Viongozi wa Zanzibar Hamlioni hili

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]Written by Awami // 29/11/2011 // Habari // 1 Comment

leo inakuwaje Tanganyika wanapiga dane dane kutia saini inapokuja kutumika kwa Ardhi yao ambayo wao wenye wanasema ni kubwa kupitia hata mahitajio yao ,sasa hapa hapataki roketi sayansi mtu kutambuwa kuwa hawa watu ni mafasiki na wenye uaduwi mkuwa ndani ya nafsi yao inapofika kuifanyia zulma Zanzibar tujiulize kwanini wakatae nawao ndio wenye kupenda mambo yakunganisha ?
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amegoma kusaini mikataba ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) unaohusu sera za ardhi, ulinzi na mambo ya nje.Sitta ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC unaofanyika hapa Burundi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa suala hilo wamelikataa ili lirejeshwe kwa wakuu wa nchi kwa uamuzi.
Hali hiyo ilifanya mkataba huo kusainiwa na nchi nne tu za Afrika ya Mashariki, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda hivyo kuiacha nafasi ya saini ya Tanzania kubakia wazi.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Stragomena-Tax Bamwenda alisema jambo hilo ni nyeti, lakini akaweka bayana kuwa ujumbe wa Tanzania utapaswa kutoa taarifa kwa baraza kufafanua msimamo wao.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Lazaro Nyalandu aliweka wazi kwamba suala la ardhi halipaswi kuwa sehemu ya EAC.Alionya kwamba kuna mazingira yanayoashiria kuwa baadhi ya wajumbe wa nchi za jumuia hiyo wamekuwa wakiangalia ardhi ya Tanzania kwa jicho la husuda.
Mbunge huyo wa Singida Kaskazini alisema Tanzania ina ardhi kubwa ambayo inawapa nafasi Watanzania kuchagua eneo la kwenda kuishi.Lakini akasisitiza kuwa ardhi hiyo lazima ibakie kwa ajili ya Watanzania na vizazi vijavyo.
Tanzania imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wanachama wa Jumuia kwa msimamo wake kuhusu ardhi hivyo kukwamisha juhudi za kuimarisha EAC.
 
Attachments

  • ;ll.png
    ;ll.png
    48.3 KB · Views: 28
Hii Taarifa ina makosa kibao ya kiuandishi
Tangu lini Lazaro Nyalundu amekuwa naibu Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki?
 
Written by Awami // 29/11/2011 // Habari // 1 Comment

leo inakuwaje Tanganyika wanapiga dane dane kutia saini inapokuja kutumika kwa Ardhi yao ambayo wao wenye wanasema ni kubwa kupitia hata mahitajio yao ,sasa hapa hapataki roketi sayansi mtu kutambuwa kuwa hawa watu ni mafasiki na wenye uaduwi mkuwa ndani ya nafsi yao inapofika kuifanyia zulma Zanzibar tujiulize kwanini wakatae nawao ndio wenye kupenda mambo yakunganisha ?
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amegoma kusaini mikataba ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) unaohusu sera za ardhi, ulinzi na mambo ya nje.Sitta ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC unaofanyika hapa Burundi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa suala hilo wamelikataa ili lirejeshwe kwa wakuu wa nchi kwa uamuzi.
Hali hiyo ilifanya mkataba huo kusainiwa na nchi nne tu za Afrika ya Mashariki, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda hivyo kuiacha nafasi ya saini ya Tanzania kubakia wazi.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Stragomena-Tax Bamwenda alisema jambo hilo ni nyeti, lakini akaweka bayana kuwa ujumbe wa Tanzania utapaswa kutoa taarifa kwa baraza kufafanua msimamo wao.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Lazaro Nyalandu aliweka wazi kwamba suala la ardhi halipaswi kuwa sehemu ya EAC.Alionya kwamba kuna mazingira yanayoashiria kuwa baadhi ya wajumbe wa nchi za jumuia hiyo wamekuwa wakiangalia ardhi ya Tanzania kwa jicho la husuda.
Mbunge huyo wa Singida Kaskazini alisema Tanzania ina ardhi kubwa ambayo inawapa nafasi Watanzania kuchagua eneo la kwenda kuishi.Lakini akasisitiza kuwa ardhi hiyo lazima ibakie kwa ajili ya Watanzania na vizazi vijavyo.
Tanzania imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wanachama wa Jumuia kwa msimamo wake kuhusu ardhi hivyo kukwamisha juhudi za kuimarisha EAC.
Asante sana kakke kwa kunisaidia hapo kwenye red,kila siku nilikuwa najiuliza hivi nani aliivunja na kuiua Tanganyika wakati Zanzibar bado inapatikana,kumbe Tanganyika yetu bado ipo asante kwa taarifa,sasa huko kwingine kaka kumbe Samwel Sitta anapotaka kutia saini katika mkataba huo wa jumuiya ya Afrika Mashariki ni kwa ajiri ya Watanganyika peke yao enhh??? nalo sikulifahamu nashukuru kwa kunifahamisha,swali langu je nyinyi Wanzanzibar katika mkataba huu wa jumuiya ya Afrika Mashariki nani kawatilia saini?

Inashangaza kuona Mzanzibari akilalamikia kulindwa kwa ardhi ya Tanganyika; wakati yeye ana uhuru wote wakuishi na kuitumia ardhi hiyo bila kikwazo chochote. Hivi ni lini Mzanzibari akiweka makao yake ya kuishi Mwanza au Mkoa wowote Tanganyika akatakiwa kupata vibali??? Chuki zingine hazina maana wala tija!!
 
Kakke yumkini unataka kusema kitu lakini hukujipanga vizuri...halafu wandugu chonde na mabandiko ya "sisi Wazanzibar" au "wao Watanganyika" Mwalimu keshamaliza...
 
Back
Top Bottom