Viongozi wetu na fikra mgando

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Nimejaribu kusikiliza muelekeo wa michango ya wabunge wetu,baraza la mawaziri na wadau mbalimbali kuhusiana na budget 2011/2012 napata masikitiko.miaka 50 baada ya uhuru bado tumejikita katika kuboresha kilimo!sio ccm au cdm wote fikra zetu zinazungukia pale pale.sijasikia mbunge aliyekuja na mawazo mapya yanayoendana na dunia ya leo. Kwa sasa kuna watanzania zaidi ya milioni 40, wengi wa watanzania wanatumia au wanatarajiwa kutumia vifaa vya kiteknolojia kama vile simu, laptop,T.V n.k

Vyombo vya usafiri,vifaa vya elimu na afya ni maeneo mengine yenye uhitaji mkubwa.kinachoshangaza ni kwamba hakuna anayefikiria kuanzisha viwanda vitakavyokidhi mahitaji haya.je tunaogopa au tunaona haiwezekani?kwa nini tusiwashirikishe wadau wa maendeleo watuwezesha kujenga viwanda hivi (at any cost), tunabaki kuimba tu kilimo kwanza kilimo endelevu na mambo kama haya.

Sekta ya mawasiliano inachangia nearly 20% kwenye GDP huku kilimo kikichangia 4%.nashangaa kwa nini tunainvest kwenye loss?eti kilimo kinaajiri 75% !!sidhani kama hii ni sababu inayoridhisha kwani naamini sio lazima wote tuajiriwe ili nchi iendelee.tusomeshe few elites ambao tutahakikisha wanarudi nchini kuleta maendeleo.kilimo tumekipendelea miaka mingi tu lakini hakina tija.wabunge vijana mnaotuwakilisha inakuaje mnakua na mawazo yale yale?

Toeni mawazo mbadala.

Kwa sasa naishia hapa.
 
Mh zitto haitoshi kutumia IPAD!Weka mawazo mbadala yanayoendana na technolagy.
 
Ntaonekana kama nachafua hali ya hewa lakini amini nawaambia dunia ya leo haitasubiri tusomeshe watanzania wote,halafu tujenge barabara ya lami kila kijiji,kila mkulima awe na trekta na mwisho tuanze kujenga viwanda.hivi vitu vifikiriwe pamoja na utekelezaji uanze immidietly.
 
Back
Top Bottom