Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Nimewaangalia viongozi wetu watano wa Afrika wakiwa na Gordon Brown kwenye mjadala wa Uchumi huko Davos, nimeishiwa na nguvu kabisa ya kuamini kwamba hawa viongozi wetu wa Afrika wanao uwezo wa kututoa hapa tulipo. Wote watano hakuna hata mmoja wao aliyeonyesha ni kwa jinsi gani Waafrika tutashiriki kwenye kuleta mabadiliko duniani na kwenye bara letu. Kila mmoja kwa kuhamanika (Desperately) alikuwa anaonyesha ni kwa jinsi gani anahitaji kusaidiwa na "wawekezaji" ili wananchi wake wapate nafuu. Nimemwangalia Kikwete hadi nikajisemea moyoni "huyu jamaa si angebaki ashughulike na mgomo wa Madaktari kuliko hili analolifanya"
Mambo ya ujenzi wa madarasa na kuongeza waalimu haya ni mambo ya kuzungumza kwenye vikao na wazee pale Diamond Jubilee na siyo Davos. Sijasikia Kilimo cha kisasa, ulinganifu wa kibiashara duniani badala yake nasikia watu wazima wakiomba omba hadharani .Sasa nimeelewa ni kwa nini watu kama Jenerali Ulimwengu kila wakiandika makala zao ni lazima jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere litajwe!! Hawa viongozi wetu wa sasa sijui wakoje?