Sitaki kuamini kuwa wagonjwa wanateseka muhimbili, na ocean road kwa ajili ya mgomo wa madaktari. Sitaki kuamini kuwa serikali imeshindwa kuwatekelezea mahtaji yao. Suala la posho kwa madaktari ndio watanzania wanaambiwa hakuna pesa, ila posho bungeni ziliongezwa hata bila ubishi. Kwa wabunge pesa zipo ila taasisi zingine mpaka wagome. Sitaki kuamini kuwa serikali imeshindwa kutatua tatizo hili na kusababisha watu wafe. Siamini zaidi kusikia kuwa mkuu wa nchi naye ameamua kusafiri huku hali hiyo ikiendelea wakati suluhisho likiwa halijapatikana. Mkuu wa nchi anafurahia ziara, wagonjwa katika nchi yake wanakufa........ Siamini. Inakatisha tamaa nchi yetu