Viongozi wa serikali watembelea CCP Moshi kwa siri

Kamende

JF-Expert Member
Mar 1, 2008
416
45
Habari zilizofika mezani hivi punde kutoka kule Moshi zinasema kuwa viongozi wa ngazi za juu serikalini hasa Mawaziri bila kujali wizara zao wamekuwa wakitembelea Chuo Cha Polisi cha mjini Moshi kuongea na wanafunzi wanaochukua mafunzo ya upolisi mambo nyeti.

Katika mambo wanayoshawishiwa kuyajua askari hao wanafunzi ni umuhimu wa kukilinda Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha kuwa wanawatumika kuvibana vyama vya upinzani ili CCM iweze kushinda chaguzi zinazikuja.

Waziri mmoja aliyekuwa Moshi mapema mwezi huu wa Januari aliwaasa askari hao wanafunzi kuwa wasifanane na hawa askari wa zamani ambao wamebadilika fikra zao zikawa za kiraia. (Maana alifafananua kuwa wapo askari wanaovujisha siri kwa vyama vya upinzani na pia wanaokataa kabisa kuisaidia CCM kushinda chaguzi zinazoikabili. Mfano aliotoa ni uchaguzi mdogo wa Tarime).

Zawadi ambayo askari hao wanafunzi wamehakikishiwa ni kupewa cheti cha askari wa kimataifa. "Hao wenzenu waliowatangulia wana vyeti vya hapa hapa nchini. Nyinyi tutawapa vyeti vya kimataifa"

Depo yote ya sasa na pengine mbili zijazo zitaingizwa FFU kwa lengo hilo hilo la kuimarisha mashambulizi dhidi ya wapinzani.

Jamani bado viongozi wetu hawajafumbuka macho waone kile watanzania wanachoona. Hawataki kuongoza kwa kupendwa. Wanataka kuendelea kutumia nguvu. Hakika ya Zimbabwe yanainyemelea Tanzania.
 
Serikali haiitaji kusumbuka kwenda Moshi kuongea na kuruta.Wao wasubiri tuu hao makuruta wakiwa maaskari watoe amri kuwa kila askari aipigie kura CCM au ahakikishe kuwa CCM inashinda.Mbona linawezekana hilo.Manake watamalizia kwa kuitikia "Ndio Afande" na salute juu.
 
Wanacheza hao...sio vijana wa sasa....

Hivi zile kambi za vijana za kuwalisha sumu za ukada pofu zimeshaanza?

Tanzanianjema
 
Hii bado tetesi, kama kuna ushahidi ndio tuanze kuchambua...

Mhalifu mwenye akili anajtahidi sana kutoacha ushahidi ili usimchambue. Lakini hii si hadithi mpya, ni kawaida makada wa CCM kutembelea majeshi ya ulinzi na usalama kuwakumbusha wajibu wao wa kukifanya chama tawala kishinde, same story UWT, idara za serikali na sehemu nyingi tu. Kama ujinga uliuokuwepo miaka iliyopita utaendelea, basi watu watakubali.
 
Kama habari hii ni kweli ni vizuri watajwe majina yao ikithibitika basi hilo liitwe jeshi la CCM na vyama vingine navyo vianzishe majeshi yao.Mtu msafi haangaiki kwani wanamjua ila kibaya kitajitembeza.Askari muwe wadau muhimu wa kuilinda nchi dhidi ya mafisadi.
 
In intelligence business never ever neglect any romours because what is a romour today may & only may be a real situation tommorow.

Wanajamii tuifatilie hii taarifa ili kupata uhakika wake na hapo ndio tupate pa kuanzia kusema
 
Back
Top Bottom