidhani kama kuna mtu ameandika bali ni mchezo wa kunogesha jukwaa!

Barua hii sio feki. Mie sitetei wazembe, bali nimerudia slogan yenu: TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE". Kwani darasa la pili kuandika barua nzuri kama hii hakuthubutu?
 
Back
Top Bottom