Viongozi wenye kuzuwia maoni ya wengine washitakiwe

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Zanzibar sio mali ya chama kimoja

Posted on August 6, 2012 by zanzibaryetu

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yussuf Mohd Yussuf akitoa hotuba ya Kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai ili kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Kumpata Mgombea Uwakilishi Jimbo la Bububu kufuatia Kifo cha aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo,Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif Suleiman ameishangaa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kushindwa kuwafikisha mahakamani baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wanaowatisha wanachama kwa kutoa maoni tofauti na mtazamo wao.

Akichangia mada ya sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakar, Waziri Rashid Seif alisema kuna kila sababu ya kukamatwa kwa viongozi hao wa CCM wenye tabia ya kutoa matamshi ya vitisho kwa watu wenye kutaka mabadiliko ya mfumo wa muundo wa Muungano.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inakataza mtu au taasisi kumzuia mtu mwengine kutoa maoni yake au kumlazimisha aseme anavyotaka yeye, sasa hawa viongozi wa CCM wanaotaka kuwanyanganya kadi Wawakilishi wao si wanakiuka sheria hii" Alisema Waziri Seif.

Waziri huyo ambaye alichukuwa nafasi ya Waziri aliyejiuzulu kufuatia kuzama kwa meli ya Mv. Skagit hivi karibuni, alisema kwamba atashangaa sana ikiwa Tume ya Jaji Warioba itakaa kimya kutokemea au kuwachukulia hatua wale wote wanaotoa vitisho dhidi ya watu wenye mitazamo na maoni tofauti kuhusu Katiba mpya.

Alisema kila mtu yuko huru kutoa maoni yake mbele ya Tume na si haki kwa mtu au Chama chochote cha siasa kuwalazimisha wanachama wake kutoa maoni ambayo hayatokani na mitazamo yao binafsi. Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT) Zanzibar , Asha Bakar Makame amewataka viongozi wenzake ndani ya CCM kutowatisha wanachama wanaotoa maoni wasiyoyapenda.

Akichangia katika semina hiyo, Makamu huyo Mwenyekiyi ambaye ni Mwakilishi wa Viti Maalum alisema ni jambo la kushangaza katika ukuaji wa demokrasia wakajitokeza watu kuanza kuwazuia wengine kuwa na mawazo huru kwenye mchakato wa kupata Katiba mpya.

"Jamani tusitishane, kama CCM kila mtu ni CCM hapa, hakuna mtu asiyenijua msimamo wangu kuhusu Chama ninakipenda na nitakitetea,lakini si vizuri kuanza kutishana kwa kuambiana huyu hivi huyu vile haifai jamani" Alisema Makamu Mwenyekiti UWT.
Makamu huyo Mwenyekiti wa UWT alikumbusha kwamba wakati wa kutafuta maridhiano ya kisiasa Zanzibar wapo wana CCM na Viongozi waliopinga suala hilo ,lakini hakuna mtu aliyeadhibiwa, hivyo aliwataka kuvumilia katika suala zima la maoni tofauti kuhusu Muungano.

"Wakati tunakwenda kwenye kura ya maoni mwaka 2010 wapo wenzetu wengi walipinga, tena walikuwa wakijulikana,lakini hakuna mtu aliyetiwa adabu na Chama ingawa msimamo wa kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ulikuwa ni maamuzi ya Chama chetu tulikutana Butiama na Dodoma tukakubaliana…mbona hakutiwa adabu mtu" Alihoji Asha Bakar.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura(CCM),Hamza Hassan Juma alisema Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Kikwete hajazuia kutoa maoni tofauti isipokuwa aliwataka wananchi kuvumiliana maana kila mtu atakuwa na maoni yake.
"Mimi nampongeza sana Mwenyekiti wetu,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa siku ile akizundua Tume pale Ikulu, alisema kama wewe uyapendi mawazo ya mwenzio na yako pia kuna wasiyoyapenda,lakini la muhimu kustahamiliana" Alisema Mwakilishi huyo.

Hamza aliongeza kwamba CCM ni Chama bora na kamwe hakiogopi mageuzi na ndio maana hata mageuzi ya kisiasa mwaka 1992 ilisimamia vema na nchi ikaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, hivyo hata katika suala la maoni kuhusu Muungano halitakuwa na matatizo maana wananchi wako huru kutoa maoni yao .
 
Hawa viongozi wa CCM ndio wavunjaji wa demokrasia tanzania. Lazima wadhibitiwe vyenginevo wanaweza kuleta hasara kubwa katika jamii yenye amani.
 
