Viongozi wawili wa chadema watishiwa maisha

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Josephat Isango- Mwenyekiti wa baraza la Vijana wa CHADEMA, Mkoa wa Singida, na Patrobas Paskali Katambi Mwenyekiti wa Chama wa tawi la St. Augustine University wametishiwa maisha katika matukio tofauti.
Josephat Isango, ameitishiwa kuuawa na Diwani wa kata ya Unyambwa, Shaban Salimu Sattu (CCM), baada ya kutoa taarifa polisi kuwa diwani huyo amesaidia watu mbalimbali akiwemo mke wake na mdogo wake, na mke wa jirani yake ambaye inadhaniwa kuwa ana uhusiano na diwani huyo pamoja na watu kadhaa kujipatia isivyo halali (kwa njia haramu) malipo ya pesa taslimu 54,000,000/-. Pesa ambazoa zilipaswa kuwa za fidia kwa watu watakaohamishwa, Diwani huyo amefikishwa mahakamani Singida mjini leo, amekana shitaka na yupo nje kwa dhamana hadi tarehe 5/June/2012.. Pamoja na kuripotiwa Wizi huo wa Shilingi 54,000,000/- Jeshi la polisi mkoani Singida limenyamazishwa kuhusu wizi huo ulioripotiwa tarehe 30/04/2012, na kuendelea kumlinda Diwani huyo aliyejipatia kitita kikubwa katika sakata hilo.
Kwa upande wa Patrobas Paskali, jana baada ya kutoka katika kipindi cha tuongee asubuhi katika kituo cha televisheni Star Tv. Kilichopo ilemela mwanza, alichukuliwa na gari ya Star TV hadi Nyegezi maeneo ya Nganza, aliposhushwa katika gari ya Star TV, na kuanza kutembea kuingia kwake alitekwa na kushikiliwa na kuhojiwa kwa nusu saaa na Njemba zilizokuwa na gari aina ya Noah , iliyokuwa na namba za Chasis, iliyoanzia na SX 212…………. na kuonywa kuwa anachafua serikali, na kusema kuwa Rais ameshindwa kuongoza nchi, watu kadhaa walijitokeza katika njia hiyo na kusababisha Patrobas kuachiwa haraka na hao watu kukimbia na Diary ya Patrobas. Mwenyekiti huyo alinyang’anywa Diary tu na kung’ang’ania begi lililokuwa na laptop na alishindwa kukariri namba zote za chasis zilizoandikwa katika gari hilo. Tukio hili limeripotiwa leo polisi, mkoani mwanza kwa MW/RB/5207/2012, JALADA LA UCHUNGUZI.
Huku ndiko tunakoelekea?
 
Magamba wanahangaika lakini hawawezi kuzuia wimbi la mabadiliko mwenye hofu yoyote na mbinu hizi za kitoto; asihofu maana nguvu za kishetani zinazowaongoza hao lakini watashindwatu, kwasababu shetani ni kiumbe hawezi kushindana na nguvu za muumba ambazo ziko nyumba ya wimbi la mabadiliko. Mungu ameikumbuka Tanzania la lazima aikomboe kupitia Watanzania jasiri. KWA JINA KUU LA YESU KRISTO MAGAMBA LAZIMA WABWAGWE
 
Yote yana mwisho, haijalishi vitisho! Siku tunakapochoka kuyasikia haya manyanyaso nafikiri hawataamini kuwa watz ni mashujaa walio tulia. Nachotaka kuwaambia hawa waonezi CCM, MSIMCHOKOZE SHUJAA ALIYETULIA
 
CCM ni Chama Cha Magaidi, hata yale makanisa kule Zanzibar ni CCM ndiyo waliyoyalipua.
 
Watahangaika sana lakini mwisho wa siku nguvu ya umma itashinda tu..!
 
Vitisho vipo kila kona ya nchi, mimi pia nimeshaonywa kwamba niache habari ya kukosoa serikali na kusifia Chadema, lakini niseme tu kwamba ukiona mtu anaanza kutoa vitisho ujue kesha zidiwa na sasa ccm imeshaona kwamba huko mbele ni giza nene kwao. tusife moyo, nchi hii ni yetu sote na hakuna mtu mwenye hati miliki ya kuiongoza yeyote yupo huru kuiongoza na hata vyama hakuna chama chenye hati miliki ya uongozi, chama chenye dira na dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo ndicho chenye haki ya kuongoza na kwa sasa chama hicho ni Chadema, ccm ni wasanii tena wahalifu wakubwa.
 
Poleni makamanda ni muda wa kukaza buti... wameshachoka hao, Mwigulu si alikuwa huko?
 
kwa wasomaji wa riwaya- the grain of wheat inamaana hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom