Viongozi walioboronga zaidi 2011; Tuwajadili...

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,968
William Ngeleja, Said Mwema, Anne Makinda wameonyesha uwezo mdogo sana katika kazi zao, je walipewa wa Merit?

Ngeleja amechemsha sana katika anga zifuatazo;
1. Nchi imekuwa katika mgao wa umeme kwa mwaka mzima 2011
2. Tanesco yake imeshindwa kesi na inajiandaa/ huenda imeshaanza kuilipa Dowans
3. Alishindwa kabisa kudhibiti uchakachuaji mafuta hadi kulazimika kupandisha bei ya mafua ya taa na kuumiza walalahoi
4. Alijaribu kumbeba Jairo kupitia mbeleko iliyochanika (Luhanjo)
5. Alichota mahela kibao TPDC kwenda ulaya kula bata ( Kamati ya bunge ilieleza)
6. Ameendelea kukumbatia mikataba feki ya madini

Said Mwema kachemsha katika anga hizi
1. Jeshi lake limetajwa na TAKUKURU kuwa ndio taasisi inayoongoza kwa rushwa nchini (pengine duniani)
2. Ajari za barabarani zimekuwa nyingi kiasi kwamba kwa sasa tumeishazizoea, latest ni Biharamulo watu 20 wameteketea
3. Bajeti ya mabomu ya machozi katika jeshi lake imemaliza kifungu chote cha overhead costs
4. Jeshi linaongoza kwa kubambikiza kesi huku wananchi wakiitwa panya
5. Jeshi lake limeua raia wengi sana mwaka 2011 wasio na hatia
6. Askari wake wanakaa katika nyumba mbovu sana na wanavaa uniform zilizochakaa

Anne Makinda amechemsha katika anga zifuatazo;
1. Amekuwa wakala wa serikali badala ya kuisimamia bungeni, haijui doctrine of separations of power
2. Amegoma kabisa kutupatia utetezi wa Mh Lema kuhusu Mh Pinda kulidanganya bunge
3. Inapokuja ishu inahitaji uongozi imara na makini kama katiba yeye anachekacheka tu (Kama JK)
4. Hajatuletea wapigakura wake jimboni muswada wa katiba tuujadili (Uliposomwa first time)
5. Alitukanwa na Six kuwa kawekwa na mafisadi hadi leo hajakanusha
6. Kageuza bunge kuwa kijiwe cha stori badala ya baraza la kutunga sheria

Wapo viongozi wengi walioboronga 2011, ila hawa naona wamezidi. Tunapouaga huu mwaka ni vizuri kuwaeleza ili wajirekebishe au kujiuzulu ikibidi.
 
Malima amesema hajiudhuru ng'o, amedai bunge halikumteua kuwa naibu waziri
 
1. Lema..kitendo cha kujipeleka gerezani kimemdhalilisha yeye, familia yake na CDM kwa ujumla.
2. Slaa..baada ya uchaguzi ameishiwa kabisa sera! Sera yake ya ufisaidi haina tena nguvu. Amekuwa tu kama raia wa kawaida, mvuto kisiasa umeporomoka kwa kasi ya ajabu.
 
Celine Kombani...
  1. Aliwai kusema Katiba haitaji kuandikwa tena ipo poa...baadae akasema nilikuwa natikisa kiberiti nione..kaharibu mchakato wa katiba mpya..
AG Warema..
  1. Kukubali kuburuzwa na magamba kwa kila kitu..hasa kwenye mswada wa kuandika katiba mpya...
 
Semeni woteeeeee ila Baba lao ni Dr Dr Dr Dr Dr Jakaya Kikwete...huyu ndio baba yao...
 
1. Lema..kitendo cha kujipeleka gerezani kimemdhalilisha yeye, familia yake na CDM kwa ujumla. 2. Slaa..baada ya uchaguzi ameishiwa kabisa sera! Sera yake ya ufisaidi haina tena nguvu. Amekuwa tu kama raia wa kawaida, mvuto kisiasa umeporomoka kwa kasi ya ajabu.
Sawa pacha wa Livingstone Lusinde...
 
1. Lema..kitendo cha kujipeleka gerezani kimemdhalilisha yeye, familia yake na CDM kwa ujumla.
2. Slaa..baada ya uchaguzi ameishiwa kabisa sera! Sera yake ya ufisaidi haina tena nguvu. Amekuwa tu kama raia wa kawaida, mvuto kisiasa umeporomoka kwa kasi ya ajabu.
Nimeskia kuwa Dr Slaa yuko busy kujenga chama ngazi ya wilaya na vijiji ili kupata ushindi wa kishindo 2015. Pia anastahili pongezi kwani chama chake kimeimarika sana mwaka huu, hasa ule usemi wa PIPOOZ PAWA ambao Pinda kasema unamnyima usingizi
 
JK...... hajawahi kuwa Rais na napata ugumu sana hata kujua km kweli JK anajua maana ya TAASISI YA URAISI - naamini mnajua namaanisha nn..... Wote waliotajwa na watakaotajwa ni kwa sababu ya huu ushindwaji wa hali ya juu sana!
 
Kikwete ndo kinara wa kuboronga kwa kila kitu,ukianza kuelezea uovu wake mpaka kesho utakuwa unaandika.
 
Father of all kuborongas ameishajadiliwa sana humu na inaonekana hana mpango wowote wa kujirekebisha. Hebu tujaribu kurekebisha walio chini yake huenda wakabadilika. Au nao wanaweza kuja na ujanja wa kuita wazee wa majimboni mwao na kuwalisha pilau ili wawapigie vigeregere kufunika uoza wao.
 
Makinda kawekwa na Mafisadi, unategemea atafanya nini kuwasaidia wananchi zaidi ya kuwafurahisha maBwana zake? kazi kuchekacheka tu utafikiri msichana aliyeko shule ya wasichana mission asiyeruhusiwa kukutana na wavulana.
 
Mjinga wewe!Sera ya kupinga ufisadi ni endelevu,kwani nani kakudanganya ufisadi umekwisha?Huyo KIKWETE wako ndio umaarufu wake umeporomoka,amebaki kama raia wa kawaida kabisa!!!!!!!
 
Back
Top Bottom