Zanzibar sio mali ya chama kimoja

Posted on August 6, 2012 by zanzibaryetu

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yussuf Mohd Yussuf akitoa hotuba ya Kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai ili kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Kumpata Mgombea Uwakilishi Jimbo la Bububu kufuatia Kifo cha aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo,Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif Suleiman ameishangaa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kushindwa kuwafikisha mahakamani baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wanaowatisha wanachama kwa kutoa maoni tofauti na mtazamo wao.

Akichangia mada ya sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakar, Waziri Rashid Seif alisema kuna kila sababu ya kukamatwa kwa viongozi hao wa CCM wenye tabia ya kutoa matamshi ya vitisho kwa watu wenye kutaka mabadiliko ya mfumo wa muundo wa Muungano.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inakataza mtu au taasisi kumzuia mtu mwengine kutoa maoni yake au kumlazimisha aseme anavyotaka yeye, sasa hawa viongozi wa CCM wanaotaka kuwanyanganya kadi Wawakilishi wao si wanakiuka sheria hii” Alisema Waziri Seif.

Waziri huyo ambaye alichukuwa nafasi ya Waziri aliyejiuzulu kufuatia kuzama kwa meli ya Mv. Skagit hivi karibuni, alisema kwamba atashangaa sana ikiwa Tume ya Jaji Warioba itakaa kimya kutokemea au kuwachukulia hatua wale wote wanaotoa vitisho dhidi ya watu wenye mitazamo na maoni tofauti kuhusu Katiba mpya.

Alisema kila mtu yuko huru kutoa maoni yake mbele ya Tume na si haki kwa mtu au Chama chochote cha siasa kuwalazimisha wanachama wake kutoa maoni ambayo hayatokani na mitazamo yao binafsi. Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT) Zanzibar , Asha Bakar Makame amewataka viongozi wenzake ndani ya CCM kutowatisha wanachama wanaotoa maoni wasiyoyapenda.

Akichangia katika semina hiyo, Makamu huyo Mwenyekiyi ambaye ni Mwakilishi wa Viti Maalum alisema ni jambo la kushangaza katika ukuaji wa demokrasia wakajitokeza watu kuanza kuwazuia wengine kuwa na mawazo huru kwenye mchakato wa kupata Katiba mpya.

“Jamani tusitishane, kama CCM kila mtu ni CCM hapa, hakuna mtu asiyenijua msimamo wangu kuhusu Chama ninakipenda na nitakitetea,lakini si vizuri kuanza kutishana kwa kuambiana huyu hivi huyu vile haifai jamani” Alisema Makamu Mwenyekiti UWT.
Makamu huyo Mwenyekiti wa UWT alikumbusha kwamba wakati wa kutafuta maridhiano ya kisiasa Zanzibar wapo wana CCM na Viongozi waliopinga suala hilo ,lakini hakuna mtu aliyeadhibiwa, hivyo aliwataka kuvumilia katika suala zima la maoni tofauti kuhusu Muungano.

“Wakati tunakwenda kwenye kura ya maoni mwaka 2010 wapo wenzetu wengi walipinga, tena walikuwa wakijulikana,lakini hakuna mtu aliyetiwa adabu na Chama ingawa msimamo wa kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ulikuwa ni maamuzi ya Chama chetu tulikutana Butiama na Dodoma tukakubaliana…mbona hakutiwa adabu mtu” Alihoji Asha Bakar.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura(CCM),Hamza Hassan Juma alisema Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Kikwete hajazuia kutoa maoni tofauti isipokuwa aliwataka wananchi kuvumiliana maana kila mtu atakuwa na maoni yake.
“Mimi nampongeza sana Mwenyekiti wetu,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa siku ile akizundua Tume pale Ikulu, alisema kama wewe uyapendi mawazo ya mwenzio na yako pia kuna wasiyoyapenda,lakini la muhimu kustahamiliana” Alisema Mwakilishi huyo.

Hamza aliongeza kwamba CCM ni Chama bora na kamwe hakiogopi mageuzi na ndio maana hata mageuzi ya kisiasa mwaka 1992 ilisimamia vema na nchi ikaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, hivyo hata katika suala la maoni kuhusu Muungano halitakuwa na matatizo maana wananchi wako huru kutoa maoni yao .

Mimi naona utoaji maoni wa Kusini Unguja urudiwe kwani hakukufanyika uadilifu na CCM ambayo inadai demokrasia, imekiuka sera yake hiyo huku ikiwashutumu wengine kuwa wanakiuka sera za CCM.
 
Back
Top Bottom