Viongozi,wabunge walijipendelea na kutoa rushwa kwa majaji, tume ya uchaguzi katika katiba ya 1977

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
NDUGU WANA JF KWA KUWA HIVI SASA TUPO KATIKA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA NI VYEMA TUAKATUMIA MUDA MWINGI KUJISOMEA KATIBA YA SASA ILI KUBAINI MAPUNGUFU YALIYOMO KWA LENGO LA KUTOA MAONI YETU ILI MAPUNGUFU HAYO YAWEZE KUREKEBISHWA BADALA YA KUTUMIA MUDA WETU MWINGI KUSHIRIKI PROPAGANDA MBALI MBALI KUTOKA PANDE ZOTE ZISIZOWEZA KUTUTALIA MATATIZO YETU.

KATIKA KUPITIA KATIBA YA SASA NILISHANGAZWA SANA NA JINSI BAADHI YA VIONGOZI WAKIWEMO WABUNGE WALIOPITISHA KATIBA HII MWAKA 1984 WALIVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAO ZA UONGOZI KUJIFIKIRIA WAO BINAFSI NA KULINDA MISHAHARA NA POSHO ZAO KUPITIA IBARA 142 HAPO CHINI.

NILISHANGAZWA PIA NA UKWELI KUWA SERIKALI A MITAA AMBAKO ZAIDI YA 99% YA WATANZANIA WANAISHI (TUKIWATOA HAWA WACHACHE WALIOJIHAKIKISHIA MISHAHARA NA POSHO KUPITIA IBARA 142) WALIVYOPUUZWA NA BUNGE LILILOPITISHA HII KATIBA MBOVU KWA KUWEKA MASLAHI MACHACHE SANA KWA WANANCHI WANAOISHI KATIKA SERIKALI ZA MITAA KATIKA IBARA YA 145 HAPO CHINI.

NAOMBA KUWASILISHA

Mishahara ya watumishi fulani wa Serikali kudhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali Sheria ya1984 Na.15 ib.43 IBARA YA 142
.-(1) Watumishi wa Serikali wanaohusika na masharti ya ibara hii watalipwa mishahara na posho kama itakavyoelezwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Fedha za malipo ya mishahara na posho za watumishiwa Serikali wanaohusika na masharti ya ibara hii pamoja na
fedha za malipo ya uzeeni na kiinua mgongo kwa wale wanaostahili malipo hayo miongoni mwa watumishi hao zitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

(3) Mshahara anaolipwa mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya ibara hii pamoja na masharti yake ya kazi
havitabadilishwa, baada ya mtumishi huyo kuteuliwa, kwa jinsi ambayo itapunguza masilahi ya mtumishi huyo, lakini maelezo haya hayahusiki na posho anayolipwa mtumishi huyo.

(4) Iwapo mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya ibara hii ana hiari ya kuchagua kima cha mshahara au aina ya masharti ya kazi, basi kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii, mshahara wa kima hicho atakachochagua na aina hiyo ya masharti ya kazi atakayochagua vitahesabiwa kuwa vina masilahi zaidi kwake kuliko kima cha mshahara kingine chochote angalichoweza kuchagua au aina ya masharti ya kazi nyingine yoyote angaliyoweza kuchagua.

(5) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Mwenyekiti na kila Mjumbe wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi, na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.

Serikali za Mitaa Sheria ya 1984 Na.15 ib.50 IBARA YA 145.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katika
kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano, ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.

(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.

146.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za
Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa
maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.

(2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na shughuli zifuatazo -
(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo lake;
(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi; na
(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.
 
Back
Top Bottom